Friday 5 July 2013

Uislamu na Khilafah



Allah (S.W) amekwisha leta khilafah (yaani utawala wa kiislamu unaohukumu kwa maelekezo ya Qur’an na Sunnah za Mtume) nayo ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambayo ina umri wa miaka 33 tokea ilipoasisiwa na Ayatollah Imam Khomaini (R.A).
Ni  jukumu la waislamu wote duniani kumtii na kula kiapo cha utii kwa kiongozi / Imam Mkuu wa Jamhuri hiyo, ambaye kwa sasa anaitwa Ayatollah Ally Khamenei (R.A), ndipo dunia itasalimika kutokana na dhulma na fitina za Makafiri na vibaraka wao.
Hii ndio itakuwa sawa kwani si jukumu la Iran kuwalazimisha watu waitii au kuifuata kama baadhi ya waislamu wanavyodai kuwa khilafah inatakiwa kuwalazimisha watu waitii, bali ni jukumu la watu wenyewe waitafute haki na kuifuata. Watu wenyewe wanatakiwa kuitii mamlaka inayotawala kwa misingi ya Allah na Mtume wake. Jukumu la jamhuri ya kiislamu ni kuwaelimisha watu wautambue Uislamu kuwa ni dini inayojiendesha yenyewe kwa sheria toka kwa Allah na kwamba dola hiyo tayari inatekeleza jukumu hilo.
Kwani Mtume Mohammad (S.A.W) hakupigana vita yoyote kwa ajili ya kuweka utawala wa kiislamu, isipokuwa aliwanasihi na kuwaelimisha watu wajue ubora wa kuishi chini ya utawala wa kiislamu. Japokuwa watu wa Makkah walimpinga kwa nguvu zote, Mtume hakuchukua silaha hata mara moja kupambana nao. Hatimaye watu wa Madinnah walielewa na kuukubali Uislamu wenyewe bila Mtume kuweko Madinnah kisha wakaunda tume ya kwenda kumleta Mtume aje kuwaongoza.
Watu hawa walikwenda kwa mara ya kwanza lakini Mtume alitaka kujua kama kweli wameamua wenyewe kwa makini au wamekurupuka kuukubali Uislamu. Hivyo Mtume aliwaapisha, nao wakaapa kwa jina na Allah na wakaahidi kuwa watamlinda pindi Mtume atakapokwenda kuwaongoza huko Madinnah. Hata hivyo Mtume hakukubaliana nao, hivyo akawaambia warudi Madinnah peke yao na kwamba yeye ataendelea kuwepo Makkah licha ya Mauaji na mateso yaliyokuwa yakifanywa na Makafiri dhidi ya waislamu.
Mwaka uliofuata watu wa Madinnah walirudi tena kwa Mtume, tena wakiwa wengi kuliko wale wa mwanzo, wakamuomba Mtume ahamie Madinnah. Bado Mtume alitaka kujua kama kweli wanadhamira ya kweli juu ya Uislamu, hivyo aliwaapisha kwa mara ya pili. Nao wakaapa na kuahidi kuwa pindi Mtume atakapokwenda kuwaongoza huko Madinnah, watajitolea kwa hali na mali ili kuhakikisha kuwa Uislamu umeshika hatamu. Ndipo Mtume aliridhika hivyo akawaagiza waende kujiandaa na yeye atawafuata baadaye. Mtume alipohamia Madinnah dola la kiislamu lilianza bila kulazimishwa mtu hata mmoja kulifuata.
Kwa hiyo waislamu waache kumwaga damu za watu kwa kisingizio cha kuweka khilafah kwani tabia hiyo si faradhi wala si sunnah ya Mtume bali ni haramu. Na Allah (S.W) amewaandalia adhabu kubwa watu wote wanaoua watu wasiokuwa na hatia ya kisheria.
(hii ni ndioto niliyoiota mimi Rajabu Shaban Kabavako, kwa mawasiliano nipigie kwa 0782721814)