WAATHIRIKA WA KARBALA – AWN BIN JAAFAR IBN ABI TALIB (R.A)
Aun ni mtoto wa Jaafar ibn Abi Talib (r.a) na Asma’a bint
Amees (r.a)..
Alizaliwa ukimbizini Ethiopia (Uhabeshi) kwani baba yake
yaani Jaafar alikuwa kiongozi wa wakimbizi wa kiislamu waliokimbilia Habash
kutokana na dhuluma na mauaji waliokuwa akifanyiwa na makafiri wa Makkah wakati
wa mwanzo wa Uislamu kutangazwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Uislamu ulipota nguvu baba wa Aun yaani Jaafar alirejea
uarabuni na kwa kipindi hicho Mtume alikuwa amekwisha hamia Madinah. Miaka michache
baadaye Jaafar aliongoza jeshi la waislamu katika mapambano yanayojulikana kama
vita vya Mu’tah. Vita hivi vilikuwa vikali sana na waislamu wengi waliuawa
ikiwa ni pamoja na kamanda wao, yaani Jaafar bin Abi Talib (r.a). Jaafar aliacha
watoto wa kiume watatu yaani Awn, Muhammad na Abdullah.
Vijana hawa walifanana sana na mzee Abu Talib (r.a), hivyo
Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Imam Ally waliwapenda sana. Baadaye Imam Ally
aliwaozesha mabinti wake. Ummu kulthumu aliolewa na Aun na Zainabu aliolewa na
Muhammad. Hapa utagundua kuwa wale wanaosema kuwa Imam Ally waliwaozesha mabinti
wake kwa Umar bin Khatab ni uongo na propaganda kwa minajiri ya kuwapotosha
watu.
Awn aliendelea kuwa Mtiifu kwa Imam Ally kama imam wake wa
kwanza, kisha akawa mtiifu kwa Imam Hassan kama imam wake wa pili na hatimaye
akawa mtiifu kwa imam Hussein kama imam wake wa tatu. Awn alichinjwa pamoja na
Mashia na Ahlulbayt wengine katika eneo la Karbala, Iraq, akipigana vita upande
wa Mashia, yaani katika jeshi dogo la imam Hussein (a.s). Innalillahi wainna
ilayhi rajiuun.
Source: Ashura Encyclopedia
By Jawad Muhaddithy
No comments:
Post a Comment