MAWAHHABI WAMDHALILISHA
MTUME KUWA HAKUJIELEWA KUWA YEYE NI MTUME
Waandishi wa kiwahhabi wameeleza suala la
mwanzo wa wahyi kwa njia nyingi tofauti zenye kugongana. Tunakusudia kudondoa
kilitokea nini kwa Mtume Muhammad (sa.w.w) baada ya kufikiwa na malaika Jibril
kwa mara ya kwanza. Hapa tutajaribu kuzitaja chache tu:
a. Khadija na Abubakr walimpeleka Muhammad
(s.a.w.) kwa Waraqa bin Nawfal baada ya kuelezwa Waraqa kuwa Muhammad amepata
matatizo, Waraqa akamuuliza Muhammad ana nini? Muhammad (s.a.w.) akamwambia:
"Ninasikia ninaitwa nyuma yangu, ewe Muhammad, ewe Muhammad, nikisikia
hivyo mimi hukimbia ovyo." Waraqa akamkataza asiwe anakimbia bali akaze
roho ili ayasikie anayoambiwa..." Muhammad alishika maelekezo hayo, mara
aliposikia akiitwa: Ewe Muhammad! Sema, Bismillahir Rahmanir Rahim,
Alhamdulillahi rabbil a'lamina.... mpaka mwisho wa suratul Fatiha. Akaambiwa:
Sema: "Laa ilaha illallahu" Muhammad (s.a.w.) baada ya hapo alikwenda
kwa Waraqa bin Nawfal, akamjulisha hali hiyo. Waraqa akambashiria habari njema
ya kuwa: "Hali kama hiyo alipewa pia Nabii Isa bin Maryam".
Tazama; Albidayatu Wannihaya J. 3 Uk. 9, Assiratun Nabawiyya J. 1 uk 83,
Assiratul Halabiyya J. 1 uk 250, Siiratu Mughlataya uk, 15.
b. Khadija alipompeleka Muhammad (s.a.w.) kwa
Waraqa na akamweleza yaliyomtokea. Waraqa alisema: "Huyu ni Nabii wa Umma
huu, mwambie atulize moyo."
Tazama: Albidayatu Wannihaya J.3 uk, 12, Siiratu Ibn Hisham J. 1 uk. 238,
Assiratul Halabiyya J. 1 Uk. 239.
c. Khadija alimwambia Muhammad (s.a.w.)
atakapokufikia huyo anayekusomesha, uniambie, Mtume (s.a.w.) alipofikiwa na
hali hiyo akamjulisha mkewe. Khadija akampakata katika mapaja yake, kisha
akavua shungi yake, mara Mtume (s.a.w.) akaona yule aliyemjia anaondoka haraka.
Mtume akamjulisha mkewe hilo, Khadija akasema, "Huyo ni Malaika, na wala
siyo shetani, basi kaza roho na furahi".
Tazama: Assiratul Halabiyya J. 1 Uk. 252.
d. Waraqa bin Nawfal alimwambia Khadija:
"Muulize Muhammad (s.a.w.), nani anaemjia! Ikiwa ni Malaika Mikaeli basi
amemletea amani. Na ikiwa ni Malaika Jibril basi amemletea vita na mateka.
Khadija Alipomuuliza Mtume (s.a.w.) akajibu: "Ni Jibril". Khadija
akapiga uso wake.
Taz: Tarikhul Yaa'quby J. 2 Uk. 23.
e. Khadija alipewa kipande cha karatasi na mganga
mmoja ili ampe Muhammad (s.a.w.) kama hali hii (iliyomfikia Muhammad)
inasababishwa na ugonjwa wa kichaa, basi atapona... Khadija aliporudi kwa
mumewe akamkuta anasoma Qur'an, Khadija akamchukua akaenda naye kwa yule
mganga, walipofika kwa mganga, akafunua mgongo wa Mtume akaona muhuri wa Utume
uko kati ya mabega mawili!!!
Tazama: Tarikhul Khamisi J. 1 Uk. 284, Assiratul Halabiyya J. 1 Uk. 243,
Assiratun Nabawiyya J. 1. Uk. 83.
f. Muhammad (s.a.w.) alipofikiwa na hali hiyo (ya
kujiwa na Malaika) alikuwa akipanda katika kilele cha mlima mrefu na akitaka
kujitupa chini (ili afe).
Tazama: Almuswannaf J. 5 Uk. 323.
g. Muhammad (s.a.w.) alirudi kwa mkewe (kutoka
katika pango) akiwa nafuraha kubwa akamwambia mkewe: "Nataka kukueleza
habari njema, mimi nimeona katika ndoto kuwa Jibril amenijulisha kwamba
ametumwa na Mola wangu aje kwangu... Khadija akamwambia: "Furahi, wallahi
Mwenyeezi Mungu hatakufanyia lolote ila lililokuwa la kheri... kisha Khadija
akaenda kwa mganga wa kinasara, kuuliza uwezekano wa kumuona Jibril. Mganga
alishangaa sana kusikia jina la Jibril katika nchi hiyo, kisha akasema kuwa:
"Huyo ni Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu..."
Taz: Albidayatu Wannihaya J. 3 Uk. 13.
Nadhani
umejionea mwenyewe uzushi wa mawahhabi, masalafi na answari sunnah dhidi ya
Mtume wetu. Watu waongo na wazushi kama hawa, hawawezi kuaacha waislamu wa
kawaida wakiishi kwa amani mustarehe bila kuleta chokochoko.
Lakini sisi
waislamu sahihi, yaani Mashia tunaamini kuwa Mtume alikuwa Mtume bado akiwa
tumboni mwa mama yake. Hivyo alipozaliwa tu alijulikana kuwa ni Mtume na
miujiza mingi ilifanyika katika utoto wake na ujana wake. Kabla ya kufikisha
miaka 40 ambapo utume wake ulizinduliwa rasmi na kuanza kazi ya kuueneza
Uislamu duniani.
No comments:
Post a Comment