BI KHADIJA, MADHULUMU WA HISTORIA
Bibi Khadija alikuwa ndiye mke wa kwanza wa Mtukufu
Mtume. Bibi huyu alikuwa tajiri miongomi mwa matajiri wakubwa wa Makka. Mtume
alikuwa na miaka 25 alipomuoa bibi huyu, aliopofikisha miaka 40, alitoa tangazo
la kwanza la utume wake, mtu wa kwamza kuamini utume wake alikuwa ni bibi
Khadija, na hivyo kuamini Upweke (tawhid) wa Allah swt. Na kuwa Mwislamu wa
kwanza ulimwenguni.
Waabudu masanamu wa Makka hawakufaurahishwa na tangazo
hili, ukazuka uadui mkubwa sana kati ya Mtukufu Mtume na waabudu masanamu hawa.
Kutokana na hali hii ilibidi Khadija atumie utajiri wake wote kuuhami Uislamu
chini ya hifadhi kubwa ya ami yake Mtume, Abu Talib. Mchango wa bibi huyu ni
mkubwa sana katika Uislamu, lakini bahati mbaya yeye na Bwana Abu Talib
wamekuwa ni madhulumu wa historia ya Uislamu. Si wanahistoria Mustashirik tu,
bali hata wanahistoria wa Kiislamu wamekwepa kuandika wasifu wake kwa ukamilifu
kama ambavyo wamekwepa kuandika kwa ukamilifu wasifu wa Bwana Abu Talib na
kumsingizia ukafiri.
Katika makala zangu nitakuwa nikiandika angalau kwa kiasi cha kuridhisha wasifu wa Bibi Khadija. Wasifu huu umeanzia kabla ya kuolewa na Mtukufu Mtume na baada ya kuolewa naye. Nitayaandika matukio muhimu yanayohusiana na bibi huyu, kwa kutumia vyanzo sahihi vya Kiislamu.

No comments:
Post a Comment