SABABU ZA MTUME MUHAMMAD
(S.A.W.W) KUMLEA IMAM ALLY (A.S)
Mtume Muhammad (a.s) na mama
yetu bibi Khadija (a.s) walimchukua Imam Ali (a.s) baada ya kufa kwa watoto wao
wenyewe wa kiume. Kwa hiyo imam Ali aliziba uwazi katika maisha yao na kuwa
kama mtoto wao wa kumzaa hasa.
Sababu nyingine ya kumchukua
imam Ali na kumlea ni kumuelimisha na kumuandaa kwa ajili ya takdir kubwa
iliyokuwa ikimngojea katika nyakati zijazo. Hapa ninakusudia kumwandaa kuwa
kiongozi wa baadaye wa Uislam.
Kiongozi wa Uislamu ni lazima
aandaliwe kiislamu, katika mazingira ya Uislamu hasa. Ni tofauti na kukurupuka
na kumpa uongozi mtu asiyeandaliwa vyema. Kumpa mtu uongozi wa jambo asilolijua
vyema ni kulidumaza jambo lenyewe.
Dr. Taha Hussein wa Mirsi
anasema kwamba Mtume wa Allah (s.w.t.) mwenyewe alikuwa kiongozi wa Ali,
mwalimu na mwelekezaji, na hii ni sifa moja nyingine zaidi ambayo anayo Ali, na
ambayo hakuna mwingine yeyote anayeshirikiana naye kwayo.
“Uislamu unaweka tamasha la maendeleo ya dini
ya ulimwengu katika mwanga wa historia.” (Uislamu, 1969)
Kadhalika, inaweza kusemwa
kwamba kati ya marafiki na Masahaba wote wa Muhammad, Mtume wa Uislamu, Ali
ndiye pekee aliyekua katika mwanga kamili wa historia.
Hakuna sehemu ya maisha
yake, ama katika uchanga wake, utoto wake, uvulana wake ujana wake, uanaume
wake au kupevuka, ambayo imefichikana kutoka kwenye mwangaza wa historia.
Alikuwa ndio kivutio kikuu cha macho yote tangu kuzaliwa kwake mpaka kufa
kwake. Kwa upande mwingine maswahaba waliobakia wa Mtume (s.a.w.) wanakuja
kwenye mvuto wa nadhari ya mwanafunzi wa historia baada tu walivyokubali
Uislamu, na kidogo, kama kipo, kinajulikana mpaka kufikia hapo.
Imam Ali alijaaliwa kuwa
mkono wa kuume wa Uislamu, na ngao na kingio la Muhammad, Mtume wa Allah
(s.w.t.) Takdira au maajaliwa yake yalikuwa kiungo kisichotenganishwa na
takdira ya Uislamu, na maisha ya Mtume wake. Alikuwepo katika kila hali ya
mambo katika historia ya harakati hii mpya, na alishika nafasi ya kuwa nyota
ndani yake. Ilikuwa, kwa dharura, ni nafasi ambayo yeye pekee ndiye angeweza
kuishika.
Aliakisi “taswira” ya mtume Muhammad
(s.a.w.w). Kitabu cha Allah (s.w.t.) chenyewe kimemuita “nafsi” au mwandani
(nafsi ya pili) ya Mtume Muhammad katika Aya ya 61 ya Sura ya tatu, na
alionyesha jina lake maarufu toka upande mmoja hadi mwengine, wa historia.
Muundo wa ufanyaji kazi
pamoja wa mtume Muhammad na imam Ali - amir na mfuasi – ulikuja kuweka “Ufalme
wa Mbinguni” katika ramani ya dunia.
No comments:
Post a Comment