Friday 16 November 2012

Hongereni kwa kuingia mwaka mpya wa kiislamu 1434

Ninapenda kutoa mkono wangu wa pongezi kwa watu wote duniani kwa kuweza kuingia ndani ya mwaka mpya wa kiislamu kwa amani na furaha. Ninamwomba Mwenyezi Mungu Allah (sw) atusameha waovu yote tuliyoyafanya katika mwaka uliopita kisha atujalie uchamungu na tuweze kujiepusha na maasi katika mwaka huu.

Wakati tukiwa na sherehe za mwaka mpya tukumbuke vilevile matukio makubwa yaliyotokea ndani ya Uislamu katika tarehe na mwezi huu wa Muharram. Siku kumi za mwanzo za mwezi huu mwaka 61 waliteswa na kuuawa shahidi baadhi ya viongozi wa kiislamu ambao waliuliwa na mtawala dhalimu Yazid ibn Muawiyyah ni kutokana na kiongozi wa wachamungu hao Imamu Hussein kukataa kuwa chini ya utawala dhalimu. 
Kwani Yazid ambaye baadhi ya waislamu wanamuita kiongozi wa waumini alikuwa mlevi, haswali, mzinzi aliyepindukia na asiyejali utu. Rushwa, uzinifu na dhuluma zilitapaa kila kona ya nchi na kuwalazimisha waumini wa Kufa, Iraq, wamuite Imam ili awaokoe kutokana na ukandamizaji huo. Imam aliamua kwenda lakini kabla kufika Kufa alikutana na kikosi cha jeshi la adui katika eneo la Karbala na kuwauwa wanaume na watoto wa kiume wapatao sabini na mbili, wengi wao walikuwa wajukuu wa mtume Mohammad (saww) na Wafuasi wao. Wanawake walichukuliwa mateka na kuvuliwa hijabu kisha walitembezwa mji mpaka mwingine wakiwa dhalili kabisa huku mbele ya msafala huo kikiwekwa kichwa cha Imam Hussein. Innalillah wa innailahir rajiun.

No comments:

Post a Comment