Ukhalifa na ungozi baada ya Mtume
ilikuwa ni sababu iliyopelekea waislamu kugawanyika makundi mawili shia na
sunni
Ambapo masuni
walidai kuwa mtume amewaachia waislamu wamchague kiongozi wamtakaye ambapo
wakamchagua Abubakar bin kuhafah kuwa Khalifa. na Mashia wakasema kuwa
mtume aliacha amemchagua atayekuwa kiongozi baada yake ambaye ni Sayyidna Ally
bin Abi Talib na kizazi chake.
Mpaka kufika hapa tunaona kuwa mtume na maswahaba ndio msingi na mhimili mkuu wa madhehebu ya Suni.
Na kwa upande wa mashia msingi na mhimili wao mkuu ni mtume na watu wa nyumbani kwa mtume (Ahlul bayt a.s).
Na hapa tunaona kuwa madhehebu haya mawili yanashuhudia kuwa: Mwenyezi Mungu ni Mmoja, hakuzaa wala hakuzaliwa na mtume Muhammad (s.a.w) ndiye mtume wa mwisho, madhehebu haya pia wanasali sala tano, wanafunga, wana kwenda hijja, wanatoa zaka na wanaamini ufufuo baada ya kifo.
Kwa kifupi hakuna shaka kwamba madhehebu haya, yanashikamana na misingi ya dini ya kiislamu kama inavyotakiwa.
Lakini jambo la kusikitisha ni kwamba kadri muda unavyo kwenda ndivyo madhehebu mapya yanajitokeza na kujipa majina ya kuvutia, wakisambaza fikra potofu na hatimaye kuchafua jina na kushusha hadhi ya waislamu na Uislam kwa jumla. Madhehebu haya yamewakufurisha kila waliopingana na mitazamo yao na hata kutoa hukumu ya kuawa wapinzani wao, wanafanya haya yote wakiamini kuwa wenyewe tu, ndio waislamu halisi na madhehebu mengine yoote ni uzushi na upotefu mtupu.
Jambo la kutia moyo ni kwamba Allah ameahidi kuilinda dini yake hata kama jambo hili litawaudhi baadhi ya watu.
Kama nilivyo tanguliza kusema hapo juu kuwa madhehebu makuu ni mawili na mengine ni matawi ya madhehebu haya, ningependa kuelezea itikadi na mitazamo za madhehebu haya, lakini kwa kuwa dhehebu la sunni ndio dhehebu lenye wafuasi wengi sana Tanzania na hata Afrika kwa Ujumla, sita lizungumzia dhehebu hili kwakina, bali nitapenda kuelezea dhehebu la Shia au (Ahlul bayt) ili tupate kuwatambua watu hawa.
Neno Shia katika lugha ya kiarabu lina maana ya mfuasi.
Katika historia neno Shia limetumika kuwaita watu wafuatao:
1. Limetumika kuwaita wanaoitikadia kuwa Sayyidna Alli bin Abii Talib ndiye sahaba bora kuliko masahaba wote.
2. Pia linatumika kuwa ita wanaoitikadia kuwa mtume aliacha amemchagua Sayyidna Ally bin abi Talib na kizazi chake kuwa ni makhalifa na viongozi wa Uislamu baada yake, na wala hakuacha waislamu wafanye uchaguzi wa makhalifa kama ilivyo kwa dhehebu la sunni.
Mashia nitaowazungumzia hapa ni mashia kwa maana ya pili ambao kwa jina lingine wanaitwa: madhehebu ya Ahlul bayt au Shia Ithna asharia .
Hivyo Allah akinipa taufiki, katika mada ifuatayo
Nitazungumzia dhehebu hili ili liwe wazi kwa woote.

No comments:
Post a Comment