BINTI WA NABII
MUHAMMAD (s.a.w.w.)
Yeye ni Fatima Zahra; Baba yake ni Rasulullah
(Mjumbe na Mtume wake Mwenyezi Mungu) Muhammad bin Abdullah (s.a.w.w.); na mama
yake ni Bibi Mtukufu Khadija Mama wa Waislamu, na mumewe ni bwana wa mawasii
Ali Ameerul-Muuminiin, na watoto wake na wajukuze ni maimam watoharifu (juu yao
Rehma na Amani).
Alizaliwa Bibi Fatima (a.s.) siku ya mwezi ishirini, mwezi wa
mfungo tisa, mwaka wa arobaini na tano toka alipozaliwa Mtume (s.a.w.w).
Na akafa bibi huyo siku ya Jumanne mwezi tatu, mfungo tisa, mwaka
wa kumi na moja wa Hijiria [5]. Na umri wake ni miaka kumi
nanane.
Na akasimamia matendo ya kifo chake Amirul Muminiin Ali (a.s.),
akamzika Madina Munawwara (Mji wenye nuru, mji wake Mtume, uliopo katika Saudia
Arabia), na akalificha kaburi lake kama alivyo usia mwenyewe Bibi Fatima.
Alikuwa bibi huyo kama baba yake kwa ibada na kumcha Mungu na
ubora, na zimeshuka katika sifa zake aya nyingi za Qur'ani al-Hakim.
Alikuwa Mtume (s.a.w.w.) akimwita "Bibi wa wanawake wa
Ulimwenguni", na akimpenda mapenzi mazuri mpaka yeye akiwa anaingia kwa
Mtume (s.a.w.w.) humkaribisha na kusimama na kumkalisha mahali pake, pengine
humbusu mikono yake.
Na Mtume (s.a.w.w.) akasema: "Mungu huridhika analoridhika nalo
Fatima na hukasirika Unalo mkasirisha Fatima."
Pia Mtukufu Mtume amesema: "Wabora wa wanawake wa peponi ni
wanne: Mariam Binti Imrani, na Khadija Binti Khuwailid, na Fatima Binti
Muhammad (s.a.w.w.) na Asia Bint Muzaahim.
Mtu mmoja akamwuliza bibi Aaisha "Mtu gani alikuwa mpenzi mno
wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Akajibu: Fatima.
Kisha akamwuliza: Ni gani kutokana na wanaume? Akajibu: Mume wake
Bibi Fatima, yaani Ali bin Abi Talib (as.).
Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) akasema: "Hakika, Mwenyezi Mungu
ameniamrisha mimi nimwoze Fatima kwa Ali (a.s.).
Kazaa bibi huyo kwa Amirul Muuminiin Ali (a.s.): Imam Hassan
(a.s.), Imam Hussein (a.s.), Bibi Zainab (a.s.), Bibi Ummu Kulthum (a.s.) na Muhsin (a.s.)- Lakini bwana Muhsin kafa tumboni zama alipopata
mama yake msukosuko wa maadui. Kwa hiyo jumla ya watoto wa bibi Fatima ni 5.
Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) amesema: "Kila mtoto huchukuwa ukoo
wa baba yake isipokuwa vizazi vya Fatima, kwani mimi ndiyo walii wao na nasaba
wao (yaani, vizazi vya Fatima wote ukoo wao unatokana kwa Mtukufu Mtume
(s.a.w.w.).
Pia Mtume Mtukufu amesema:- "Kila ukoo na uhusiano utafutika
siku ya qiyama isipokuwa ukoowangu na uhusiano wangu.
No comments:
Post a Comment