Friday, 20 September 2013

Je Mashia wanaamini Qur'an nyingine?

Kwa hakika sisi tumeuteremsha ukumbusho huu (Qur'an) na hakika sisi ndio tuulindao (Qur'an: Sura 15, Aya 9).
Mashia mara kwa mara tumetuhumiwa kwa imani ya Tahrif ndani ya Qur'an, ambayo maana yake ni kuamini kwamba Qur'an imepotoshwa na haiko sawa na ile aliyoteremshiwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.).

HII SI KWELI!!! (Madai haya hutolewa na maadui wa Uislamu ili kuzuia umoja baina yetu)
Wanavyuoni wakubwa wote wa Shi’ah Imaamiya tangu siku za mwanzo hadi karne za sasa wanaamini kuwa Qur’an imehifadhiwa kikamilifu. Wanavyuoni mashuhuri wa Shia wa mwanzoni wamesema hivi wazi katika vitabu vyao, miongoni mwao ni:
-       Shaykh al-Saduq (aliyefariki 381 AH), Kitabu'l-Itiqadat, (Teheran.1370) Uk. 63;
-       Shaykh al-Mufid (aliyefariki 413 AH), Awa'ilu l-Maqalat, Uk. 55-6;
-       Sharif al-Murtadha (aliyefariki 436 AH), Bahru 'l-Fawa'id (Teh, 1314) Uk. 69;
-       Shaykh at-Tusi (aliyefariki 460 AH), Tafsir at-Tibyan, (Najaf, 1376), Juz. 1 Uk. 3;
-       Shaykh at-Tabrasi (548AH), Majma'u 'l-Bayan, (Lebanon), Juz. 1 Uk. 15.

Baadhi ya Wanavyuoni waliokuja baadaye waliotoa maoni kama hayo ni:
-       Muhammad Muhsin al-Fayd al-Kashani (aliyefariki 1019 AH), Al-Wafi, Juz. 1 Uk.273-4,
-       al-'Asfa fi Tafsir al-Qur'an, Uk. 348;
-       Muhammad Baqir al-Majlisi (aliyefariki 1111 AH), Bihar al-'Anwar, Juz 89 Uk. 75.

Imani hii iliendelea bila ya kukatizwa mpaka leo hii.
Wanavyuoni wa Shia wa karne hii waliokariri imani hii, kwamba Qur’an imehifadhiwa kikamilifu na
haikubadilishwa, ni wale miongoni mwa wenye majina mashuhuri kama vile:
-       Sayyid Muhsin al-Amin al-'Amili (aliyefariki 1371 AH);
-       Sayyid Sharaf al-Dinal-Musawi (aliyefariki 1377 AH.);
-       Shaykh Muhammad Husein Kashif al-Ghita' (aliyefariki 1373 AH);
-       Sayyid Muhsin al-Hakim (aliyefariki 1390 AH);
-       'Allamah at-Tabataba'i (aliyefariki 1402 AH);
-       Sayyid Ruhullah al-Khumayni (aliyefariki 1409 AH);
-       Sayyid Abu al-Qasim al-Khu'i (aliyefariki 1413 AH)
-       Sayyid Muhammad Ridha al-Gulpaygani (aliyefariki 1414 AH).
Hii, kwa kweli, si orodha nzima.

Swali: Lakini ni vipi kuhusu Mashia waliokuwapo kabla ya Wanavyuoni hawa, je wao waliamini tahrif?
Hapana! Hebu chukulia mfano wa 'Ubaydullah b. Musa al-'Absi (120-213 AH), Mwanachuoni wa Shia mwaminifu ambaye masimulizi yake kutoka kwa Maimamu yanapatikana katika mkusanyo wa Hadith wa Shia kama vile al-Tahdhib na al-Istibsar.

Hebu na tuangalie baadhi ya Wanavyuoni wa Sunni
wanasema nini kumhusu 'Ubaydullah b. Musa al-'Absi:
_ “... ni mcha Mungu, miongoni mwa Wanavyuoni muhimu wa Shia
...alikubaliwa kuwa mwaminifu na Yahya b. Ma’in. Abu Hatim amesema:
‘Alikuwa mwaminifu, mkweli...’ al-'Ijli amesema kwamba yeye alikuwa ni
mtu mwenye cheo kikuu katika elimu ya Qur’an...”
[Al-Dhahabi, Tadhkirat al-Huffaz (Haydarabad, 1333 AH), Juz. 1 Uk. 322]
_ “...Yeye alikuwa ni Imam katika Fiqh, Hadith na Qur'an, alisifika kwa
uchaji Mungu na wema, lakini alikuwa mmoja kati ya wakuu wa Shia.”
[Ibn al-'Imad al-Hanbali, Shadharat al-Dhahab (Cairo, 1350 AH), Juz. 2 Uk. 29]
Kama wanavyuoni hawa wa Sunni wangeona kuwa yeye aliamini kuwapo kwa Qur’an nyingine, basi hata mmoja wao asingelimsifu kwa ujuzi wake!
Na Ubaydullah alikuwa akichukuliwa kuwa ni mwaminifu sana, licha ya kuwa alikuwa ni Shia, kiasi kwamba Wanavyuoni maarufu wa kisunni wa Hadith, al-Bukhari, Muslim na wengineo wengi, katika mikusanyiko ya Hadith, wamechukuwa Hadith kutoka kwake!
[The Creed of the Imaam of Hadeeth al-Bukhari (Salafi Pub., UK, 1997), Uk. 87-89]

Swali: Je Shia hawaamini Msahafu wa Fatimah ambao mkubwa mara tatu ya ukubwa wa Qur'an?
Qur'an ni Mushaf (Kitabu), lakini, si kwamba kila kitabu lazima kiwe Qur’an! Hakuna kamwe “Qur'an ya Fatimah”! Mushaf Fatimah kilikuwa ni kitabu kilichoandikwa au kuelezwa na Fatimah (a.s.) baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w). Hicho si sehemu ya Qur’an na hakina uhusiano wowote na amri za
Mwenyezi Mungu au hukmu za kisharia.

Swali: Lakini je, hakuna Hadith katika vitabu vya Shia zinazotaja Aya za Qur’an zenye maneno mengine zaidi ya hii tuliyo nayo leo?
Kuna baadhi ya mifano ambapo maneno zaidi yametajwa lakini kwa minajili ya kufafanua tu, haimaanishi kwamba Aya asili za Qur’an zimegeuzwa. Hii hutokea pande zote, kwa upande wa Shia na wa Sunni. Hebu zingatia mifano ifuatayo, yote ni kutoka upande wa sherhe maarufu za Qur’an za Sunni:
_ “Ubayy b. Ka'b alikuwa akisoma ‘…basi wale mnao faidi nao kwa kipindi maalum, wapeni mahari yao kama ilivyoamriwa…’ (Qur'an, Sura 4, Aya 24), na Ibn Abbas pia alikuwa akisoma hivyo hivyo.”
[Fakhr al-Din al-Razi, Mafatih al-Ghayb (Beirut, 1981), Juz. 9 Uk. 53]
[Ibn Kathir, Tafsir al-Qur'an al-'Adhim (Beirut, 1987), Juz. 2 Uk. 244]

Maelezo yaliyomo katika hashia ya Tafsir ya Ibn Kathir yanafafanua kwamba maneno yaliyoongezwa hapo juu, ambayo si sehemu ya Qur’an, yalisomwa na maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.) kwa ajili ya tafsir na ufafanuzi tu.

_ “Ibn Mas'ud amesema: “Wakati wa Mtume (s.a.w.w.) tulikuwa tukisoma, ‘Ewe Mtume wetu (Muhammad) fikisha lile ulilotumwa kutoka kwa Mola wako nalo ni 'Ali ni Bwana wa Waumini na kama hukufanya, basi hujafikisha ujumbe Wake.’” (Qur'an Sura 5, Aya 67).
[Jalal al-Din al-Suyuti, Durr al-Manthur, Juz. 2 Uk. 298]

Katika hali hii pia inavyoonyesha, kipande kilichoandikwa kwa mshazari (italics) kwa hakika si sehemu ya Qur'an, hata hivyo, swahaba Ibn Mas'ud alikuwa akisoma hivyo alipokuwa akifafanua ufunuo wa Qur’an.

Swali: Ni vipi kuhusu zile Hadith zisemazo kwamba baadhi ya Aya si sehemu ya Qur'an?
Shia hawaamini kwamba mwandishi au mpokezi ana kinga ya kutofanya makosa, na kwa hivyo hawachukulii kwamba Hadith zote ni sahihi. Kitabu pekee chenye kinga ya kutokuwa na kosa lolote ni Qur'an. Mara nyingi Hadith hizi huchukuliwa kuwa ni dhaifu au maneno yaliyo teremshwa nje ya Qur’an.
_ Ni vizuri itajwe kwamba kuna baadhi ya Hadith kwenye Sahih al-Bukhari na Sahih Muslim zisemazo kwamba Aya nyingi za Qur’an haziko. [Al- Bukhari, Al-Sahih, Juz. 8 Uk. 208; Muslim, Al-Sahih, Juz. 3 Uk. 1317].
_ Si hivyo tu, Hadith hizi za Sunni zadai kwamba Sura mbili za Qur’an hazipo, ambapo mojawapo ni kama Sura ya al-Bara’ah (Sura ya 9) kwa kirefu!!! [Muslim, Al-Sahih, Kitab al-Zakat, Juz. 2 Uk. 726].

_ Hata kuna baadhi ya mapokezi ya Hadith ya Sunni yanayodai kuwa Sura ya al-Ahzab (33) ilikuwa ni ndefu kama ilivyo Sura ya al-Baqarah!!!
Ambapo hakika Sura ya al-Baqarah ndio Sura iliyo kubwa zaidi katika Qur'an. Kuna hata Hadith ndani ya Sahih al-Bukhari na Muslim ambazo zimetaja kwa urefu baadhi ya Aya ambazo hazipo. [Al-Bukhari, Al-Sahih, Juz. 8 Uk. 208].

Kwa bahati nzuri, Shia katu hawajawatuhumu ndugu zao Sunni kwa kuamini kwamba Qur’an haikukamilika. Sisi tunasema kwamba Hadith hizi za Sunni, ama ni dhaifu, au zimezushwa.

Hitimisho:
“Sisi MASHIA twaamini kwamba Qur'an ambayo Mwenyezi Mungu alimteremshia Mtume wake Muhammad (s.a.w.w.) ni kama ile iliyoko baina ya jalada mbili. Na ndiyo hiyo hiyo iliyoko mikononi kwa watu.
Na anayedai kuwa sisi tunasema kwamba (Qur’an) ni tofauti kuliko hii (ya
sasa), huyo ni muongo.”
[As-Saduq, Kitabu'l-I`tiqadat (Tehran: 1370 AH) Uk. 63; Tafsir ya kiingereza,
The Shi'ite Creed, tr. A.A.A. Fyzee (Calcutta: 1942) Uk. 85].

Ili kujua zaidi kuhusu dini ya Kiislamu, tazama Tovuti hii: http://al-islam.org/faq/

Life Lessons from the Ahlul Bayt (a)




Four things will destroy a house and remove blessings from it: treachery, theft, consumption of alcohol, and adultery.‛


Brief Explanation

These will not only destroy a household; but they will destroy a society as well. Whenever treachery influences the social structure trust will be removed from the people. Whenever theft becomes rampant there will be no peace. Whenever alcoholism grows the level of intellectualism will diminish and the number of children with physical defects will increase. Whenever adultery is the norm the family structure will be destroyed causing the future generation to turn to sin.

 Quoted from Nahj al-Fasahah
By: Ayatollah Makarem Shirazi

Syria: Evidence shows insurgents responsible for gas attack

Russian Foreign Minister Sergei Lavrov said:

“We have plenty of reports on chemical weapons use, which indicate that the opposition regularly resorts to provocations in order to trigger strikes and intervention against Syria.”

“There’s a lot of data. It’s widely available on the Internet. This data is presented in the report, which our experts put together in association with the use of chemical weapons in Aleppo in March this year.”

“There’s also plenty of data on the incidents that occurred in August in Ghouta, near Damascus.”

“All of this will be considered in the Security Council, together with a report, which was submitted by UN experts, confirming that chemical weapons were used.”

Russian Deputy Foreign Minister Sergei Ryabkov spent two days in Damascus. He met with Syrian Foreign Minister Walid al-Moallem and President Bashar al-Assad.

Voice of Russia headlined “Damascus provides Russia with new info on Syrian opposition’s use of chemical weapons - Ryabkov.”

Syria provided “very convincing” evidence, he said. It shows insurgents’ responsibility for Ghouta’s gas attack.

“There is some confusion in this regard,” said Ryabkov. “We received additional proof, which had been gathered and analyzed by the Syrian authorities.”

“They consider it to be evidence of chemical weapons use by the so-called Syrian opposition in eastern Ghouta on the 21st, 22nd, 23rd and 24th.”

“The material received, given to us in Arabic, will be translated into Russian. What kind of conclusions can Russia draw?”

“This will be studied in detail and without hurry. I assure that this could change the course of further talks.”

“As for possible conclusions that may be drawn by Russia from this new evidence.”

“It’s a case that requires further scrutiny. It will take some time and should be done without haste.”

“This evidence was previously given to (UN inspectors head) Mr. Selstrem, who was here in Syria and headed the group of experts.”

His report is “limited in terms of scope, preliminary and insufficient. It’s not “grounds for far-reaching conclusions.”

“We come across the situation often when materials prepared by UN experts and released by the UN secretariat are not grounds for sufficient, comprehensive and far-reaching summaries.”

Ryabkov added that Security Council resolution language should cover only Syria agreeing to eliminate its chemical weapons. Force threats won’t be permitted.

It should support an expected Organization for the Prohibition of Chemical Weapons (OPCW) decision backing the US/Russian deal, “and nothing more than that.”

Lavrov said he hasn’t seen evidence Syria supplied, “but I’m sure that the experts are going to work with it and, of course, we’ll provide it to the security council.”

According to Russia’s Presidential Administration Chief of Staff Sergei Ivanov, Moscow and the USSR never supplied chemical weapons to other countries.

“Nobody disputes the fact (it ever) shipped warheads armed with sarin to Syria or any other country.” Toxic agents used in Ghouta were likely “backyard produced.”

US Defense Secretary Chuck Hagel accused Russia of supplying Damascus with chemical weapons. He and other US officials lied.

On September 19, Itar Tass headlined “Russia’s Deputy Foreign Minister meets Syrian opposition in Damascus.”

Russia’s Deputy Foreign Minister Mikhail Bogdanov said Moscow “is ready to submit evidence of Syrian opposition using chemical weapons to the UN on Thursday.”

“We plan to do is as quickly as possible, tonight or tomorrow,” he said. “We expect all available information, not just one investigation into one incident, will be taken into consideration.”

Bogdanov met with Popular Front for Change and Liberation’s Qadri Jamil, as well as Syrian National Council officials.

He called it important to do so. Resolving Syria’s conflict requires their cooperation.

“We are ready to organize contacts not only with the opposition, but also between the opposition groups, maybe in Moscow,” Bogdanov added.

On September 19, Russia Today headlined” “Russia: UN inspectors ignored evidence on Syria,” saying:

Deputy Russian Foreign Minister Sergei Ryabkov told RT:

“The Syrian authorities have conducted their own sampling and investigation, analysis in terms of possible evidence of the rebels being responsible for the tragic episodes both on August 21, but beyond that also on August 22, 23 and 24.

“This is new material - new material for us. But this is not already completely new material for the UN.”

“This material was discreetly handed over to Ake Sellstrom, the head of the UN mission of experts here (in Syria) which came to investigate the Ghouta incidents.”

“Sellstrom was asked to look into it and eventually factor this new evidence into the final report. It never happened in fact.”

“This is one of the reasons why we criticize the speed with which the report was released and also an incomplete content of this report.”

“We expect the UN Secretariat to both send Sellstrom and his people back to Syria to continue investigation of the three remaining incidents, and also to write a full and comprehensive report against the background of all information they have received.”

Ryabkov’s concerned about Syrian/Russian provided evidence being “nullified and disregarded.”

UN inspectors should follow the same procedure Russia did in analyzing a March Aleppo chemical attack. It showed insurgents responsible for chemical weapons use.

Ryabkov wants Sellstrom’s team to return to Syria. He wants their investigation continued. He wants a legitimate, unbiased report. The one submitted was, one-sided, fraudulent and worthless.

“We are concerned about (further) provocations, Ryabkov stressed. We have seen it before that the moment something better, positive is out there, is looming, you will always find (elements) who would try immediately to change these dynamics and establish a new reality, so to say, through a provocation.”

“And it’s just amazing how little of this understanding is among those who now advocate a very different course fighting the government with weapons in their hands.”

“It’s unforgivable. This is the real crime which they are committing against their own people and their country.”

On Tuesday, Fox News contributor/former congressman Dennis Kucinich and journalist Greg Palkot interviewed Assad in Damascus. He said in part:

“Last week we joined the international agreement of preventing chemical WMDs, and part of this agreement, the main part, is to not to manufacture these armaments, not to store, and not to use, and of course not to distribute, and part of it is to get rid of those materials, the chemical materials.”

“Of course, when we are part now of this agreement, we have to agree on that chapter (o)n getting rid of all these armaments. I mean to destroy them.”

Ten years ago, he said, he proposed a WMD-free Middle East. Washington opposed it. Letting Israel maintain formidable nuclear, chemical and biological weapons reflects US policy.

Asked if joining the Chemical Weapons Convention is a stalling tactic, Assad responded:

“When you join the agreement, you have a mechanism, and you have to obey this mechanism, and according to the history of Syria, we never made an agreement with any party in this world and we didn’t fulfill what we have to do or our role in that agreement, never.”

“We didn’t say that we are joining partially that agreement or that organization. We joined fully. We sent the letter. We sent the document, and (we) are committed to the full requirements of this agreement.”

Asked if he can destroy CWs quickly, and if not, why, he responded:

“I think it’s a very complicated operation technically, and it needs a lot of money. Some estimated about a billion for the Syrian stockpile.”

“We’re not experts in that regard, but that’s the estimate that we’ve had recently.”

“So, you have to ask the experts what do they mean by ‘quickly’ because this has a certain schedule. It needs a year, maybe a little bit less or a little bit more. So, what do you mean by ‘quickly?’ ”

He’s willing to let America destroy his CWs if it’ll pay for it. A “specified” UN organization will handle the task.

Syria has no conditions, Assad said. “In the end, if they’re going to be destroyed, they could be destroyed anywhere.”

“As I said, (they’re) very detrimental to the environment, so whichever country is ready to take risk of these materials let them take it.”

Asked if destroying his CWs by mid-2014 is doable, he said:

“(W)e have to discuss these details with the organization first. This is first. Second, the time is not our problem.”

“It is the problem of the organization. How much time (they) need to implement this agreement.”

“The only thing we have to do is provide the information, and to make them accessible to our sites, which is not a problem. We can do it tomorrow. We don’t have any problem.”

“The problem is how fast they can be in getting rid of any chemical material, because this is a very complicated situation. It’s not about will. It’s about techniques. So, only experts can answer your question.”

Assad wants evidence UN inspectors reported fully assessed. He wants further investigation. He wants unbiased analysis. He wants conclusions based on it.

He questioned suspect videos. No one verified them. They’re easy to fake.

Mother Agnes Mariam de La Croix’s International Support Team for Mussalaha in Syria (ISTEAMS) reported fabricated ones. They’re commonly used. They were used against Gaddafi in Libya. They’ll be used again.

Assad stressed there’s “a lot of forgery on the internet. Any rebel can make sarin. (It’s called) kitchen gas. (W)e know that all those rebels are supported by governments, so any government (with) chemical material can hand it over to” insurgents.

Responding to allegations of a ton of sarin used, as well as rockets and launchers Syria’s army uses, he said:

“This realistically cannot be possible. You cannot use the Sarin beside your troops, this is first.”

“Second, you don’t use WMDs while you are advancing. You’ve not been defeated, and you’re not retreating.”

“The whole situation was in favor of the army. Third, we didn’t use (CWs) when we had bigger problems last year.”

“When they talk about any troops or any unit in the Syrian army that used this kind of weapon, this is false for one reason because chemical weapons can only be used by specialized units.”

“It cannot be used by any other units like infantry or similar traditional units. So, all what you mentioned is not realistic and not true.”

“Definitely, so far as government, we have evidence that the terrorist groups have used Sarin gas and those evidences have been handed over to the Russians.”

“The Russian satellites, since the beginning of these allegations at the 21st of August, they said that they have information through their satellites that the rocket was launched from another area.”

So, why ignore this point of view? So, the whole story doesn’t even hold together. It’s not realistic.”

“In one word, we didn’t use any chemical weapons in the Ghouta, because if you want to use it, you would harm your troops. You would have harmed tens of thousands of civilians living in Damascus.”

Assad wants further investigations. He invited UN inspectors to come in March. He asked them to come back.

More work needs to be done. Other areas need examining. Washington pressured Sellstrom to report quickly. He didn’t finish his mission. It’s suspect. It’s incomplete. It lacks credibility.

Full and accurate analysis shows insurgents alone used chemical weapons. They’re responsible for multiple incidents. They attacked Ghouta with gas. Syrian forces had nothing to do with it, Assad stressed.

Asked if he’d characterized ongoing conflict as civil war, he said:

“No. Civil war start(s) from within society. (Syria’s conflict has) 80 or 83 nationalities coming to fight within your countries supported by foreign countries.”

“What we have is not a civil war. What we have is a war, but it’s a new kind of war.”

“(N)o one has precise numbers. We know that we have tens of thousands of Jihadists” involved 80 to 90% of the rebels or terrorists on the ground are Al Qaeda and their offshoots.”

“We have tens of thousands of Syrians that have died, mainly because of the terrorist attacks, assassinations, and suicide bombers, the majority.”

“More than 15,000″ soldiers were killed, he said. He has no insurgent casualty numbers. “(W)e cannot count them,” he said.

“The majority of the innocent people have been killed by the terrorists, not by the government.”

“No wise government in the world would kill its own people. How can you withstand if you kill your own people for two years and a half, while the West is against you, many of the regional countries are against you, and your people are against you while you kill them? Is it possible? Is it realistic?”

Attacks on villages, residential and suburban areas target terrorists. “(T)he army has to go there to get rid of” them, Assad stressed.

“The army should defend the civilians, not the opposite. You cannot leave the terrorists free, killing the people, assassinating the people, beheading the people and eating their hearts.”

“When we go to defend them, you say you are killing your own people! You don’t, but in every war, you have casualties.”

“This is war. You don’t have clean war. You don’t have soft war, and you don’t have good war.”

Asked about diplomacy and confidence-building measures, he responded:

“Any diplomatic move without having stability and getting rid of the terrorists is going to be just an illusion.”

“Any diplomatic move should start with stopping the flow of the terrorists, the logistical support of those terrorists, the armament support and the money support.”

“Then, you have a full plan. The Syrians could sit on the table, discuss the future of Syria, the political system, the constitution and everything.”

Negotiating with opposition elements “doesn’t mean (doing it) with the terrorists.” Syria is fully committed to peaceful conflict resolution, Assad stressed.

National reconciliation excludes amnesty for terrorists. They have blood on their hands.

At the same time, he said, “we invited every militant in Syria to give up armament, and offered amnesty to whoever laid down his armament and wants to go back to his normal life as a Syrian citizen. Of course we believe in that.”

Assad covered much more important ground. His interview was long and detailed. Everything he said deserves careful consideration.

He’s thoughtful, straightforward, and honest. He says what he means and means what he says. He deserves to be taken seriously.

He priorities peaceful conflict resolution. He wants Syrians alone able to choose who’ll lead them.

He wants foreign intervention stopped. He wants bloodshed ended. Syrians overwhelmingly support him. It’s for good reason.

He’s their last line of defense. Restoring peace depends on him. Don’t expect Fox News to explain.

Qur’ani inapaswa kutawala maisha ya jamii ya Kiislamu


Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa mwongozo wa Qur'ani na mtindo wa maisha ya Kiislamu vinapaswa kutawala katika jamii ya Kiislamu.
Ayatullah Khamenei aliyasema hayo jana alasiri baada ya majlisi ya qiraa ya Qur'ani iliyoendelea kwa kipindi cha zaidi ya masaa matatu. Alisema kuwa kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu ni utangulizi na mwanzo wa kufika kwenye jamii inayotakikana ya Qur'ani. Amesisitiza kuwa, mwongozo wa Qur'ani na mtindo wa maisha ya Kiislamu vinapaswa kutawala jamii ya Kiislamu.
Ayatullahil Udhmaa Ali Khamenei amesema kuwa, kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu hutayarisha uwanja mzuri wa kuelewa kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu na kujipamba kwa maadili yake. Ameongeza kuwa utamaduni wa jamii ya Kiislamu unapaswa kuoana na akhlaki na maadili ya Qur'ani pamoja na mafundisho ya maasumu.
Ameashiria baadhi ya njama za kutaka kuathiri utamaduni, mtindo wa maisha ya jamii na mahusiano yake ya kijamii kwa kutumia utamaduni wa Kimagharibi na akasema: Kufuatwa utamaduni wa Magharibi na watu wengi duniani hakuwezi kuwa kigezo na hoja ya kufuatwa utamaduni huo katika jamii ya Kiislamu.
Amesema dini, akili timamu na semi za maasumina ndiyo vigezo vilivyoainishwa na Qur'ani ambavyo vinapaswa kuwa mizani na kigezo.
Ayatullahil Udhmaa Khamenei ameelezea kufurahishwa kwake na jinsi vijana wanavyovutiwa zaidi na Qur'ani, kusoma na kuhifadhi kitabu hicho na amesisitiza kuwa: Watu wote wa jamii wanapaswa kujenga uhusiano na Qur'ani Tukufu kwa sababu kusoma na kuielewa Qur'ani ni mwanzo wa kutadabari na kuzama ndani ya maana ya aya za kitabu hicho.

Wamagharibi hawasiti kuua mamilioni ya watu kwa ajili ya kudhamini maslahi yao


Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa serikali, viongozi wa nchi, wanasiasa, wanadiplomasia na wananchi wote wanapaswa kuchambua kwa umakini harakati, mwenendo tata na madai ya kutetea haki za binadamu ya Magharibi.
Ayatullahil Udhmaa Khamenei ambaye leo alihutubia hadhara ya maimamu wa Swala za Ijumaa kote nchini waliokwenda kuonana naye ameeleza sababu za udharura wa kuwa na mtazamo mpana na wa kutilia maanani ukweli wa mambo kuhusu masuala ya Iran na dunia na akasema: Katika kipindi cha ukoloni, Magharibi ilieneza udhibiti wake wa kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni katika eneo la mashariki mwa dunia ukiwemo ulimwengu wa Kiislamu, na kwa kutumia maendeleo ya sayansi na teknolojia, imewafanya watu waamini kuwa, ulimwengu wa Magharibi ndio kigezo na kituo kikuu cha mahesabu yote.
Ayatullah Khamenei amesema kuwa, hata mahesabu ya kijografia Wamagharibi wameyapanga kwa msingi wa kuitambua dunia ya Magharibi kuwa ndiyo bora zaidi na kuanzisha istilahi zisizo sahihi kama "Mashariki ya Karibu", Mashariki ya Kati" na "Mashariki ya Mbali".
Ameashiria udhibiti mutlaki wa nchi za Magharibi katika masuala ya dunia kwa kutumia kipindi cha ukoloni wao katika maeneo mbalimbali ya dunia na kusema: Katika hali hiyo ambapo nchi za kanda hii ikiwemo Iran, zilikuwa zimeathiriwa na udhibiri wa Magharibi na ulimwengu wa kimaada,
Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yakijitegemea kikamilifu na kwa mujibu wa Uislamu na misingi ya Qur'ani, yalipata ushindi na kutoa pigo kubwa kwa misingi ya kihistoria ya Wamagharibi.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia taathira za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika ulimwengu wa Kiislamu na vilevile utambulisho wa Kiislamu ulioletwa na mapinduzi hayo kwa watu wa mataifa mbalimbali na akasema: Kuenea hatua kwa hatua fikra na utambulisho wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kuliwatia wasiwasi mkubwa Wamagharibi ambao walianza kupanga njama na mikakati kabambe ya kukabiliana na mapinduzi hayo.
Amesema kuwa hali ya sasa Katika Mashariki ya Kati na ulimwengu wa Kiislamu imewafanya Wamagharibi waamini kuwa, wamebaki nyuma katika mpambano wao na fikra za Mapinduzi ya Kiislamu na kwa msingi huo wanafanya kila wawezalo ili kufidia kubakia nyuma kwao.
Ayatullah Khamenei amesema kuwa, katika hali kama hiyo kumeanza harakati ya mwamko wa Kiislamu, na Wamagharibi ambao walikuwa wakijiona kuwa wamebakia nyuma katika mpambano wao na harakati ya fikra za Mapinduzi ya Kiislamu wameingia kwenye medani wakiwa na kiwewe kwa ajili ya kukabiliana na mwamko wa Kiislamu na Uislamu wa kisiasa.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameitaja Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ndiye mshindi mkubwa katika mpambano wa ulimwengu wa kimaada dhidi ya Uislamu. Ameongeza kuwa, mshindi huyo mkubwa anaendelea kusimama kidete na mshikamano wa ndani na kushikamana na misingi na thamani zake kutalinda na kuimarisha zaidi ushindi huo.
Ayatullah Ali Khamenei amesisitiza kuwa, Iran inapaswa kuwa imara na yenye nguvu mbele ya ulimwengu wa Magharibi kwa sababu Wamagharibi wameonesha kuwa, hawana huruma kwa mtu yeyote, na kinyume na madai yao ya kutetea haki za binadamu, hawawezi kuathiriwa na kuuliwa mamilioni ya wanadamu.
Amesema kuwa kusema uongo na kutaka kujionesha ni miongoni mwa sifa za wanasiasa za Kimagharibi. Ameongeza kuwa, ukweli wa mambo ni kuwa Wamagharibi hawaumizwi na mauaji ya watu wa Hiroshima, kuuliwa kwa mamilioni ya watu katika Vita vya Kwanza na vya Pili vya Dunia na kuuliwa kwa watu wasio na hatia katika nchi za Pakistan, Afghanistan na Iraq na hawatasita kuua watu katika siku za usoni kwa ajili ya kutimiza maslahi yao. Amesisitiza kuwa: Kwa msingi huo Iran inapaswa kuzidisha uwezo wake wa ndani katika nyanja mbalimbali za kisaisa, kiserikali na kimaisha.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameitaja Swala ya Ijumaa kuwa ni kanali yenye thamani kubwa ya kidini, ya wananchi na serikali na kuongeza kuwa, Sala ya Ijumaa ni mchanganyiko wa kuweka wazi hakika za kiroho na Kiislamu, mahudhurio ya wananchi katika medani na yenye mfungamano na serikali ya Kiislamu.
Kuhusu mfungamano wa Swala ya Ijumaa na serikali, Ayatullah Khamenei amesema kuwa tofauti na baadhi ya watu anavyodhania, wadhifa wa serikari hauishii katika kudhamini hali bora ya kimaisha, uhuru na kujitegemea kisiasa kwa wananchi, bali serikali inawajibika mbele ya masuala ya dini na itikadi za wananchi.
Ayatullah Khamenei pia amewausia maimamu wa Swala za Ijumaa kutoa hotuba fupi, zilizojaa maana na kuambatana na mawaidha na akasema: Hotuba za Swala ya Ijumaa zinapaswa kuzungumzia mahitaji ya watu na kujibu maswali yao hususan tabaka la vijana katika nyanja za kiitikadi, kielimu na kisaisa.   

HADITH YA MTUME INAYOWALAUMU MASAHABA KWA KUWAFUATA WAYAHUDI NA WAKRISTO



Amesema Mtume Mohammad (S.A.W) kuwaambia Masahaba wake, “Bila shaka Mtafuata nyendo za waliokutangulieni shubiri kwa shubiri na dhiraa kwa dhiraa (Hatua kwa hatua au kidogo kidogo) hata kama wataingia katika shimo la kenge, mtawafuata”. Masahaba wakauliza, “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni wayahudi na wakristo?” Mtume akajibu, “Ni nani basi (kama sio hao)?”
Rejea:
1.     Sahihi bukhari juzuu 4 ukurasa wa 187
2.     Sahihi Muslim juzuu ya 8 ukurasa wa 57
3.     Musnad Ahmad bin Hambal juzuu ya 3 ukurasa wa 84 na 94

Ndani ya Qur’an na katika Historia sahihi inaeleweka wazi kuwa Wayahudi walimuasi Mtume wao Nabii Mussa (a.s), wakaiasi amri yake, wakamuudhi na wakaiabudia ndama alipokuwa hayupo, kisha walifanya njama dhidi ya Hurun nduguye Mussa (a.s) na walikaribia kumuua. Kwa ajili hiyo walipewa adhabu ya unyonge na umaskini na wakastahiki adhabu ya Mwenyezi Mungu, yakiwa ni malipo yao kwa matendo waliyokuwa wakiyafanya. Walirtadi baada ya kuamini kwao na wakafanya njama dhidi ya Mitume ya Mwenyezi Mungu na kumpinga Mtume kila alipowaambia jambo wasiololitaka.
Ebu tulinganishe maelezo haya ya Mayahudi na hali halisi katika Uislamu.
1.     Nabii Mussa (a.s) alimuomba Allah ajalie nduguye Haruna awe Msaidizi wake na Allah alikubali, Harun naye akawa Mtume kama alivyokuwa Mussa (a.s). Mtume Mohammad (S.A.W) naye alimuomba Allah amfanye nduguye Imam Ally (a.s) kuwa khalifah baada yake na ikawa hivyo, hata kama Baadhi ya Masahaba walimzuia Imam Ally (a.s) kuongoza dola ya kiislamu lakini bado Mashia wanafuata mungozo wa Imam Ally mpaka leo hii kama imam na khalifah wa kwanza wa Mtume.
2.     Mtume alimteua Imam Ally (a.s) kuwa khalifah baada yake lakini baadhi ya Masahaba walifanya njama na kumzuia kuwaongoza waislamu
3.     Omar bin Khatab (R.A) alikuwa akimpinga Mtume Mohammad (S.A.W) katika kila tukio aliloona halipendi yeye Omar na wafuasi wake wanamsifu kwa hilo hadi leo hii. Kwa mfano Omar alimpinga Mtume katika sulhu ya Hudaibiyya, Msiba wa Alhamis, na pia aligoma kujiunga na jeshi la Usama bin Zaid.