Mashia
mara kwa mara tumetuhumiwa kwa imani ya Tahrif ndani
ya Qur'an, ambayo maana yake ni kuamini kwamba Qur'an
imepotoshwa na haiko sawa na ile aliyoteremshiwa Mtume
Muhammad (s.a.w.w.).
HII SI
KWELI!!! (Madai haya hutolewa na maadui wa Uislamu ili kuzuia umoja baina yetu)
Wanavyuoni
wakubwa wote wa Shi’ah Imaamiya tangu siku za mwanzo hadi karne za sasa wanaamini
kuwa Qur’an imehifadhiwa kikamilifu. Wanavyuoni mashuhuri wa Shia wa mwanzoni
wamesema hivi wazi katika vitabu vyao, miongoni mwao ni:
- Shaykh
al-Saduq (aliyefariki 381 AH), Kitabu'l-Itiqadat,
(Teheran.1370) Uk. 63;
- Shaykh
al-Mufid (aliyefariki 413 AH), Awa'ilu l-Maqalat,
Uk. 55-6;
- Sharif
al-Murtadha (aliyefariki 436 AH), Bahru 'l-Fawa'id (Teh,
1314) Uk. 69;
- Shaykh
at-Tusi (aliyefariki 460 AH), Tafsir at-Tibyan,
(Najaf, 1376), Juz. 1 Uk. 3;
- Shaykh
at-Tabrasi (548AH), Majma'u 'l-Bayan,
(Lebanon), Juz. 1 Uk. 15.
Baadhi ya
Wanavyuoni waliokuja baadaye waliotoa maoni kama hayo ni:
- Muhammad
Muhsin al-Fayd al-Kashani (aliyefariki 1019 AH), Al-Wafi,
Juz. 1 Uk.273-4,
- al-'Asfa
fi Tafsir al-Qur'an, Uk. 348;
- Muhammad
Baqir al-Majlisi (aliyefariki 1111 AH), Bihar al-'Anwar,
Juz 89 Uk. 75.
Imani hii
iliendelea bila ya kukatizwa mpaka leo hii.
Wanavyuoni
wa Shia wa karne hii waliokariri imani hii, kwamba Qur’an imehifadhiwa
kikamilifu na
haikubadilishwa,
ni wale miongoni mwa wenye majina mashuhuri kama vile:
- Sayyid
Muhsin al-Amin al-'Amili (aliyefariki 1371 AH);
- Sayyid
Sharaf al-Dinal-Musawi (aliyefariki 1377 AH.);
- Shaykh
Muhammad Husein Kashif al-Ghita' (aliyefariki 1373 AH);
- Sayyid
Muhsin al-Hakim (aliyefariki 1390 AH);
- 'Allamah
at-Tabataba'i (aliyefariki 1402 AH);
- Sayyid
Ruhullah al-Khumayni (aliyefariki 1409 AH);
- Sayyid
Abu al-Qasim al-Khu'i (aliyefariki 1413 AH)
- Sayyid
Muhammad Ridha al-Gulpaygani (aliyefariki 1414 AH).
Hii, kwa
kweli, si orodha nzima.
Swali: Lakini ni vipi kuhusu Mashia waliokuwapo kabla ya Wanavyuoni
hawa, je wao waliamini tahrif?
Hapana!
Hebu chukulia mfano wa 'Ubaydullah b. Musa al-'Absi (120-213
AH), Mwanachuoni wa Shia mwaminifu ambaye masimulizi yake kutoka kwa Maimamu
yanapatikana katika mkusanyo wa Hadith wa Shia kama vile al-Tahdhib
na al-Istibsar.
Hebu na tuangalie baadhi ya Wanavyuoni wa Sunni
wanasema
nini kumhusu 'Ubaydullah b. Musa al-'Absi:
_ “...
ni mcha Mungu, miongoni mwa Wanavyuoni muhimu wa Shia
...alikubaliwa
kuwa mwaminifu na Yahya b. Ma’in. Abu Hatim amesema:
‘Alikuwa
mwaminifu, mkweli...’ al-'Ijli amesema kwamba yeye alikuwa ni
mtu mwenye
cheo kikuu katika elimu ya Qur’an...”
[Al-Dhahabi,
Tadhkirat al-Huffaz (Haydarabad, 1333
AH), Juz. 1 Uk. 322]
_ “...Yeye
alikuwa ni Imam katika Fiqh, Hadith na Qur'an, alisifika kwa
uchaji
Mungu na wema, lakini alikuwa mmoja kati ya wakuu wa Shia.”
[Ibn
al-'Imad al-Hanbali, Shadharat al-Dhahab (Cairo,
1350 AH), Juz. 2 Uk. 29]
Kama
wanavyuoni hawa wa Sunni wangeona kuwa yeye aliamini kuwapo kwa Qur’an
nyingine, basi hata mmoja wao asingelimsifu kwa ujuzi wake!
Na
Ubaydullah alikuwa akichukuliwa kuwa ni mwaminifu sana, licha ya kuwa alikuwa
ni Shia, kiasi kwamba Wanavyuoni maarufu wa kisunni wa Hadith, al-Bukhari,
Muslim na wengineo wengi, katika mikusanyiko ya Hadith, wamechukuwa Hadith
kutoka kwake!
[The
Creed of the Imaam of Hadeeth al-Bukhari (Salafi Pub., UK,
1997), Uk. 87-89]
Swali: Je
Shia hawaamini Msahafu wa Fatimah ambao
mkubwa mara tatu ya ukubwa wa Qur'an?
Qur'an ni Mushaf
(Kitabu), lakini, si kwamba kila kitabu lazima kiwe Qur’an!
Hakuna kamwe “Qur'an ya Fatimah”! Mushaf Fatimah kilikuwa
ni kitabu kilichoandikwa au kuelezwa na Fatimah (a.s.) baada ya kufariki Mtume
(s.a.w.w). Hicho si sehemu ya Qur’an na hakina uhusiano wowote na amri za
Mwenyezi
Mungu au hukmu za kisharia.
Swali:
Lakini je, hakuna Hadith katika vitabu vya Shia zinazotaja Aya za Qur’an zenye
maneno mengine zaidi ya hii tuliyo nayo leo?
Kuna
baadhi ya mifano ambapo maneno zaidi yametajwa lakini kwa minajili ya kufafanua
tu, haimaanishi kwamba Aya asili za Qur’an zimegeuzwa. Hii hutokea pande zote,
kwa upande wa Shia na wa Sunni. Hebu zingatia mifano ifuatayo, yote ni kutoka
upande wa sherhe maarufu za Qur’an za Sunni:
_ “Ubayy
b. Ka'b alikuwa akisoma ‘…basi wale mnao faidi nao kwa
kipindi maalum, wapeni mahari yao kama ilivyoamriwa…’
(Qur'an, Sura 4, Aya 24), na Ibn Abbas
pia alikuwa akisoma hivyo hivyo.”
[Fakhr
al-Din al-Razi, Mafatih al-Ghayb (Beirut,
1981), Juz. 9 Uk. 53]
[Ibn
Kathir, Tafsir al-Qur'an al-'Adhim (Beirut,
1987), Juz. 2 Uk. 244]
Maelezo
yaliyomo katika hashia ya Tafsir ya Ibn Kathir yanafafanua kwamba maneno
yaliyoongezwa hapo juu, ambayo si sehemu ya Qur’an, yalisomwa na maswahaba wa
Mtume (s.a.w.w.) kwa ajili ya tafsir na
ufafanuzi tu.
_ “Ibn
Mas'ud amesema: “Wakati wa Mtume (s.a.w.w.) tulikuwa tukisoma, ‘Ewe Mtume wetu (Muhammad) fikisha lile ulilotumwa
kutoka kwa Mola wako nalo ni 'Ali ni Bwana wa Waumini na kama
hukufanya, basi hujafikisha ujumbe Wake.’” (Qur'an Sura 5, Aya 67).
[Jalal al-Din
al-Suyuti, Durr al-Manthur,
Juz. 2 Uk. 298]
Katika
hali hii pia inavyoonyesha, kipande kilichoandikwa kwa mshazari (italics)
kwa hakika si sehemu ya Qur'an, hata hivyo, swahaba Ibn Mas'ud alikuwa akisoma
hivyo alipokuwa akifafanua ufunuo wa Qur’an.
Swali: Ni
vipi kuhusu zile Hadith zisemazo kwamba baadhi ya Aya si sehemu ya Qur'an?
Shia
hawaamini kwamba mwandishi au mpokezi ana kinga ya kutofanya makosa, na kwa
hivyo hawachukulii kwamba Hadith zote ni sahihi. Kitabu pekee chenye kinga ya
kutokuwa na kosa lolote ni Qur'an. Mara nyingi Hadith hizi huchukuliwa kuwa ni
dhaifu au maneno yaliyo teremshwa nje ya Qur’an.
_ Ni
vizuri itajwe kwamba kuna baadhi ya Hadith kwenye Sahih al-Bukhari na Sahih
Muslim zisemazo kwamba Aya nyingi za Qur’an haziko. [Al-
Bukhari, Al-Sahih, Juz. 8 Uk. 208;
Muslim, Al-Sahih, Juz. 3 Uk.
1317].
_ Si
hivyo tu, Hadith hizi za Sunni zadai kwamba Sura mbili za Qur’an hazipo, ambapo
mojawapo ni kama Sura ya al-Bara’ah (Sura ya 9) kwa kirefu!!! [Muslim,
Al-Sahih, Kitab al-Zakat, Juz. 2 Uk.
726].
_ Hata
kuna baadhi ya mapokezi ya Hadith ya Sunni yanayodai kuwa Sura ya al-Ahzab (33)
ilikuwa ni ndefu kama ilivyo Sura ya al-Baqarah!!!
Ambapo
hakika Sura ya al-Baqarah ndio Sura iliyo kubwa zaidi katika Qur'an. Kuna hata
Hadith ndani ya Sahih al-Bukhari na
Muslim ambazo zimetaja kwa urefu baadhi ya Aya
ambazo hazipo. [Al-Bukhari, Al-Sahih, Juz.
8 Uk. 208].
Kwa bahati
nzuri, Shia katu hawajawatuhumu ndugu zao Sunni kwa kuamini kwamba Qur’an
haikukamilika. Sisi tunasema kwamba Hadith hizi za Sunni, ama ni dhaifu, au
zimezushwa.
Hitimisho:
“Sisi
MASHIA twaamini kwamba Qur'an ambayo Mwenyezi Mungu alimteremshia Mtume wake
Muhammad (s.a.w.w.) ni kama ile iliyoko baina ya jalada mbili. Na ndiyo hiyo
hiyo iliyoko mikononi kwa watu.
Na
anayedai kuwa sisi tunasema kwamba (Qur’an) ni tofauti kuliko hii (ya
sasa),
huyo ni muongo.”
[As-Saduq, Kitabu'l-I`tiqadat
(Tehran: 1370 AH) Uk. 63; Tafsir ya kiingereza,
The Shi'ite
Creed, tr. A.A.A. Fyzee (Calcutta: 1942) Uk. 85].
Hakika Mashia wanaamini Qur'an tuliyonayo ni timilifu na isiyokuwa na kasoro. Kama haitoshi ndugu hawa wanaamini kuwa Qur'an iliandikwa na kukamilika Katika zama za Uhai wa Mtume mwenyewe na ni yeye aliyesimamia uandishi wake.
ReplyDelete