Amesema Mtume Mohammad (S.A.W) kuwaambia Masahaba wake, “Bila
shaka Mtafuata nyendo za waliokutangulieni shubiri kwa shubiri na dhiraa kwa
dhiraa (Hatua kwa hatua au kidogo kidogo) hata kama wataingia katika shimo la
kenge, mtawafuata”. Masahaba wakauliza, “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni
wayahudi na wakristo?” Mtume akajibu, “Ni nani basi (kama sio hao)?”
Rejea:
1. Sahihi bukhari juzuu 4 ukurasa wa 187
2. Sahihi Muslim juzuu ya 8 ukurasa wa
57
3. Musnad Ahmad bin Hambal juzuu ya 3
ukurasa wa 84 na 94
Ndani ya Qur’an na katika
Historia sahihi inaeleweka wazi kuwa Wayahudi walimuasi Mtume wao Nabii Mussa (a.s),
wakaiasi amri yake, wakamuudhi na wakaiabudia ndama alipokuwa hayupo, kisha
walifanya njama dhidi ya Hurun nduguye Mussa (a.s) na walikaribia kumuua. Kwa ajili
hiyo walipewa adhabu ya unyonge na umaskini na wakastahiki adhabu ya Mwenyezi
Mungu, yakiwa ni malipo yao kwa matendo waliyokuwa wakiyafanya. Walirtadi baada
ya kuamini kwao na wakafanya njama dhidi ya Mitume ya Mwenyezi Mungu na
kumpinga Mtume kila alipowaambia jambo wasiololitaka.
Ebu tulinganishe maelezo haya ya Mayahudi na hali halisi
katika Uislamu.
1. Nabii Mussa (a.s) alimuomba Allah
ajalie nduguye Haruna awe Msaidizi wake na Allah alikubali, Harun naye akawa
Mtume kama alivyokuwa Mussa (a.s). Mtume Mohammad (S.A.W) naye alimuomba Allah
amfanye nduguye Imam Ally (a.s) kuwa khalifah baada yake na ikawa hivyo, hata
kama Baadhi ya Masahaba walimzuia Imam Ally (a.s) kuongoza dola ya kiislamu
lakini bado Mashia wanafuata mungozo wa Imam Ally mpaka leo hii kama imam na
khalifah wa kwanza wa Mtume.
2. Mtume alimteua Imam Ally (a.s) kuwa
khalifah baada yake lakini baadhi ya Masahaba walifanya njama na kumzuia
kuwaongoza waislamu
3. Omar bin Khatab (R.A) alikuwa
akimpinga Mtume Mohammad (S.A.W) katika kila tukio aliloona halipendi yeye Omar
na wafuasi wake wanamsifu kwa hilo hadi leo hii. Kwa mfano Omar alimpinga Mtume
katika sulhu ya Hudaibiyya, Msiba wa Alhamis, na pia aligoma kujiunga na jeshi
la Usama bin Zaid.
No comments:
Post a Comment