Mawahhabi wanadai kuwa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab alikuwa akihubiri
mawazo yake kwa ajili ya kujipatia utukufu katika imani yake katika upweke wa
Allah swt na kuwakomboa Waislamu wasitumbukie katika Shirk. Wao wanadai kuwa Waislamu wamekuwa wakitenda
dhambi ya Shirk kwa karne sita mfululizo na hivyo yeye alikuja kuirejesha upya
dini ya Uislamu. Yeye anazitoa Ayah za Qur’an Tukufu nambari 5 ya Surah
al-Ahqaf, Ayah 106 surah Yunus, Ayah 14
sura al-Ra’d ili kwamba Waislamu wote wakubaliane na mawazo yake. Hata hivyo,
zipo Ayah nyingi kama hizo, na Maulamaa wanasema kuwa hizo Ayah zimekuwa
zikiwazungumzia makafiri waliokuwa wakiabudu miungu na masanamu au waliokuwa washirikina.
Kwa mujibu wa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab, Mwislamu anakuwa Mushrik pale anapoomba kwa Mtume
Muhammad s.a.w.w, au kwa Mtume a.s. mwingine, au walii au mcha Mungu karibu na
kaburi au mbali kutoka hapo, yaani, iwapo anapomwomba msaada wa kutokana na
shida aliyonayo, au anapoomba kutetewa mbele ya Allah swt kwa kutaja jina lake au anapotaka kuzuru kaburi lake. Allah swt anatuambia kuhusu makafiri wanaoabudu miungu na masanamu katika Ayah ya tatu ya surah al-Zumar, lakini
Mawahhabi wanaonyesha Ayah hii kama ndio waraka wa kuhalalisha utumiaji wao wa
neno la Mushrik kwa ajili ya Waislamu
waombao kwa kuwaweka Mitume a.s. au Mawalii kama ndio watu walio baina yao na
Allah swt. Wao wanasema kuwa hata Mushrik waliokuwa wakiabudu miungu pia
walikuwa wakijua kuwa vyote vilikuwa vimeumbwa na Allah swt. Wao wanasema kuwa
Allah swt amebainisha: Na kama ukiwauliza, Ni nani aliyeumba mbingu
na ardhi na akalitiisha jua na mwezi?” Bila shaka watasema, Allah (Surah
Ankabut, ayah ya 61 na Sura Zukhruf, Aya ya 87). Wao wanadai kuwa hao Mushrik walikuwa hivyo makafiri Mushrik si kwa sababu walikuwa wakiamini
hivyo bali wao walizungumza kama ilivyosemwa katika Ayah ya 3 ya Surah
az-Zumar: Wale wanaofanya wengine kuwa
marafiki badala ya Allah, wanasema, “Wao wanatusaidia kutufikisha karibu (ya
Allah swt) kwa kututetea mbele Allah” Wao wanadai kuwa Waislamu wanaoomba
katika makaburi ya Mitume, ma-Awliya’ kwa utetezi na misaada basi wanakuwa Mushrik kwa kusema hivyo.
Ni jambo la kipumbavu kabisa kwa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab kuwasema
Waislamu wanakuwa makafiri na Mushrik
kwa Ayah hiyo. Kwa sababu, makafiri wanawaambudu masanamu ili kwamba ni masanamu hayo tu ndiyo
yatakayowasaidia kuwatetea wao; wao wanamwacha Allah swt na badala yake wanakuwa na imani moja tu ya
kuwaomba miungu na masanamu hayo kuwa watetezi wao. Lakini ni uhakika uliyo bayana kuwa Waislamu
kamwe hawawabudu Mitume a.s. au Ma-Awliya’ lakini wanayo imani kuwa kila kitu kinatoka
kwa Allah swt. Sisi tunapenda kuwa hao ma-Awliya’
wawe ni Wasila wetu.
Makafiri wanaamini kuwa miungu na masanamu yao inawaombea chochote kile
wakitakacho na kumfanya Allah swt kuwatimizia chochote kile wakitakacho.
Wakati ambapo, Waislamu
wanaomba msaada wa Awliya’ ambao wanawajua kuwa hao ndio watumwa
wapenzi wa Allah swt, kwa sababu Allah
swt ameahidi katika Qur’an tukufu kuwa Yeye atawaruhusu waja wake wapenzi
kuwatetea na atakubali utetezi wao na Sala na kwa sababu Waislamu wanaamini
ubashiri mzuri katika Qur’an. Kamwe huwezi kulinganisha baina ya kafiri
anayeabudu miungu na masanamu na Waislamu wakiomba msaada wa Awliya’.
Waislamu na Makafiri wote ni binadamu
kwa miili, na wanafanana kwa
kuonekana, lakini Waislamu ni marafiki wa Allah swt na watakuwa Peponi milele
wakati ambapo Makafiri ni maadui wakubwa wa Allah swt na watakuwa Motoni milele. Kujionesha kwao hakumaanishi kuwa watabakia
vivyo hivyo daima. Wale wanaowaabudu
masanamu na miungu ambao ndio maadui wakubwa wa Allah swt, yatawafikisha hadi
kuingia Jahannam. Lakini wale wanaowafanya marafiki wa Allah swt kuwa marafiki
wao, basi Allah swt atawabariki na kuwarehemu.
Ipo Hadith isemayo: Rehema za Allah
swt zinateremka pale waja wake wapenzi wanapotajwa, nayo pia inatuonyesha
kuwa Allah swt ataonyesha rehema zake na misamaha yake pale Mitume a.s. na Awliya’
wanapoombwa.
Waislamu wote kwa pamoja wanatambua waziwazi kuwa Mitume a.s. na Awliya'
si watu wa kuabudiwa na wala si washiriki wa Allah swt. Waislamu wanatambua vile vile kuwa wapo waja
wa Allah swt ambao hawastahili kuombwa na papo hapo wapo waja wengineo ambao
maombi yao hukubaliwa Kwake. Katika
surah Maidah, Ayah ya 35 tunaambiwa: “Tafuteni
Wasila wa kunifikia Mimi” Allah swt
anamaanisha kuwa Yeye atakubalia ibada za waja wake halisi na kuwapatia kile
wakiombacho. Tunapata Hadith sharif iliyonakiliwa na al-Bukhari, Muslim na
katika Kunuz ad-daqaiq, isemayo: “Kwa hakika, wapo wacha Mungu halisi wa Allah
swt ambapo Yeye anawaumbia kile walacho kiapo; kamwe hawasingizii.” Waislamu
wanawachukulia Awliya' kama Wasila na kutegemea maombi na msaada wao kwa sababu
wao wanaamini Ayah na hadith za hapo juu.
No comments:
Post a Comment