Muda mfupi baada ya Abubakar
kujinyakulia madaraka ya kuongoza Uislamu pale Saqifat Bani Saidah, Bi Fatumah
alikwenda kwa Maanswar kuwaomba watekeleze maagizo ya Mtume kwa kumpatia baia
Ally ibn Abi Talib, lakini Maanswar wakamwambia tayari tumekwishampa Abubakar
na kwamba kama angekwenda mapema wasingempatia baia mtu yeyote isipokuwa Ally.
Kwa hili Imam Ally anasema, “hivi kweli ni busara nimuache Mjumbe wa Allah
nyumbani kwake bila kumzika ili tu nitoke kuja kugombana na watu juu ya cheo changu?”
Fatumah naye akasema, “alichofanya Abul-Hassan ndicho kilichompasa kukifanya,
na wao wamefanya jambo ambalo Mwenyezi Mungu atawauliza na atawalipa (kwa tendo
la kupora madaraka).
Tazama:
tarikh Al-Khulafaa cha ibn Qutaibah J. 1 uk. 19 na Sharh Nahjul Balagha cha ibn
Abil Hadid (Baiatu Abubakar).
Kwa dhuluma aliyoifanya
Abubakar na wenziwe dhidi ya Ahlulbayt wa Mtume, Bi Fatumah alimchukia Abubakar
kiasi kwamba alipokufa aliagiza Abubakar asihudhurie mazishi yake na wala
asijue kaburi lake lilipo. Hivyo Mmewe alimzika bibi huyo usiku na mpaka leo
hakuna kauli moja inayoonesha kaburi la bi Fatumah lilipo.
Tazama:
sahihi Bukhar J. 3 uk 36, na Sahih Muslim J. 2 uk. 72
Hivyo utagundua kuwa bibi
huyo mtukufu ambaye Mtume alimtangaza kuwa mmoja wa wanawake bora zaidi
ulimwenguni akiwa kati ya wanawake bora wane tu, alihitaji mazishi yake liwe
fundisho kwa waislamu ili wajiulize kuna kitu gani kilitokea baina yake na
watawala wa zama hizo. Na kwa hakika tumekwisha jiuliza na kujuwa hujuma uliza
fanyiwa ewe mama wa Makhalifa na maimamu watukufu.
No comments:
Post a Comment