Mtume wa Allah alisema, “Wana wa Israel walifarakana na kuwa
makundi 71, Manaswara nao wamefarakana na kuwa makundi 72, na umati wangu
utafarakana na kufikia makundi 73 na yote yataingia motoni, isipokuwa kundi
moja tu.” Ebu niambieni kundi hilo enyi watu wenye akili.
Mimi nashangaa kuona waislamu wote na makundi yao wanaifahamu
hadith hii lakini hawaifanyii kazi kwa kufanya utafiti na kubaini ni kundi gani
lenye kuokoka na kuachana na makundi mengine yenye kupotoka.
Cha ajabu ni kuwa kila kundi linadai kuwa ndilo
lenye kuokoka bila kuleta ushahidi uliosahihi.
Tafadhali tufanye
utafiti ili tubaini kundi hili lenye kuokoka ili tujiunge nalo, vinginevyo
tutaangamia. Mwenyezi Mungu anasema, “Na wale wanaojitahidi kwa ajili yetu, tutawaongoza
kwenye njia zetu” Qur’an 29:69.
Na amesema
tena, “Wale ambao husikiliza kauli (zisemwazo)
wakafuata zile zilizo njema, hao ndio aliowaongoa Mwenyezi Mungu na hao ndio
wenye akili”.
Bila shaka
amesema kweli Mjumbe wa Mwenyezi Mungu pale aliposema kuwa fanya utafiti kuhusu
dini yako mpaka isemwe kuwa wewe ni maj-nun.
No comments:
Post a Comment