Friday 23 August 2013

OMAR BIN KHATAB AIPINGA QUR’AN



Katika zama za ukhalifa wa Umar bin Khatab, sahaba mmoja alimuuliza, “Ewe Amirul-muumin, mimi nimepatwa na janaba lakini sikupata maji.” Umar akamwambia, “Usisali”. Hapo Ammar bin Yasir alilazimika kumkumbusha kutayamam, lakini Umar hakuafikiana naye kwa hilo na akamwambia Ammar, “Tutakubebesha jukumu kwa yale uliyojibebesha.”
Basi yu wapi Umar na kufuata kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume? Je sio Mtume aliyewafundisha Masahaba namna ya kutawadha na kutayamam? Cha kushangaza kuna watu wanaopandisha cheo mtu huyu asiyekuwa na ujuzi wa Uislamu na kumwita al-farooq na wakati Umar mwenyewe anakiri kuwa hana elimu kuliko watu wote. Na pia alisema mara nyingi, “Lau si Ali, basi Umar angeangamia, na mpaka anakufa hakuwahi kutambua maana ya Al-kalalah ambayo alihukumu kwa hukumu nyingi tofauti tofauti kama inavyoshuhudia Historia. Omar waliwapiga watu waliomuuliza tafsiri ya Qur’an na masuala mengine ya kisheria.
Soma:
1.     Tarikh Al-Yakubi juz. 2 uk. 106
2.     Futuhul Buldan uk 437
3.     Sahihi Bukhari juz. 1 uk. 52
Tumesimuliwa masimulizi mengi juu ya Ushujaa wa Umar bin Khatab lakini ukifuatilia Historia utagundua kuwa Umar alikuwa shujaa wa kuuwa waislamu wenzake na watu wasiokuwa na hatia. Lakini anapokuwa vitani alikuwa ni mwoga kweli kweli.
Omar na wenziwe walikimbia katika vita vya Uhud, na Hunain. Pia Mtume alipomtuma katika vita vya Khaibar alirudi bila ushindi na hata katika vikosi vidogo vidogo alivyoshiriki hakupewa uongozi. Kwa mara ya mwisho aliagizwa na Mtume kuwa chini ya jeshi lililokuwa linaongozwa na kijana wa miaka 18 yaani Usamah bin Zaid bin Harith.
Umar alithubutu kumtisha Fatumah bint Rasulullah kuwa kama wasipotoka kwenda kukubali utawala wa Abubakar basi ataiunguza nyumba yake. Kama haitoshi alidiriki kuwa dhidi ya kitabu cha Allah na Sunnah za Mtume wake, akahukumu katika zama za Ukhalifah wake, hukumu zinazokwenda kinyume na Qur’an na Sunnah tukufu.
Soma:
1.     Tarikh At-Tabari na Tarikh ibn Al-Athir
2.     Al-Imamah was-Siyasah cha ibn Qutaibah
3.     An-Nas wal-Ijtihad
Uko wapi ucha Mungu wa Umar enyi watu? Kama kiongozi yuko hivi itakuwaje kwa wanaomfuata? Tafakari, chukua hatua.
Mambo mengi mazuri kumhusu Umar yaliandikwa na watu aliowaajiri ili kuhalalisha ufedhuli na dhuluma zake dhidi ya Mtume na Ahlulbayt wake na hata waislamu kwa ujumla. Lakini mtu atakayesoma vitabu kwa makini, uovu wa Umar haufichi hata ufanyeje.

No comments:

Post a Comment