Huru alipewa amri na Yazid bin Muawiyyah (Khalifah wa
Mawahhabi) kuongoza kikosi kimojawapo kwa ajili ya kumpiga vita Imam Hussein
Mjukuu wa Mtukufu Mtume Mohammad (S.A.W.W) mpaka pale Imam atakapokuwa tayari
kuwa chini ya mtawala huyo aliyekuwa mlevi, mzinzi na mcheza kamari.
Kikosi cha Huru kilikuwa cha kwanza kukutana na Imam Hussein
lakini alishindwa kuanza mashambulizi, na hivyo kumlazimisha Imam na Msafala
wake kwenda katika eneo linaloitwa Karbala na hapo walikuwepo askari wa Yazid
wengi zaidi na amri ikatoka kwa Ziyad bin Abih aliyekuwa gavana wa eneo hilo ya
kwamba Imam Hussein akatwe kichwa mara moja.
Huru alianza kutetemeka kama kuti, na baadhi ya wenziwe
walipomuuliza kuwa, “Je wewe unaogopa kufa?” Huru alijibu, Wallahi hapana,
lakini ninaihiyarisha nafsi yangu baina ya pepo na moto.” Kisha hapo hapo
alimpiga farasi wake, akaenda kwa Imam Hussein akamuuliza, “Ewe mwana wa Mjumbe
wa Mwenyezi Mungu naweza kutubia?” Basi Huru alikubaliwa kuwa miongoni mwa
wapiganaji wachache aliokuwa nao Imam Hussein na akawa mtu wa kwanza kuuwawa
akiwa upande wa Imam Hussein (a.s).
Nami natamani kuwa kama Huru na niwe wa kwanza kuuliwa nikiwa
upande wa haki.
No comments:
Post a Comment