Imam Hussein alipouliwa na vikosi vya jeshi vilivyosheheni wanafiki
waliotumwa na Yazid bin Muawiyyah, alikatwa kichwa, kikachomekwa juu ya mkuki
na kutembezwa mbele ya msafala wa jeshi la Yazid na mateka wao yaani wajukuu na
vitukuu wa kike wa Mtume Mohammad (S.A..W.W) miongoni mwao akiwamo Zainabu bint
Ally and Sukaina bint Hussein. Mateka hawa wa kike walikuwa wamevuliwa hijabu, kusimangwa
na kuzomewa kila walikopita mpaka walipofika makao makuu ya utawala wa Bani
Umayyah yaliyokuwa katika msikiti ya Umayyah ulioko Damascus Syria.
Walipofika huko mateka walipewa wasaa wa kujitetea ili
wasiuliwe kama walivyouwawa ndugu zao wa kiume. Bi Zainabu alisimama na
kuulaumu utawala wa Yazid kutokana na dhulma yake juu ya Uislamu na Waislamu.
Akamwambia, “hata mfanye juhudi za kiasi gani kuufifiza utajo wa Ahlulbayt
hamtoweza kwani sisi tumeinuliwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake.”
Alisema kweli Bi Zainab kwani leo utajo wa Ahlulbayt unazidi
kuongezeka na watu wanaotumia majina yao ni wengi kiasi kwamba karibia kila
nyumba utakuta jina la Ahlulbayt limetumika. Kinyume chake unaweza kuzunguka
mji mzima na ukakosa mtu anayeitwa Yazid, Muawiyyah, Hindu au Abusufian. Hawa
watu wane walikuwa ni msingi wa madhila yaliyowakuta Ahlulbayt Rasulullah na
waislamu kwa ujumla.
Kiwiliwili cha Imam Hussein (a.s) kilizikwa na Mashia wake
hapo hapo Karbala na kichwa chake kikazikwa na maadui zake katika msikiti wa
Banu Umayyah huko Damascus Syria.
No comments:
Post a Comment