Mawahhabi wanadai kuwa kuzuru makaburi, kuyagusa na kuwaomba
watu wema na kutabaruku kwao ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Ukweli ni kuwa Kuyagusa makaburi na na kuwaomba wenye
makaburi hayo ni shirki tu endapo kama muombaji atakuwa anaamini kuwa marehemu
hao wanadhuru na kunufaisha. Lakini waislamu wanampwekesha Allah na wanafahamu
kwamba ni Allah pekee ndiye mwenye kudhuru na kunufaisha na wao wanaomba
mawalii wa Allah na maimamu ili wawe ni wasila tu na hii sio shirki.
Masunni na Mashia wanakubaliana juu ya hilo tangu zama za
Mtume mpaka leo, isipokuwa Mawahhabi ambao ni wanachuoni wa Saudia wameikhalifu
ijmai ya waislamu kwa Madhehebu yao mapya ambayo yalianzishwa katika karne ya
18 miladia. Kwa hakika hawa Mawahhabi wamewafitini waislamu kutokana na itikadi
yao hii na wamewakufurisha na kuhalalisha kumwaga damu zao, wao huwapiga wazee
miongoni mwa mahujaji wa nyumba tukufu ya Allah kwa kusema tu, “Assalaam alayka
yaa Rasulullah” na hawamruhusu yeyote kugusa kaburi tukufu ya Mtume wetu. Hii
ni dhulma kwa Mtume na waislamu kwa ujumla.
Sayyid Sharafuddin (sheikh wa Shia) alikwenda kuhiji nyumba
tukufu zama za Mfalme Abdul Aziz Al-Suud, siku ya idd akaenda kusalimiana na
mfalme na akampa mfalme huyo zawadi ya Qur’an iliyofungwa ndani ya ngozi, naye
mfalme alifurahi na akaubusu Msahafu huo na kuuweka juu ya paji lake la uso kwa
kuuheshimu na kuutukuza. Hapo ndipo Sayyid Sharafuddin alipomuuliza mfalme,
‘ewe mfalme, kwanini unaibusu ngozi na kuitukuza wakati hiyo ni ngozi ya
mbuzi?’ Mfalme alijibu, ‘mimi nimeikusudia Qur’an tukufu ambayo imo ndani ya
ngozi na sikukusudia kuitukuza ngozi.” Basi Sayyid akasema, “vema ewe mfalme,
basi ni hivyo hivyo tufanyavyo sisi tunapoyabusu madirisha ya chumba cha Mtume
au milango yake. Sisi pia tunafahamu kuwa hivyo ni vyuma tu, havidhuru wala
havinufaishi, lakini huwa tunakusudia kilichopo nyuma ya vyuma hivyo na mbao
hizo, kwa hiyo sisi hukusudia kumtukuza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.W) kama
wewe ulivyoikusudia Qur’an kwa kuibusu ngozi ya mbuzi ambayo imefunika Qur’an.
Basi waalikwa walitoa takbira “Allah akbar” kwa kufurahia maelezo ya sayyid na
wakasema umesema kweli. Jambo hili lilimlazimisha mfalme huyo awaruhusu
mahujaji kuligusa na kutabaruku kwenye kaburi la Mtume mpaka mwisho wa utawala
wake. Mfalme aliyemfuatia akarudia hoja zao dhidi ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu
na waja wema wengine.
Basi tatizo la Mawahhabi sio kwamba, hofu yao ni kuwa watu
watamshirikisha Mwenyezi Mungu, laa hasha, lakini tatizo lao ni la kisiasa na
ni kwa ajili ya kuwapinga waislamu na kuwaua ili kuimarisha ufalme wao na
utawala wao dhidi ya waislamu, na Historia ni ushahidi mkubwa juu ya mambo
waliyowafanyia umati Mohammad (s.a..w.w).
No comments:
Post a Comment