Mtume Mohammad (S.A.W.W) aliandaa jeshi ili kulikabiri jeshi
la Rumi siku mbili kabla ya kifo chake na akampa uamiri Usamah bin Zaidi ibn
Harith, aliyekuwa na umri wa miaka 18. Katika jeshi hilo Mtume aliwaamrisha
wakuu wa Muhajirina na Answar kama vile Abubakar bin Quhafah, Umar, Abu-Ubaidah
kujiunga na jeshi hilo. Miongoni mwao wapo waliopinga uamiri wa Usamah na
wakasema, itakuwaje tuongozwe na kijana ambaye bado hajakomaa?
Hivyo Mtume alitoka akiwa mgonjwa na amefungwa kitambaa
kichwani akiyumba kati ya watu wawili akapanda juu ya mimbari na kusema, “Enyi
watu ni maneno gani yanayonifikia kutoka kwa baadhi yenu kuhusu uamiri wa
Usamah, basi ikiwa mtakebehi kwa kumpa kwangu uamirijeshi Usamah, kwa hakika
mlikwisha kebehi kumpa kwangu uamiri baba yake kabla ya mwanawe. Basi namuapa
Mwenyezi Mungu kwa hakika Zaid alistahili kuwa amiri na mwanaye pia anastahili
kuwa amiri baada yake.
Tazama:
1.
Taqabat cha ibn Saad Juz. 2 uk. 190
2.
Tarikh Ibn al-Athir juz. 2 uk. 317
3.
Tarikh At-Tabari Juz. 3 uk. 226
4.
As-Siratul Halabiyyah ju. 3 uk. 207
Kisha Mtume akawa anawahimiza wafanye haraka kwenda kuungana
na jeshi la Usamah ili kuindinda nchi. Lakini mpaka Mtume anafariki Masahaba
wengi wakiwemo Abubakar na Umar walikuwa hawajajiunga na jeshi la Usamah,
vinginevyo wasingekuwapo Madinah wakati Mtume alipofariki.
Ukweli wa tukio hili ni kuwa kwa mara nyingine tena Baadhi ya
Masahaba walipinga amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Rejea Qur’an 33:36 na
59:7 upate maelekezo ya Mwenyezi Mungu juu ya kumtii Mtume wake.
Ikiwa tutataka kufanya mazingatio katika kisa hiki tutagundua
kuwa Khalifah Umar bin Khatab ndiye chimbuko la upinzani huu kwani baaada ya
kifo cha Mtume alikwenda kwa Khalifah Abubakar na akamtaka amuuzulu Usamah na
kumbadilisha na kuweka amiri mwingine. Abubakar akamwambia, “mama yako amekula
hasara ewe mwana wa Khatab, waniamuru nimuuzulu na hali ya kuwa Mtume wa
Mwenyezi Mungu alimtawalisha?”
Tazama:
1.
Taqabat al-Qubra cha Ibn Saad juz. 2 uk. 190
2.
Tarikh At-Tabari juz. 3 uk. 226
No comments:
Post a Comment