Baadhi ya wapinzani wa USHIA wamekuwa wakipotosha suala hili
la Mashia kusujudu juu ya udongo kwa kudai kuwa mashia tunasujudia udongo.
Ukweli ni kuwa tunamsujudia Mwenyezi Mungu kwa kusujudu juu ya udongo kama
ambavyo nao husujudu juu ya mazuria. Ukisema kwa kusujudu juu ya udongo basi
tumeabudu udongo utakuwa unamaanisha vilevile kuwa anayesujudu juu ya zuria
atakuwa ameabudu zuria.
Kwetu Mashia sijidah ni kwa ajili ya Allah pekee, na
kilichothibiti kwetu sisi na kwa Masunni ni kwamba, kilichobora ni kusujudu juu
ya ardhi au kitu kilichoota ardhini kisicholiwa, na wala haisihi kusujudu juu
ya kitu kinginecho.
Mtume Mohammad (S.A.W.W) alikuwa akitandika udongo na makuti kisha
kusujudu juu yake, na aliwafundisha Masahaba wake (R.A) wakawa wanasujudu juu
ya ardhi na changarawe, na akawakataza kusujudu kwenye nguo au ncha za nguo
zao. Mambo haya kwa Mashia yanajulikana bila hata kuulizana dalili.
No comments:
Post a Comment