Ibn Abas
anasema kuwa, “Siku ya Alhamis, hiyo siku ya Alhamis ilikuwa na tukio gani?
Mtume wa Mwenyezi Mungu yalimzidia maumivu yake akasema, njooni nikuandikieni
maandiko ambayo hamtapotea baada yake. Umar bin Khatab akasema Mtume anaweweseka
kwa kuzidiwa na maradhi, nanyi mnayo Qur’an, Kinatutosha kitabu cha Mwenyezi
Mungu, basi hapo watu waliokuwepo ndani ya nyumba ya Mtume wakakhitilafiana na
kuzozana juu ya kuandikiwa wosia. Wapo waliotaka wasogee ili Mtume awaandikie
wosia na wapo waliopinga na kusema kama alivyosema Omar bin Khatab kuwa Qur’an
inawatosha. Masahaba walipozidisha zogo Mtume akawafukuza”.
Ibn Abas
anasema, huu ndio msiba mkubwa kuliko yote katika Uislamu kwani Masahaba
walimzuia Mtume wao kuandika wosia.
Soma:
Sahihi Muslim, Juz. 5 uk. 75 mwishoni wa kitabul-wasiyyah.
Mpaka hapa
nashangazwa na msimamo wa Umar bin Khatab dhidi ya amri ya Mtume Mohammad
(S.A.W) juu ya kuulinda umma usipotee na bila shaka maandishi hayo yangesaidia
kuondoa khitilafu baina ya waislamu.
Hivi Omar
anaposema kuwa ninyi mnayo Qur’an, nayo inatutosha anamaana gani? Je, Omar
anafahamu Qur’an zaidi ya Mtume Mohammad (S.A.W.W)? Hili haliwekani bali tabia
ya Omar ni kumpinga Mtume kwa kila maagizo ayatoayo kwa waislamu. Nadhani
unakumbuka msimamo wa Masahaba katika sulhu ya Hudaibiyyah ambapo Omar
aliongoza uasi dhidi ya Mtume wetu kwa mara nyingine.
Lakini kama
kweli walifahamu kuwa Mtume anaweweseka, kwa nini alipowafukuza chumbani
walitoka? Hii inamaana kuwa waligoma kumruhusu Mtume kuandika wosia kwa sababu
walijua Mtume alitaka kuandika nini na hivyo wakaona wamzue kuandika ili
wafanye wanavyotaka pindi atakapofariki dunia.
Matendo haya
ya Omar bin Khatab yanapingana na Qur’an 49:2
isemayo, “Enyi mlioamini msipaze sauti zenu juu ya sauti ya Mtume na wala
msisemezane naye kwa sauti ya nguvu kama mnavyosemezana ninyi kwa ninyi, visije
vitendo vyenu vikakosa thawabu na hali ya kuwa hamtambui”.
Katika tukio
hili walivuka mipaka ya kupaza sauti na kumsemesha kwa nguvu hadi wakamtuhumu
Mtume kwa kuweweseka. Waislamu nakuombeni mjitenge mbali na watu walioongoza
fitina ndani ya Uislamu na kumdhulumu Mtume wetu kwa kumzuia kuuongoza Uislamu
kwa misingi aliyoagizwa na Mola wake. Pia jitengeni na watu wanaoongoza kwa
kutenganisha watu kwa kuwasingizia waislamu wengine kuwa ni makafiri ili wapate
sababu ya kuwaua.
No comments:
Post a Comment