Masahaba wa Mtume Mohammad
(S.A.W.W) wamegawanyika katika makundi makuu manne:
1. Masahaba
wema
Masahaba hawa walimtambua Mwenyezi Mungu na
Mtume wake kwa maarifa ya kweli kabisa na wakamuunga mkono Mtume Mohammad
(S.A.W.W) kwa dhati na kusuhubiana naye kwa ukweli katika kauli na utakaso wa
moyo katika matendo, na wala hawakugeuka baada yake, bali waliimarika katika
ahadi waliyomuahidi. Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamewasifia Masahaba hawa kwa
dhati kabisa. Mfano wa Masahaba wema ni Abudhar bin Ghiffar, Ammar bin Yasin,
Salman Farsii, Mohammad bin Abubakar na Bilal bin Rabah.
2. Masahaba
waliosimu kwa woga au kupenda jambo fulani la waislamu.
Masahaba hawa kuna kipindi walimfuata Mtume
na wakati mwingine walimpinga na kumuudhi Mtume kwa kuacha kufuata maagizo yake
na kufanya makatazo yake. Maoni yao waliyapa nguvu juu ya hukumu tukufu za
Qur’an na Qur’an iliwakemea mara nyingi watu hawa. Mfano wa Masahaba hawa ni
Abusufian baba wa Muawiyyah na familia yake.
3. Masahaba
waliokuwa wanafiki
Masahaba hawa walimfuata Mtume Mohammad
(S.A.W.W) kwa lengo la kumfanyia vitimbi, wakadhihirisha Uislamu, wakaficha
ukafiri, wakajisogeza ili wauvuruge Uislamu na Waislamu. Bila shaka Mwenyezi
Mungu ametelemsha sura nzima kuwalaani aina hii ya Masahaba, akawaonya kuwa
wataingia katika tabaka la chini la moto wa Jahannam.
Mtume aliwataja baadhi yao na Sunni na Shia
tunaafikiana kuwa kuna Masahaba walikuwa wanafiki na walijulikana. Mfano ni
Abdallah bin Salun
4. Masahaba
maalumu (Ahlulbayt wa Mtume)
Majina ya Ahlulbayt ni Mtume
Mohammad mwenyewe, Ally ibn Abitalib, Fatumah bint Mohammad, Hassan bin Ally na
Hussein bin Ally (a.s)
Watu hawa wametakaswa na Allah na kuondolewa
uchafu (Qur’an 33:33). Allah amewajibisha kuwasalia sambamba na Mtume (Qur’an
8:41). Allah amewajibisha kwa kila Muislamu kuwapenda watu hawa na ndio malipo
ya utume wa Mtume Mohammad (S.A.W.W). (Qur’an 42:23). Wao ndio wenye mamlaka
ambao Mwenyezi Mungu ameamrisha kuwatii (Qur’an 4:59). Wamebobea katika elimu
(4:59). Wao ni wenye kumbukumbu ambao Mtume ametuagiza kushikamana nao, tena
akawafananisha na safina ya Nuhu ambayo mwenye kuipanda ataokoka na mwenye
kuikengeuka ataangamia.
Soma; As-sawaiqul Muhriqah ya Ibn Hajar uk.
184 na 234
Musnad Ahmad Juz. 5 uk. 182
Kanzul Umaal juz. 1 uk. 44
No comments:
Post a Comment