Saturday 23 June 2012

KITOTO KICHANGA CHATUPWA KATIKA MAJI MACHAFU



Ameokotwa mtoto wa kiume katika eneo la Unit 3 Mazimbu Campus ya Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Tanzania akiwa ametupwa katika masinki ya maji machafu. Mtoto huyo akiwa amekufa kama anavyoonekana katika picha anasemekana kutupwa na mwanachuo mmojawapo wa hapa Solomon Mahlangu (Mazimbu) campus. Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia mazingira mabaya ya wanachuo wa hapa ambao hawana hata chembe ya dini. Utawakuta wanatembea wamevaa nguo mithili ya machangudoa. Uasharati umeshamiri kwa kiwango cha juu na huwezi kuamini kwamba hawa ndio wasomi wa chuo kikuu.

Tunatoa wito kwa viongozi wa dini, hasa viongozi wa Uislam kuongeza juhudi katika kuelimisha wananchi ili wafuate mafunzo sahihi ya dini na kuacha uasharati. Nimesema uislamu kwa sababu ndio dini pekee ambayo imeonesha njia kuwaandaa waumini wake wavae nguo za stara na wajiepushe na zinaa na mambo yote machafu.

No comments:

Post a Comment