Wednesday 19 September 2012

MASHIA TUTAUAWA NA MAWAHABI MPAKA LINI

Mawahabi ambayo huitwa vilevile kama Salafi na kwa Tanzania wamejipatia jina la Answar Sunna wamekuwa msitari wa mbele kuwauwa Mashia kwa visingizio kwamba sisi si waislamu. Lakini utashangaa hivi kama sisi si waislamu wao wauaji ndio watakuwa waislamu?
Sisi hatukubaliani na fikra zao potofu za kutumia hasira na mauaji kama ngao ya kulinda dini kwa kuwa si mafundisho ya Uislamu toka kwa Mtume na Ahlulbayt wake (as). Mtume aliweza kuishi na watu wasiokuwa waislamu kwa muda wote wa uhai wake. Mfano wake ni pale alipoishi na wakristo wa Najran na hata walipoleta upinzani dhidi ya mtume Mwenyezi Mungu hakumuagiza Mtume wake awaue. Badala yake aliwaomba waapizani ili Mungu atoe hukumu mwenyewe.
Sasa hii tabia ya kumuua kila anayekwenda kinyume na Mawahabi wameipata wapi wapotofu hawa. Ninawaomba wasome Qur'an kwa mazingatio na pia waisome vizuri historia ya Mtume na Uislamu. Kwa bahati mbaya wamekuwa wakichukua mifano mibaya ya watu waliokuwa wahalifu, hakiona kuwa ndio Uislamu sahihi. Kwa mfano wanamtaja Khalid bin Walid kuwa ni mfano wa makamanda wazuri wa vita. Huyu ni mtu ambaye alifanya mauaji ya watu wasiokuwa na hatia katika kipindi ambacho Mtume alirudi Maka akitoka Madina (Fat'hu Makka), na Mtume mtukufu alimlaani kwa mauaji hayo.

No comments:

Post a Comment