Monday, 1 October 2012

MAUAJI YA WAUMINI WA MADHEHEBU YA SHIA

Shia ni waislamu wanaofuata kizazi cha Mtume Mohammad (SAWW) kwa kuwa Mtume mwenyewe aliacha amekabidhi utawala kwa Imamu Ali ambaye ni kiongozi wa Ahlulbayt wa Mtume. Lakini Mtume alipokufa tu waislamu wachache walikutanika katika ukumbi uitwao Saqifatu ban Saada na kufanya mapinduzi ambayo Abubakar bin Quhafa alinyakuwa ukhalifa.
Kuanzia siku hiyo waislamu waliofuata usia wa Mtume alipata mateso ya kila aina na kuuawa. Wa kwanza kuuawa alikuwa bint wa pekee wa mtume yaani Fatumat Zahra, ambaye alimfuata baba yake kabla miezi haijapita tokea afe mtume.
Kipindi cha mauaji kimeendelea hadi leo ambapo Mashia wamekuwa wakiuawa katika kila kona ya dunia. Nchi zilizokithiri kwa mauaji hayo ni Pakstan, Bahrain, Iraq, Yemen, Saudi Arabia na Syria. Katika mwaka 2012 peke yake katika mji mmoja tu uitwa Queta huko Pakstan wameuawa mashia zaidi ya 100.

No comments:

Post a Comment