Monday 1 October 2012

VITISHO VYA VITA VYA ISRAEL DHIDI YA IRAN

Naibu Kamanda wa majeshi ya Iran, Brigedia Jenerali Massoud Jazayeri amesama kuwa pamoja na Utawala Haramu wa Israel kuendeleza sera yake ya vitisho dhidi ya Jamhuri ya Kislamu ya Iran, inajua fika kuwa ikifyatua risasi au kombora moja tu dhidi ya Iran utakuwa ndio mwisho wa utawala huo haramu kwa Iran itawapiga vilivyo na kisha kuwakabidhi wapalestina nchi yao ili waanzishe serikali ya kidemokrasia na kushirikisha watu wa dini mbalimbali badala ya utawala wa sasa ambao ni wa kiyahudi peke yao, wengine ni vibarua wao na ukubali kufanyiwa kila watakacho.

Ameyasema hayo kwa sababu Iran inauwezo mkubwa kijeshi kuliko Israel na hivyo waziri mkuu wa Israel Benjamini Nitanyahu kujaribu bila mafanikio kuishinikiza dunia iwasaidie katika njama zao za kuishambulia Iran.

No comments:

Post a Comment