Saturday 20 October 2012

RAIS MORSI WA MISRI NI NGUVU YA SODA

Juhudi za Rais Mursi wa Misri za kutetea waislamu na Uislamu zimeonekana kuwa ni nguvu ya soda baada ya rais huyo aliyeingia madarakani kwa mgongo wa Uislamu (kupitia chama cha udugu wa kiislamu) kuonesha udhaifu mkubwa, pale alipomtuma balozi mpya kuiwakilisha nchi yake kwa utawala Haramu wa Israel.
Balozi huyo mpya alikabidhi barua kwa rais wa Israel bwana Shimon Peres. Ndani ya barua hiyo pamoja na Mursi kumtambulisha Atef Mohammad Salem kuwa ni balozi wake lakini imesema bayana kuwa Shimon Perez in Rafiki mkubwa wa Mursi na kuwa Perez ni mtu mzuri sana.
Maneno haya ya Mursi ni kinyume cha ukweli kwani Wapalestina wamekuwa wakipigwa na kuuawa kila siku na serikali hiyo haramu. Ardhi ya Palestina imekuwa ikiporwa kila siku kwa mabavu na wababe hao tena kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa.
Kama kuna adui wa Uislamu na Waislamu basi atakuwa ni Israel ambaye anaongoza kwa kuandaa njama na hujuma dhidi ya waislamu. Hii inamaana kuwa Muslim Brother hood wamepoteza uelekeo na hivyo wamisri wanatakiwa kujikomboa kwa mara nyingine.
Isome barua ya Mursi kwa lugha mkono wake mwenyewe kupitia link ifuatayo;
http://www.abna.ir/data.asp?lang=3&id=357775


No comments:

Post a Comment