Sunday, 20 January 2013

How should I deal with having a friend who I care about but who has bad behavior?


Use your love towards him as a means of advising him and saving him by taking him towards guidance! It has been narrated in a Prophetic tradition that guiding one person is better than the worldly life and all it contains.

Do not forget that love is good when it reaps goodness and it is a means of deviation when it transfers bad morals from your friend to you! A rational person is one who thinks of the outcome of things and then considers the actual situation – what is important and what is more important.

Try to be more reasonable than sentimental because if emotion overpowers you in the important situations, it will destroy you and then convey you to Hell! Of course, this is not what you want nor can bear.

How do I ask forgiveness for my sins?


Question: I am a young man. I have been involved in a great sin. Feeling sin on the one hand and my weak determination before my lust on the other hand have made me desperate of the forgiveness of Allah, and I feel that I will definitely be in Hell. At the same time, I fear that I am not right in this opinion. Would you please guide me to the right solution?

The answer: Confess your sin before Allah and pray to Him to help you with a real repentance! You do not need to ask for forgiveness with a difficult language or eloquent words. Speak easily and spontaneously and say what is inside your heart in any way you can, for Allah knows what is in one’s heart even before it comes to his tongue.
Know well that despairing of the forgiveness of Allah is a sin even greater than the sin you were originally involved in, because despair opens the door wider before you to commit all sins and it is this that will get you into Hell and not your first sin! Therefore, Islam has considered despairing of Allah’s mercy as the greatest of sins. It is this that Satan, the first enemy of man, wants for you on the Day of Resurrection.

O young man, fill your heart with a big hope of getting the forgiveness of Allah and try determinedly not to commit the sin again! When you commit a sin, you should hasten immediately to Allah and ask Him to forgive you. You should never cut your relation with Allah in any case. If you go east or west, you shall not find a god like your Lord, Whom you disobey but He, although able to punish you at once, grants you a respite and says that He loves those who ask Him for forgiveness, loves the repentant, and loves those who purify themselves. Besides, He loves to reward you with His Paradise if you turn to Him sincerely.

O young man, whatever you may have done to disobey Allah, you are still not a polytheist. Allah has made incumbent on Himself to forgive everything other than polytheism. Let the Satan not delay you in seeking forgiveness and make you lose the opportunity, for you do not know when you shall die. You may die at the moment of your procrastination and then you will have wasted the opportunity and lost the eternal happiness.

When you decide to return to Allah, do not forget that the crux of repentance is feeling regretful for what you have committed, determining to give up that sin forever, giving the dues of people back to them, and offering the missed obligations as much as possible! Abide by this sincerely and you will find that the pleasure of lawful things is sweeter than the pleasure of unlawful things.

Saturday, 19 January 2013

Hukumu ya mtu anayegoma kutoa zaka


Sahaba wa Mtume aliyejulikana kwa jina la Tha'alaba ni Tha'laba bin Hatib Ansari ambaye baadhi ya wanahistoria wanasema kuwa aliaga dunia katika kipindi cha ukhalifa wa Omar alihali wengine wanasema aliuawa katika zana za ukhalifa wa Othman.
Wafasiri wa Qur'ani Tukufu wanasema kwamba aya za 75 na 76 za Sura at- Tauba ziliteremshwa kuhusiana naye. Inasemekana kuwa siku moja Mtume Mtukufu SAW alikuwa ameketi msikitini na wafuasi wake alipoingia Tha'laba bin Hatib na kujiunga nao. Alimwomba Mtume ombi moja kwa kusema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Niombee dua ili Mwenyezi Mungu anipe mali nyingi."
Mtume alimtazama na kunyamaza. Tha'alaba alidhani kwamba angejibiwa kama angeendelea kusisitiza na kukariri ombi lake kwa Mtume. Kwa hivyo alirudia tena ombi lake hilo na mara hii akionyesha unyenyekevu wa kiwango fulani. Alisema: "Ewe Mtume! Sijui ni kwa nini nina hamu ya kuwa tajiri. Kila mara ninapofanya juhudi za kuufikia utajiri huo siupati!" Hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa Mtume kusikia ombi hilo kutoka kwa sahaba wake huyo bali alikuwa amelisikia mara kadhaa na kukaa kimya. Ama mara hii alimwambia: "Mali chache ambayo unaweza kuitumia vyema ni bora kuliko mali nyingi ambayo huwezi kuitumia vyema." Tha'laba alitaka kuzungumza lakini Mtume baada ya kunyamaza kidogo aliendelea kusema: "Ewe Tha'laba! Si ni vyema uyatazame maisha ya Mtume wako na kukinai?"
Baada ya kimya kifupi Mtume alisema: "Watu wengi huwa hawatekelezimajukumu ya Mwenyezi Mungu mara wanapopata mali nyingi." Baada ya kuyasikia maneno hayo ya Mtume Tha'laba alisema: "Naapa kwa jila la Mwenyezi Mungu ambaye alikuteuwa wewe kuwa Mtume kwamba, kama nitajaaliwa kuwa na utajiri mkubwa nitatekeleza majukumu na faradhi zote ninazotakiwa kutekeleza na Mwenyezi Mungu." Mtume ambaye aliona Tha'laba anaendelea kusisitiza juu ya msimamo wake na kutaka aombewe dua ya utajiri alimwombea hivi: "Ewe Mwenyezi Mungu! Mtekelezee Tha'alaba kile anachokiomba!" Haukupita muda mrefu kabla ya dua ya Mtume kujibiwa na Mwenyezi Mungu. Mtoto wa ami yake Tha'laba ambaye alikuwa mzee na tajiri mkubwa aliugua kwa muda na kisha kuaga dunia ambapo Tha'laba alirithi mali yake yote. Tha'laba alitumia utajiri huo kununua kondoo wengi na kujishughulisha na ufugaji mifugo. Baada ya muda, alifanikiwa sana katika shughuli hiyo ambapo idadi ya mifugo wake iliongezeka kwa haraka kwa kadiri kwamba hakupata tena malisho ya kutosha mjini Madina. Kwa hivyo aliamua kuhama Madina na kwenda kuishi katika kijiji kimoja kilichokuwa nje kidogo ya mji huo ili apate fursa ya kulisha mifugo wake kwa urahisi. Kijiji hicho kilimtosheleza vyema Tha'laba kwa ajili ya malisho ya mifugo wake wengi. Licha ya kuridhishwa na wingi wa mifugo hiyo na mafanilkio makubwa aliyoyapata katika uwanja huo lakini shughuli hiyo ilimzuia kushiriki katika swala za jamaa na kuamua kushiriki swala za Ijumaa tu jambo ambalo pia taratibu alizembea kulidumisha na mwishowe kutoshiriki kabisa katika swala hizo.
Baada ya kuteremka aya ya 103 ya Sura at-Tauba ambayo iliwawajibisha Waislamu kutoa zaka, Waislamu wote waliokuwa mjini Madina na ambao walikuwa na uwezo wa kutoa kodi hiyo ya Kiislamu walilazimishwa kuilipa. Baada ya hapo zamu iliwafikia wale waliokuwa wakiishi nje ya mji, hivyo Mtume akawatuma watu wawili ili wachukue zaka kutoka kwa Tha'laba. Idadi ya mifugo ya Tha'laba ilikuwa kubwa kiasi kwamba ilimwezesha kutoa zaka bila matatizo yoyote, lakini alikataa kufanya hivyo mara tu wajumbe wa Mtume walipomjia na kumuomba atoe zaka. Alisema: "Aah, mashaka ya maisha! Mwambieni Mtume kwamba maisha ya Tha'laba ni mabaya sana na kwa hivyo hawezi kutoa zaka ya mifugo wake!"
Wakusanyaji zaka ambao walikuwa wakijua vyema utajiri wa Tha'laba, na wakifahamu kwamba mamia ya kondoo waliowaona njiani walikuwa ni wake walishangaa na msimamo huo na kumuuliza: "Tha'laba unawezaje kutamka maneno hayo ilihali unafahamu vyema kwamba wewe ni mmoja wa wamiliki wakubwa wa kondoo pambizoni mwa mji wa Madina?!" Huku akiwa na uso uliojaa huzuni alisema: "Mliona kondoo njiani na kudhani kwamba ni wa Tha'laba. Hata kama itakuwa ni hivyo, lakini jueni kwamba kandoo wanene na walio salama wanatokana na malisho mazuri na uchungaji mkubwa, jambo ambalo humletea mtu matatizo na machungu mengi. Ni vipi Tha'laba anaweza kuvumilia machungu haya yote?!"
Mmoja wa wakusanyaji zaka alisema: "Tha'laba! Sisi tumetumwa hapa na Mtume wa Mwenyezi Mungu ili tuchukue haki unazopaswa kutoa kwa ajili ya wanaozistahiki. Elewa kwamba kutoa haki za kisheria kutakuwa na baraka za kuongezeka mifugo wako humu duniani na kupata thawabu za Mwenyezi Mungu huko Akhera."
Tha'laba alicheka kwa kejeli na kusema: "Nina swali: Ninataka kujua iwapo kuna tofauti kati ya zaka na jizia." Afisa yule wa ukusanyaji zaka ambaye hakuwa amefahamu vyema kusudio la swali la Tha'laba alimuuliza: "Yaani wewe haufahamu tofauti ya mambo haya mawili?" Tha'laba akajibu: "Watu wasiokuwa Waislamu wanaoishi chini ya himaya na ulinzi wa Waislamu huwa wanatozwa kodi inayoitwa jizia, ni kweli au si kweli? Zaka pia ni aina ya jizia ambayo sisi Waislamu tunapasa kuitoa. Sasa niambieni, je, Waislamu na wasiokuwa Waislamu wanapasa kutoa jizia au la?
Afisa mwingine wa ukusanyaji zaka akamjibu Tha'laba kwa kusema, "Zaka ni haki ya wanyonge na wahitaji wa Kiislamu ambayo Mwenyezi Mungu amewatengea kutoka kwa matajiri na inatofautiana na jizia." Tha'laba aliinamisha chini kichwa chake ikiwa ni alama ya kupinga maneno ya afisa huyo na kusema: "Hakuna tofauti yoyote kati ya zaka na jizia; hii ni fikra na imani yangu ambayo nimewaza sana juu yake." Maafisa hao wa ukusanyaji zaka ambao walishuhudia ujanja, ukorofi na inadi kutoka kwa Tha'laba waliinamisha chini vichwa vyao huku wakiwa wamekata tamaa. Ilifahamika wazi kwamba kwa kutoa dalili hizo batili na zisizo na msingi Tha'laba alitaka kukwepa kutoa zaka. Mmoja wa maafisa hao alitaka kutoa hoja ya mwisho kwa kusema: "Tutakaporejea Madina tumwambie nini Mtume wa Mwenyezi Mungu...?' Hata kabla hajamaliza kuuliza swali hilo, Tha'laba alimkatiza kwa makelele na kumwambia: "Hakuna! Tusijisumbue. Mwambieni Mtume kwamba Tha'laba ima hataki au hana uwezo wa kutoa zaka..." Baada ya hapo aliwapa mgongo wajumbe wawili hao wa Mtume na kwenda zake bila kusema neno jingine lolote.
Wakusanyi kodi hao walirejea mjini Madina na kumueleza Mtume SAW mambo yalivyokwenda walipokutana na Tha'laba. Mtume alisikitika sana aliposikia maneno aliyonukuliwa kutoka kwa Tha'laba na kusema: "Ole wake Tha'laba! Ole wake Tha'laba!
Muda si mrefu Malaika Jibril alimteremshia Mtume aya za 75 na 76 za Suratu Tauba zinazosema: Na miongoni mwao (hao wanafiki) wako waliomuahidi Mwenyezi Mungu kuwa: "Akitupa katika fadhila zake tutatoa sadaka na tutakuwa miongoni mwa wanaotenda mema." Lakini alipowapa hizo fadhila zake, walizifanyia ubakhili na wakakengeuka, nao (mpaka hivi sasa) wanakengeuka.
Inasemekana kuwa baada ya Tha'laba kusikia kwamba aya hizo ziliteremka kwa ajili yake alimwendea Mtume kwa madhumuni ya kutaka kutoa zaka lakini Mtume SAW aliikataa na kusema kuwa Mwenyezi Mungu alikuwa amemkaza kupokea zaka kutoka kwake. Baada ya kuaga dunia Mtume Tha'laba aliwapelekea makhalifa waliotawala baada yake sadaka hiyo lakini nao pia waliikataa kwa kumfuata Mtume SAW.
Kama mtume hakumuadhibu Tha'alaba pamoja na kwamba aligoma kutoa zaka, je Sayyidna Abubakari aliyeagiza watu waliogoma kulipa zaka wauawe aliipata wapi hiyo sheria?

Kikao cha Waumini wa Shia - Islam Mkoa wa Morogoro

Assalaam alaykum: ninachukua fursa hii kuwakaribisha kwenye kikao viongozi wote wa Shia mkoa wa Morogoro. Kikao kitafanyika saa 8 kamili mchana mpaka saa 11 jioni hapa manispaa ya Morogoro. kufika kwenu ndio mafanikio ya kikao.
wabillah tawfiiq
wasalaam alaykum

CLINTON; Marekani ni mfadhili wa Ugaidi duniani

Marekani inajidai kupambana na magaidi ambao iliwaandaa na kuwafadhili yenyewe ili kuyumbisha amani katika nchi zingine. sikiliza hotuba ya Hillary Clinton utauona ukweli huo.

Hotuba ya Mhe. Nassari huko Kigoma


Imamu Mahdi by sheikh Abdillah Nassir hotuba


Mufti wa Tanzania wa Waislamu wa madhehebu ya Shia

Mufti wa Tanzania na Sheikh mkuu wa Shia Islam sheikh Abdallah Seif akisalimiana na vijana wa kiislamu baada ya kuongoza maandamano ya maombolezo ya kifo cha Mtume Mohammad (S.A.W.W), Tarehe 28 Safari 1434 hijiria huko Dar es Salaam.

Iran itaendelea kuwaunga mkono wananchi wa Syria


Iran itaendelea kuwaunga mkono wananchi wa Syria

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, uungaji mkono wa Iran kwa Rais Bashar Assad hauna maana ya kupuuzwa haki ya wananchi wa Syria katika kuainisha mustakbali wao. Akizungumza na Televisheni ya al Mayadin Dakta Ali Akbar Velayati ameongeza kuwa, sababu kuu ya kujikita Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Syria, ni kuzuia kusambaratika  harakati ya muqawama mkabala wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Veleyati ameongeza kuwa, Rais Bashar Assad ni mstari mwekundu kwa Iran, na serikali ya Tehran itaendelea kumuunga mkono hadi mwisho na kusisitiza kuwa jambo hilo  halina maana ya kupuuzwa haki za wananchi wa Syria za kuainisha mustakbali wa nchi yao. Akizungumzia hitilafu zilizoko kati ya Iran na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas kuhusiana na mgogoro wa Syria, Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, kuna uwezekano kwa pande mbili zikawa zinahitilafiana katika baadhi ya mambo na hilo ni jambo la kawaida, lakini sababu kuu ya uungaji mkono wa Iran kwa Hamas na Jihadul Islami ni katika muktadha wa kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel. source: www.irib.ir 

Kuhani Mzayuni mwenye misimamo mikali asilimu


Kuhani Mzayuni mwenye misimamo mikali asilimu

Kuhani mmoja ambaye zamani alikuwa ni miongoni mwa wahubiri wenye misimamo mikali ya Kizayuni ameamua kusilimu yeye pamoja na familia yake yote. Kuhani Yosef Kuhin alikuwa ni mmoja kati ya wahubiri wenye misimamo mikali ya Kizayuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na mwanachama wa chama chenye misimamo ya kufurutu ada cha Shas. Kuhin amesilimu kutokana na mawaidha aliyoyoyapata kutoka kwa mwanachuoni mmoja wa Kuwait yapata miaka miwili iliyopita, na baada ya kukinaishwa na dalili zilizotolewa na mwanachuoni huyo aliamua kusilimu pamoja na familia yake. Josph Kohen amesilimu na kuitwa jina la Yussuf Muhammad, ameanza kukabiliwa na matatizo na vikwazo kadhaa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Kuhani huyo wa zamani wa Kiyahudi hivi sasa anakabiliwa na matusi, vitendo vya kumvunjia heshima na hata kumfanyia kejeli, na baadhi ya wanachama wa chama cha Shas wametaka achunguzwe akili yake kama iko salama kutokana na hatua yake ya kuingia katika dini tukufu ya Kiislamu. Hivi karibuni gazeti la Yadioth Aharonot la Israel liliandika kuwa, kwa mwaka Mayahudi 20 husilimu kutokana na mahubiri na mafundisho ya kidini wanayoyasikiliza kupitia kwenye satalaiti, internet na hali kadhalika kuingia wahubiri wa Kiislamu katika jamii ya Israel.

Jeshi la Mali laudhibiti tena mji wa Konna


Jeshi la Mali laudhibiti tena mji wa Konna
Jeshi la Mali limesema kwamba limeudhibiti tena mji wa Konna baada ya waasi kukimbia, kufuatia mapigano makali kati ya pande mbili. Hayo yanajiri huku askari wa kwanza 100 wa Kiafrika kutoka nchi za Togo na Nigeria wakiwasili katika mji mkuu wa Mali, Bamako. Askari hao ni sehemu ya kikosi cha nchi za Afrika Magharibi kitakachoungana na askari wa Ufaransa na Mali katika kupambana na waasi wa kaskazini mwa nchi hiyo. Katika upande mwingine Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limetangaza kuwa, lina wasiwasi mapigano nchini Mali yatapelekea zaidi ya watu laki 7 kuwa wakimbizi. Shirika hilo limesema tayari wakimbizi laki na nusu wameelekea katika nchi jirani na Mali huku maelfu ya wengine wakiwa wakimbizi ndani ya nchi yao.

Khatami: Marekani, mfadhili mkuu wa magaidi



Khatami: Marekani, mfadhili mkuu wa magaidi
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amelaani mauaji ya kigaidi ya Waislamu wa Pakistan, Iraq na Syria na kusema kwamba magaidi wanafanya jinai na kutekeleza malengo ya Marekani katika eneo kutokana na msaada wa fedha na kijeshi wa Washington. Ayatullah Ahmad Khatami ameongeza kuwa, baadhi ya nchi za Kiarabu pia zinashiriki katika kufanikisha malengo ya Marekani katika eneo na kutenda jinai na mauaji katika nchi za Syria, Iraq na Pakistan. Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran aidha amesema, muqawama na kusimama kidete mataifa ya eneo hili dhidi ya njama za Marekani ndiko kutakakoleta ushindi na kwamba maadui wataangamizwa hivi karibuni.
Aidha amebainisha kuwa, mabeberu wa dunia na utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel wanapinga dini tukufu ya Uislamu na kutiwa wasiwasi na kuenea mwamko wa Kiislamu katika eneo, hivyo Waislamu wanapaswa kuwa macho na kuimarisha umoja.  Hii ni kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Iran www.irib.ir. 

watuhumiwa wa miripuko ya Nigeria watiwa mbaroni

watuhumiwa wa miripuko ya Nigeria watiwa mbaroni
Jeshi la Polisi nchini  Nigeria limewatia mbaroni washukiwa wa miripuko ya mabomu  ya mwezi Novemba mwaka jana kwenye Kanisa moja huko kaskazini mwa  nchi hiyo. Taarifa zinasema kuwa, Polisi ya Nigeria imewatia mbaroni Ibrahim Muhammad na Muhammad Ibrahim Idriss kwa tuhuma za kuchoma moto Kanisa moja kaskazini mwa nchi hiyo. Watuhumiwa hao wamekiri kutekeleza shambulio hilo lililopelekea  watu wasiopungua 11 kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa. Mashambulio yanayofanywa na wafuasi wa kundi la Boko Haram yalianza mwaka 2009 katika sehemu ya kaskazini mwa Nigeria na hadi  sasa maelfu ya watu wamepoteza maisha yao kutokana na mashambulio hayo. Aidha kundi hilo limekuwa likitekeleza mashambulio dhidi ya mashule, hospitali na idara nyingine za serikali za Nigeria.