Saturday 19 January 2013

watuhumiwa wa miripuko ya Nigeria watiwa mbaroni

watuhumiwa wa miripuko ya Nigeria watiwa mbaroni
Jeshi la Polisi nchini  Nigeria limewatia mbaroni washukiwa wa miripuko ya mabomu  ya mwezi Novemba mwaka jana kwenye Kanisa moja huko kaskazini mwa  nchi hiyo. Taarifa zinasema kuwa, Polisi ya Nigeria imewatia mbaroni Ibrahim Muhammad na Muhammad Ibrahim Idriss kwa tuhuma za kuchoma moto Kanisa moja kaskazini mwa nchi hiyo. Watuhumiwa hao wamekiri kutekeleza shambulio hilo lililopelekea  watu wasiopungua 11 kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa. Mashambulio yanayofanywa na wafuasi wa kundi la Boko Haram yalianza mwaka 2009 katika sehemu ya kaskazini mwa Nigeria na hadi  sasa maelfu ya watu wamepoteza maisha yao kutokana na mashambulio hayo. Aidha kundi hilo limekuwa likitekeleza mashambulio dhidi ya mashule, hospitali na idara nyingine za serikali za Nigeria.

No comments:

Post a Comment