Saturday 19 January 2013

Kuhani Mzayuni mwenye misimamo mikali asilimu


Kuhani Mzayuni mwenye misimamo mikali asilimu

Kuhani mmoja ambaye zamani alikuwa ni miongoni mwa wahubiri wenye misimamo mikali ya Kizayuni ameamua kusilimu yeye pamoja na familia yake yote. Kuhani Yosef Kuhin alikuwa ni mmoja kati ya wahubiri wenye misimamo mikali ya Kizayuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na mwanachama wa chama chenye misimamo ya kufurutu ada cha Shas. Kuhin amesilimu kutokana na mawaidha aliyoyoyapata kutoka kwa mwanachuoni mmoja wa Kuwait yapata miaka miwili iliyopita, na baada ya kukinaishwa na dalili zilizotolewa na mwanachuoni huyo aliamua kusilimu pamoja na familia yake. Josph Kohen amesilimu na kuitwa jina la Yussuf Muhammad, ameanza kukabiliwa na matatizo na vikwazo kadhaa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Kuhani huyo wa zamani wa Kiyahudi hivi sasa anakabiliwa na matusi, vitendo vya kumvunjia heshima na hata kumfanyia kejeli, na baadhi ya wanachama wa chama cha Shas wametaka achunguzwe akili yake kama iko salama kutokana na hatua yake ya kuingia katika dini tukufu ya Kiislamu. Hivi karibuni gazeti la Yadioth Aharonot la Israel liliandika kuwa, kwa mwaka Mayahudi 20 husilimu kutokana na mahubiri na mafundisho ya kidini wanayoyasikiliza kupitia kwenye satalaiti, internet na hali kadhalika kuingia wahubiri wa Kiislamu katika jamii ya Israel.

No comments:

Post a Comment