Saturday 19 January 2013

Jeshi la Mali laudhibiti tena mji wa Konna


Jeshi la Mali laudhibiti tena mji wa Konna
Jeshi la Mali limesema kwamba limeudhibiti tena mji wa Konna baada ya waasi kukimbia, kufuatia mapigano makali kati ya pande mbili. Hayo yanajiri huku askari wa kwanza 100 wa Kiafrika kutoka nchi za Togo na Nigeria wakiwasili katika mji mkuu wa Mali, Bamako. Askari hao ni sehemu ya kikosi cha nchi za Afrika Magharibi kitakachoungana na askari wa Ufaransa na Mali katika kupambana na waasi wa kaskazini mwa nchi hiyo. Katika upande mwingine Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limetangaza kuwa, lina wasiwasi mapigano nchini Mali yatapelekea zaidi ya watu laki 7 kuwa wakimbizi. Shirika hilo limesema tayari wakimbizi laki na nusu wameelekea katika nchi jirani na Mali huku maelfu ya wengine wakiwa wakimbizi ndani ya nchi yao.

No comments:

Post a Comment