Saturday, 19 January 2013

Iran itaendelea kuwaunga mkono wananchi wa Syria


Iran itaendelea kuwaunga mkono wananchi wa Syria

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, uungaji mkono wa Iran kwa Rais Bashar Assad hauna maana ya kupuuzwa haki ya wananchi wa Syria katika kuainisha mustakbali wao. Akizungumza na Televisheni ya al Mayadin Dakta Ali Akbar Velayati ameongeza kuwa, sababu kuu ya kujikita Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Syria, ni kuzuia kusambaratika  harakati ya muqawama mkabala wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Veleyati ameongeza kuwa, Rais Bashar Assad ni mstari mwekundu kwa Iran, na serikali ya Tehran itaendelea kumuunga mkono hadi mwisho na kusisitiza kuwa jambo hilo  halina maana ya kupuuzwa haki za wananchi wa Syria za kuainisha mustakbali wa nchi yao. Akizungumzia hitilafu zilizoko kati ya Iran na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas kuhusiana na mgogoro wa Syria, Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, kuna uwezekano kwa pande mbili zikawa zinahitilafiana katika baadhi ya mambo na hilo ni jambo la kawaida, lakini sababu kuu ya uungaji mkono wa Iran kwa Hamas na Jihadul Islami ni katika muktadha wa kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel. source: www.irib.ir 

No comments:

Post a Comment