Friday, 16 August 2013

HADITH YA MTUME KUHUSU MGAWANYIKO WA WAISLAM



Mtume wa Allah alisema, “Wana wa Israel walifarakana na kuwa makundi 71, Manaswara nao wamefarakana na kuwa makundi 72, na umati wangu utafarakana na kufikia makundi 73 na yote yataingia motoni, isipokuwa kundi moja tu.” Ebu niambieni kundi hilo enyi watu wenye akili.
Mimi nashangaa kuona waislamu wote na makundi yao wanaifahamu hadith hii lakini hawaifanyii kazi kwa kufanya utafiti na kubaini ni kundi gani lenye kuokoka na kuachana na makundi mengine yenye kupotoka.
 Cha ajabu ni kuwa kila kundi linadai kuwa ndilo lenye kuokoka bila kuleta ushahidi uliosahihi.
Tafadhali tufanye utafiti ili tubaini kundi hili lenye kuokoka ili tujiunge nalo, vinginevyo tutaangamia. Mwenyezi Mungu anasema, “Na wale wanaojitahidi kwa ajili yetu, tutawaongoza kwenye njia zetu” Qur’an 29:69.
Na amesema tena, “Wale ambao husikiliza kauli (zisemwazo) wakafuata zile zilizo njema, hao ndio aliowaongoa Mwenyezi Mungu na hao ndio wenye akili”.
Bila shaka amesema kweli Mjumbe wa Mwenyezi Mungu pale aliposema kuwa fanya utafiti kuhusu dini yako mpaka isemwe kuwa wewe ni maj-nun.

DUA ILI ALLAH ATUONGOZE TUJUE NA KUFUATA KUNDI SAHIHI



Ewe Mwenyezi Mungu wanadamu tumekhitilafiana na kuwa Wayahudi, Wakristo na Waislamu, ama wayahudi wamekhitilafiana na kuwa makundi 71, Wakristo wamekhitilafiana na kuwa makundi 72, waislamu nao wamekhitilafiana na kuwa makundi 73 na yote yamo katika upotofu isipokuwa kundi moja tu, Kama alivyosema Mtume wako Mohammad (S.A.W.W). Je huu ndio utaratibu uliouweka kama wanavyosema baadhi ya waislamu kuwa Wewe ndiwe uliyeiandikia kila nafsi ikiwa bado tumboni mwa mama yake; iwe Yahudi, Mkristo, Muislamu, mwizi, mshirikina, mlafi, mcha Mungu, muuaji, mchawi n.k. na hatimaye mtu akawa hivyo alivyo?
Kwa hakika nafsi yangu haikubali fikra hizi ya kwamba Qadhaa na Qadar ndiyo iliyoamua hatima ya mtu kimatendo yake, bali karibu nikate shauri kwamba wewe Mwenyezi Mungu ndiwe uliyetuumba, ukatuongoza na ukatufahamisha mabaya na mema, ukatuagiza tufanye mema na kuacha mabaya, na ukawatuma Mitume wako ili watubainishie yanayotutatiza na watujulishe haki kutokana na batili lakini mtu mwenyewe ndiye aliyezugwa na maisha ya dunia na mapambo yake akasahau maelekezo yako.
Kwa ubinafsi na ujeuri wake, kwa ujinga wake na kujitosa kwake katika mambo yasiyo na faida, na kwa inadi yake na uhasama wake, na kwa dhulma yake na kuvuka kwake mipaka, ameiacha haki na kumfuata shetani na akajitenga na wewe Muumba wake. Bila shaka Qur’an tukufu imekwisha lieleza hilo, “Kwa hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu kitu chochote lakini watu wanajidhulumu wenyewe (10:44).
Na Mtume wako alitutahadharisha sana pale aliposema, “sio halali kwa muislamu kumnunia ndugu yake muislamu zaidi ya siku tatu,” lakini bado tumegawanyika na kuwa vidola vidogo vidogo vinavyofanyiana uadui vyenyewe kwa vyenyewe na kupigana wao kwa wao.
Umma huu unanini ewe Mwenyezi Mungu, baada ya kuwa ulikuwa umma bora kuliko umati zote na ulipata nguvu duniani na kuwafikishia watu uongofu, elimu, maarifa na maendeleo, ghafla leo hii umekuwa ni umma mdogo na dhaifu mno, ardhi yao imeporwa na wananchi wake wametawanyika na msikiti wao mtakatifu umekaliwa na kupokonywa na wazayuni na wala hawawezi kuukomboa. Hivi na hii nayo umetuandalia tuwe hivi? La hasha kwani fikra inapingana na malengo wako matukufu ya kuuinua Uislamu ili uiongoze dunia. Naomba ewe Mola wangu kama fikra zangu ni sahihi niimarishe katika fikra hizi na niweke pamoja na watu wenye fikra kama zangu. Na kama nimepotoka ninakuomba uniongoze njia iliyonyooka kwani wewe ndiye mbora wa waongozaji.

MASAHABA SIKU YA SULHU YA HUDAIBIYA



Katika mwaka wa 6 hijiria, Mtume na masahaba wake (1400) walitoka Madina kwenda Makah kuhiji. Walipofika eneo liitwalo Dhil-halifah walivaa Ihram na pia aliwaagiza waweke panga zao katika ala. Wakawatanguliza ngamia kwa ajili ya kuchinja ili kuwatambulisha Maquraish kuwa wamekwenda kwa ajili ya hija na wala sio vita.
Makuraish kwa kiburi chao walimtumia mjumbe aitwaye Suhail na ujumbe kuwa Mtume arudi alikotoka na kwamba mwaka ujao watamwachia Makkah kwa muda wa siku tatu. Ujumbe huu uliambatana na mkataba wenye masharti magumu lakini Mtume aliyakubali kwa kutegemea maslahi ambayo Mola wake mtukufu alimfunulia.
Hata hivyo baadhi ya Masahaba walimpinga kwa nguvu zao zote na Umar bin Khatab akamwendea Mtume na kumuuliza, “Je, wewe siyo Mtume wa Mwenyezi Mungu wa haki?” Mtume akajibu, “bila shaka mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu wa haki.” Umar akauliza tena, “je sisi hatuko kwenye haki na adui yuko kwenye batili?” Mtume akajibu, “bila shaka ndivyo.” Umar akauliza, “basi ni kwa nini tunaonesha udhaifu katika dini yetu?” Mtume akamwambia, “bila shaka mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na siwezi kumuasi Mola wangu, naye ndiye hunilinda.” Umar akauliza tena, “je, si ulikuwa ukituambia kuwa tutaingia kwenye nyumba tukufu na kuitufu?” Mtume akasema, “bila shaka nilisema, lakini, je nilikuambia tutaingia mwaka huu? Umar akasema, “hapana.” Mtume akasema, “bila shaka utaingia na utaitufu.”
Hatimaye Umar bin Khatabu hakuridhika na majibu ya Mtume hivyo akaenda kumuuliza maswali yale yale Abubakar bin Quhafah.
Basi Mtume alipomaliza kusaini mkataba wa hudaibiyyah aliwaambia Masahaba wake wasimame wachinje na wanyoe. Wallahi hakuna miongoni mwao aliyesimama mpaka akasema mara tatu na ilivyokuwa hapana aliyetekeleza amri yake, aliingia kwenye hema lake kisha akatoka na wala hakumsemesha yeyote kati yao, akachinja mnyama wake na akamuita kinyozi wake akamnyoa.
Masahaba walipoona hali hiyo, walisimama, wakachinja na wakawa wananyoana wao kwa wao, karibu wauane wao kwa wao. Kisa hiki kimeandikwa na waandishi wa Sira na Tarekh, kama ambavyo amekiandika Bukhari ndani ya sahihi yake katika Kitabus-Shurut fil-jihad, juz. 2 uk. 122. Pia Sahih Muslim katika babu Sul-hul-hudaibiyah juz. 2.
Hivi huu ndio utii wa Masahaba kwa Mtume wao? Je Masahaba hawa hawakuisoma Qur’an 4:65 ambapo Mwenyezi Mungu amesema, “Naapa kwa Mola wako, hawawi waumini mpaka wakufanye wewe uwe muamuzi katika yale wanayozozania baina yao. Kisha wasione uzito katika nafsi zao kwa yale uliyoyaamua na wasalimu amri mara moja.”
Je Umar bin Khatab alisalimu amri mara moja mahali hapo na hakuona uzito ndani ya nafsi yake kwa maamuzi aliyoyafanya Mtume? Bila shaka Umar na wenziwe walionesha mashaka makubwa juu ya hukumu aliyoifanya Mtume wao kinyume na maagizo ya Allah (S.W)

MIGAWANYIKO (MAKUNDI) YA MASAHABA



Masahaba wa Mtume Mohammad (S.A.W.W) wamegawanyika katika makundi makuu manne:
1.   Masahaba wema
Masahaba hawa walimtambua Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa maarifa ya kweli kabisa na wakamuunga mkono Mtume Mohammad (S.A.W.W) kwa dhati na kusuhubiana naye kwa ukweli katika kauli na utakaso wa moyo katika matendo, na wala hawakugeuka baada yake, bali waliimarika katika ahadi waliyomuahidi. Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamewasifia Masahaba hawa kwa dhati kabisa. Mfano wa Masahaba wema ni Abudhar bin Ghiffar, Ammar bin Yasin, Salman Farsii, Mohammad bin Abubakar na Bilal bin Rabah.

2.   Masahaba waliosimu kwa woga au kupenda jambo fulani la waislamu.
Masahaba hawa kuna kipindi walimfuata Mtume na wakati mwingine walimpinga na kumuudhi Mtume kwa kuacha kufuata maagizo yake na kufanya makatazo yake. Maoni yao waliyapa nguvu juu ya hukumu tukufu za Qur’an na Qur’an iliwakemea mara nyingi watu hawa. Mfano wa Masahaba hawa ni Abusufian baba wa Muawiyyah na familia yake.

3.   Masahaba waliokuwa wanafiki
Masahaba hawa walimfuata Mtume Mohammad (S.A.W.W) kwa lengo la kumfanyia vitimbi, wakadhihirisha Uislamu, wakaficha ukafiri, wakajisogeza ili wauvuruge Uislamu na Waislamu. Bila shaka Mwenyezi Mungu ametelemsha sura nzima kuwalaani aina hii ya Masahaba, akawaonya kuwa wataingia katika tabaka la chini la moto wa Jahannam.
Mtume aliwataja baadhi yao na Sunni na Shia tunaafikiana kuwa kuna Masahaba walikuwa wanafiki na walijulikana. Mfano ni Abdallah bin Salun
4.   Masahaba maalumu (Ahlulbayt wa Mtume)
Majina ya Ahlulbayt ni Mtume Mohammad mwenyewe, Ally ibn Abitalib, Fatumah bint Mohammad, Hassan bin Ally na Hussein bin Ally (a.s)
Watu hawa wametakaswa na Allah na kuondolewa uchafu (Qur’an 33:33). Allah amewajibisha kuwasalia sambamba na Mtume (Qur’an 8:41). Allah amewajibisha kwa kila Muislamu kuwapenda watu hawa na ndio malipo ya utume wa Mtume Mohammad (S.A.W.W). (Qur’an 42:23). Wao ndio wenye mamlaka ambao Mwenyezi Mungu ameamrisha kuwatii (Qur’an 4:59). Wamebobea katika elimu (4:59). Wao ni wenye kumbukumbu ambao Mtume ametuagiza kushikamana nao, tena akawafananisha na safina ya Nuhu ambayo mwenye kuipanda ataokoka na mwenye kuikengeuka ataangamia.
Soma; As-sawaiqul Muhriqah ya Ibn Hajar uk. 184 na 234
           Musnad Ahmad Juz. 5 uk. 182
           Kanzul Umaal juz. 1 uk. 44

'US, Israel, Saudi Arabia: World-leper Axis of Evil'


A political commentator says the United States, the Israeli regime and Saudi Arabia constitute the real Axis of Evil in the Middle East but one that is increasingly becoming a ‘pariah,’ Press TV reports.


In an article published on Press TV website on Friday, Rodney Shakespeare described Washington, Tel Aviv and Riyadh as the “Evil Incarnate,” which is behind the upheavals plaguing the region.

Referring to the grisly crimes of the foreign-baked militants in Syria, Shakespeare said, “These three - USA, Israel and Saudi Arabia - who are Evil Incarnate, are behind the heart-eaters, the throat-slitters, the gas chokers and head-choppers of the Jabhat al Nusra, Wahhabis, Salafists and Takfiris in Syria.”

“They are behind the Egyptian military which, in one day, has slaughtered well over six hundred people … They are behind the destruction and creeping genocide of Palestine and they are behind yesterday’s bombing in Beirut,” he added.

Shakespeare was pointing to Thursday’s bomb blast in Beirut, which killed at least 21 people and injured over 200; and the Egyptian army’s violent clampdown on supporters of ousted President Mohamed Morsi a day earlier, which according to officials, claimed 638 lives and injured 4,200.

Shakespeare said the agenda of the trio goes beyond torturing, assassinations, bombings, and “smashing of countries.”

“It’s worse than that,” he said, “They are trying to ignite world-wide war.”

Shakespeare’s comments came after the Israeli Minister for Military Affairs Moshe Ya’alon in a meeting with Chairman of the US Joint Chiefs of Staff General Martin Dempsey on August 14 branded Iran, Syria and Lebanon as the new “Axis of Evil” in the region.

The term was first used by former US President George W. Bush in January 2002 to refer to Iran, North Korea and the former Iraqi regime of Saddam Hussein.

Shakespeare further pointed to the comments by US General Wesley Clark, former supreme commander of NATO forces in Europe, who revealed just days after the 9/11, “We’re going to take out seven countries in five years, starting with Iraq, and then Syria, Lebanon, Libya, Somalia, Sudan and, finishing off, Iran.”

“9/11 was done by the USA, Israel and Saudi Arabia. Iraq was done, and is being done, by the USA, Israel and Saudi Arabia. And Libya and Somalia and Sudan have been, or are being done, as is Lebanon. Furthermore, when the opportunity arises, another country gets done by the Axis and that’s what’s happening with Egypt.” wrote Shakespeare.

Shakespeare went on to say, “They are not just the Axis of Evil. They are becoming something else as well - pariahs, as they’ll find out one day when even their best friends will buck up the courage to tell them.”

He also said the recent remarks by former US Ambassador to Baghdad Christopher Hill that Saudi Arabia is sponsoring violence in Iraq only partially reflects the reality and was meant as a diversionary tactic.

“Yes, Saudi Arabia was fomenting violence but he said that to hide the fact that the USA and Israel were also fomenting the violence in Iraq,” Shakespeare said, adding, “And it’s the same with Egypt.”

MSIBA WA IMAM HUSSEIN (a.s).



Imam Hussein alipouliwa na vikosi vya jeshi vilivyosheheni wanafiki waliotumwa na Yazid bin Muawiyyah, alikatwa kichwa, kikachomekwa juu ya mkuki na kutembezwa mbele ya msafala wa jeshi la Yazid na mateka wao yaani wajukuu na vitukuu wa kike wa Mtume Mohammad (S.A..W.W) miongoni mwao akiwamo Zainabu bint Ally and Sukaina bint Hussein. Mateka hawa wa kike walikuwa wamevuliwa hijabu, kusimangwa na kuzomewa kila walikopita mpaka walipofika makao makuu ya utawala wa Bani Umayyah yaliyokuwa katika msikiti ya Umayyah ulioko Damascus Syria.
Walipofika huko mateka walipewa wasaa wa kujitetea ili wasiuliwe kama walivyouwawa ndugu zao wa kiume. Bi Zainabu alisimama na kuulaumu utawala wa Yazid kutokana na dhulma yake juu ya Uislamu na Waislamu. Akamwambia, “hata mfanye juhudi za kiasi gani kuufifiza utajo wa Ahlulbayt hamtoweza kwani sisi tumeinuliwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake.”
Alisema kweli Bi Zainab kwani leo utajo wa Ahlulbayt unazidi kuongezeka na watu wanaotumia majina yao ni wengi kiasi kwamba karibia kila nyumba utakuta jina la Ahlulbayt limetumika. Kinyume chake unaweza kuzunguka mji mzima na ukakosa mtu anayeitwa Yazid, Muawiyyah, Hindu au Abusufian. Hawa watu wane walikuwa ni msingi wa madhila yaliyowakuta Ahlulbayt Rasulullah na waislamu kwa ujumla.
Kiwiliwili cha Imam Hussein (a.s) kilizikwa na Mashia wake hapo hapo Karbala na kichwa chake kikazikwa na maadui zake katika msikiti wa Banu Umayyah huko Damascus Syria.