Friday, 30 May 2014

ARABIA KABLA YA UISLAMU 4 --------- HALI YA USTAWI WA JAMII

Arabia ilikuwa ni jamii iliyoshikiliwa na wanaume. Wanawake hawakuwa na hadhi ya aina yoyote zaidi ya kuwa bidhaa za ngono. Idadi ya wanawake mtu anayoweza kuoa haikukadiriwa. Mwanaume alipokufa, mwanae 'alirithi' wake zake wote isipokuwa mama yake mzazi tu. Tabia ya kikatili ya Waarabu ilikuwa ni kuwazika watoto wao wa kike wachanga wakiwa hai. Hata kama Mwarabu hakutaka kumzika binti yake akiwa hai, alikuwa bado lazima adumishe mila hii ya 'heshima' kwa vile hana uwezo wa kuhimili shinikizo la jamii.
Ulevi ullikuwa ni mazoea mabaya ya kawaida ya Waarabu. Ulevi wao ulifuatana na uchezaji kamari. Walikuwa walevi waliokithri na wacheza kamari waliokubuhu. Mahusiano ya jinsia zao yalikuwa yamelegea sana. Wanawake wengi waliuza mapenzi kupata maisha yao kwa vile kulikuwa na kidogo sana kingine ambacho wangeweza kufanya. Wanawake hawa walipeperusha bendera kwenye nyumba zao na waliitwa "mabibi wa bendera" Dhaat-ur-rayyat).
Sayyid Qutb wa Misri katika kitabu chake, Milestone kilichochapishwa na International Islamic Federation of student organizations, Salimiah, Kuwait mnamo 1978 (uk; 48,49), amemnukuu mpokezi wa Hadithi mashuhuri, Imam Bukhari, juu ya desturi ya ndoa katika Arabia kabla ya Uislamu kama ifuatavyo:
"Shihab (az-Zuhri) amesema: 'Urwah b. az-Zubayt alimfahamisha yeye kwamba Aisha, mke wa Mtume (s.a.w.) alimjulisha kwamba ndoa wakati wa Ujahilia zilikuwa za aina nne:
1.        Moja ilikuwa ni ndoa ya watu kama ilivyo hivi sasa, ambapo mtu anamfungia uchumba mtoto wa kulea au binti yake kwa mtu mwingine, na huyu mwingine anatoa mahari kwa binti kisha anamuoa.
2.        Aina nyingine ilikuwa pale ambapo mtu alimwambia mkewe akiwa ametakasika kutokana na hedhi, 'Nenda kwa N. (yaani fulani) na muombe kufanya ngono naye;' kisha mumewe anakaa mbali naye na hamgusi kabisa mpaka iwe wazi kwamba ana mimba kutoka kwa mwanaume mwingine aliyefanya naye ngono.
Inapodhihirika kwamba anayo mimba, mumewe anafanya naye ngono kama akipenda. Anafanya hivyo kwa sababu tu ya kutaka kupata mtoto mwenye daraja (mwema). Aina hii ya ndoa ilijulikana kama nikah al-Istibda (ndoa ya kutafuta ngono).
3.  Aina nyingine ilikuwa pale ambapo kikundi cha wanaume chini ya kumi walipomtembelea mwanamke mmoja na wote wakawa wamefanya ngono naye. Kama alipata ujauzito na kuzaa mtoto, wakati siku kadhaa kupita baada ya kumzaa, aliwaita wote, na hakuna mmoja wao angeweza kukataa. Walipofika wote mbele yake, huwaambia 'Ninyi' mnajua matokeo ya matendo yenu; nimezaa mtoto na ni mwanao wewe, akimtaja anayemtaka kwa jina lake. Mtoto wake anaambatanishwa kwa mwanaume huyo, naye hangeweza kukataa.
4.  Aina ya nne ni wakati ambapo wanaume wengi wanapomuendea mwanamke mmoja mara kwa mara, na haepukani na yeyote anayemjia. Wanawake hawa ni malaya (baghaya). Walitumia kuweka mabango milangoni kwao kama ishara. Yeyote aliyewataka wao aliwaingilia.
Kama mmoja wao alishika mimba na akazaa mtoto, walijikusanya (wanaume) wote kwake na kumuita mtaalamu wa utambuzi wa Sura (physiognomist). Kisha walimuambatanisha mtoto huyo kwa mwanaume ambaye wamemfikiria ndio baba, na mtoto alibakia ameambatanishwa kwake na aliitwa mwanae, hakuna pingamizi lolote kwa mwenendo huu lililoweza kufanyika.

Alipokuja Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuhubiri haki alivunja aina zote za ndoa za ujahilia isipokuwa ile watu wanayotumia leo. Hivyo tuendelee kufuata mafundisho sahihi ya Mtume huyu mtukufu kwani kinyume chake ni upotofu.

Tuesday, 27 May 2014

Maana ya Ahlu-sunna:

Kuna maana tatu zinazotafsiri kinachokusudiwa kunako neno Ahlu-sunna,na maana hizo zinapatikana katika vitabu vya wanazuoni wa Kisunni. Na zimekuwa maana tatu kutokana na tofauti iliyopo baina yao kuhusiana na uhakika wa Istilahi hii Ahlu-sunna, lini hasa imeenza na ni nani mwanzilishi wa Istilahi hii.Tunazitaja maana hizo za neno Ahku-sunna kama ifuatavyo:

1-Madh-hebu ya Ahlu-sunna maana yake: Ni kundi la watu wa Hasan Al-basri, walioshikamana na "dhahiri ya Nassu" hata kama dhahiri hiyo inakwenda kinyume au inapingana na akili.
Kwa muhtasari: Maana hii inasema hivi:Ahlu-sunna ni kundi lile la waislaam waliokuwa wakiongozwa na Hasan Al-Basri, ambao hukabiliana na Dhahiri ya Nasu (kama vile kushikamana na dhahiri ya  hadithi au Riwaya) pasina kufanya tafsiri wala Taawili, sawa sawa (dhahiri ya Nasu hiyo) iwe inaafikiana na akili au inapingana na kwenda kinyume na akili.

Rejea: Al-firqatun-najia: Juzuu ya 1, Ukurasa wa 405.

2-Madh-hebu ya Ahlu-sunna: Maana yake ni yale madh-hebu aliyoyaasisi Abu Hasan Al-Ash-ari.

3-Madh-hebu ya Ahlu-sunna: Maana yake ni wale waislaam wanaoamini uhalali  na haki ya Ukhalifa wa Abubakari na Umar, na Uthman, na kwamba hao watatu  ukhalifa wao ni halali na ni haki kutangulia ukhalifa wa Imam Ali bin Abi Talib (a.s). Zaidi ya hilo pia huitikadia kuwa: KHERI NA SHARI VYOTE HUTOKA KWA MWENYEEZI MUNGU (S.W).
Hao ndio huitwa Ahlu-sunna.Kwa maana ikiwa wewe si mwenye kuamini au kuitikadia kuwa Khalifa wa kwanza ni Abubakar, na wa pili ni Omar na wa tatu ni Othman na wa nne ni Ali, bali unaamini na kuitikadia kuwa Khalifa wa kwanza ni Imam Ali Bin Abi Talib (a.s) kwa mujibu wa Nasuu (Hadithi) za Mtume (s.a.w.w), basi wewe hutoitwa kuwa ni katika Ahlu-sunna, na pia ukiwa unaamini kuwa Kheri hutoka kwa Mwenyeezi Mungu (s.w) na Shari haitoki kwa Mwenyeezi Mungu (s.w) bali hiyo ni natija au matokeo ya matendo ya watu, basi pia hilo litakufanya usiitwe au usiwe miongoni wa Madh-hebu hii ya Ahlu-sunna maana utakuwa umeenda kinyume na maana kamili ya neno Ahlu-sunna kama ilivyotajwa katika sehemu hii (namba 3). Maana hii namba tatu ndio maana anayoita mwanazuoni maarufu wa kissuni katika kitabu chake, anayeitwa: Abu Zuhra, na kitabu chake kinaitwa: Tarikh Al-madhahibul-Islamiyya. Na hii ndio maana yenye uzito zaidi kuliko maana zile mbili zilizotangulia.

Rejea: Tarikh Al-madhahibul-Islamiyya: Juzuu ya 2;ukurasa wa 58.


Ushia katika Mashariki ya Kati


UCHUMI WA UARABUNI KABLA YA UISLAMU

Kiuchumi, Wayahudi ndio waliokuwa viongozi wa Arabia. Walikuwa ndio wenye ardhi nzuri yenye kulimika katika Hijazi, na walikuwa wakulima wazuri zaidi nchini humo. Walikuwa pia ndio wawekezaji wa vile viwanda vilivyokuwepo katika Arabia wakati huo, na walikamata ukiritimba wa utengenezaji wa zana za kivita.
Utumwa ulikuwa ni asisi ya kiuchumi ya Waarabu. Watumwa wa kiume na wa kike waliuzwa na kununuliwa kama wanyama, na waliunda tabaka la waliokandamizwa zaidi katika jamii ya kiarabu.
Tabaka lenye nguvu zaidi, la waarabu, liliundwa na mabepari na wakopeshaji fedha. Viwango vya riba walivyotoza kwenye mikopo vilikuwa vikubwa mno, na viliundwa maalum kuwafanya matajiri zaidi na zaidi, na wale wakopaji kuwa masikini zaidi.
Vituo maarufu zaidi vya mjini katika Arabia vilikuwa Makka na Yathrib, vyote katika Hijazi. Wakazi wa Makka zaidi walikuwa ni wafanyabiashara, wachuuzi na wakopeshaji wa fedha.
Misafara yao ilisafiri wakati wa kiangazi kwenda Syria na wakati wa kipupwe kwenda Yemen. Walisafiri pia kwenda Bahrain upande wa Mashariki na Iraq upande wa Kaskazini Mashariki. Misafara ya biashara ilikuwa msingi wa uchumi wa Makka, na kuiendesha kwake kulihitaji ujuzi, uzoefu na uwezo.
R.V.C. Bodley asema:
"Kuwasili na kuondoka kwa misafara kulikuwa ni matukio muhimu katika maisha ya watu wa Makka. Karibu kila mmoja ndani ya Makka alikuwa na namna ya kitega uchumi katika ile mali ya maelfu ya ngamia, mamia ya watu, farasi na punda walioondoka na ngozi za wanyama, zabibu kavu na minara ya fedha na kurudi na mafuta, manukato na bidhaa mbalimbali kutoka Syria, Misri na Fursi (Persia/Iran), na viungo na dhahabu kutoka upande wa Kusini."
(The Messenger, 1946, Uk. 31)
Huko Yathrib, Waarabu waliendesha maisha yao kwa kilimo na Wayahudi waliendesha maisha yao kama wafanyabiashara na wanaviwanda. Lakini Wayahudi hawakuwa wafanyabiashara tu na viwanda; miongoni mwao pia walikuwepo wakulima wengi, na waliileta ardhi nyingi mbovu kwenye kulimika. Kiuchumi, kijamii na kisiasa, Hijazi ilikuwa ndio sehemu mashuhuri zaidi katika Arabia mwanzoni mwa karne ya saba.

Francesco Gabrielli anasema:
"Katika mkesha wa Uislamu, watu wenye kujishughulisha mno na walioendelea wa Arabia waliishi katika mji wa Maquraish. Wakati wa himaya za Arabu ya Kusini za Petra na Palmyra ulikuwa umepita kwa muda kiasi katika historia ya Arabia. Sasa hali ya baadae ilikuwa inaandaliwa hapo katika Hijazi."
(The Arabs - A Compact History-1963)
Waarabu na Wayahudi wote walikula riba. Wengi miongoni mwao walikuwa wala riba wajuzi; waliishi kwa riba waliyotoza kwenye mikopo yao.
E.A.Belyaev anaeleza:
"Riba ilitumika sana Makka, kwani ili kushiriki katika msafara wenye faida, watu wa Makka wengi waliokuwa na kipato cha wastani walikimbilia kwa wala riba; mbali na riba kubwa, angeweza kutegemea kupata faida baada ya kurudi salama kwa msafara. Wafanyabiashara matajiri zaidi walikuwa wachuuzi na wala riba.
Wakopeshaji fedha kwa kawaida walichukua dinari kwa dinari, dirham kwa dirham, kwa maneno mengine, asilimia mia moja ya riba. Katika Qur'an 3:125, Allah (s.w.t.) akiwaambia waumini, alisema: 'Msile riba mara mbili maradufu.' Hii ingeweza kumaanisha kwamba riba ya asilimia mia mbili au hata mia nne ilidaiwa.
Nyavu za riba ya Makka hazikuwakamata wakazi wenzao tu na wa makabila yao bali pia watu wa makabila ya KiBedui ya Hijazi walioshugulika katika biashara ya Makka. Kama katika Athens ya zamani "njia kuu za kukandamiza uhuru wa watu zilikuwa ni pesa."

(Arabs, Islamu and the Arab Caliphate in Early Middle Ages, 1969)

Monday, 26 May 2014

SILAHA MPYA YA MAWAHHABI KTK KUKABILIANA NA DALILI PAMOJA NA HOJA ZA WAFUASI WA AHLUL BAIT (A.S) KIZAZI KITUKUFU CHA MTUME (S.A.W.W):

Siku hizi imeibuka kauli mpya ya kiwahhabi nayo ni hii:Washindwa kustahmili vishindo vya Dalili na Hoja zenye nguvu kuhusu mas-ala mbalimbali zitolewazo na Mashia Wafuasi wa Qur'an Tukufu na Itrah wa Mtume (s.a.w.w) yaani Maimam Watukufu ambao ndio Ahlul-Bait wake (a.s),basi utawaona wakihaha na kukimbilia neno lao dhaifu wakisema:HUU NI UONGOOO!
Hilo ndio neno lao ambalo sasa wanalitumia kukwepa dalili na hoja ambazo zinawajia mithili ya vimondo vyenye kuunguza fikra zao na itikadi zao za kiwahhabi ambazo zipo mbali kabisa na uislam kama vile fikra ya kuharamisha kusoma khitma kwa Maiti wetu,au kuharamisha kwao Maulid ya kuzaliwa Mtume wetu (s.a.w.w),au kuharamisha kwa Ziara kwa Mtume (s.a.w.w),au kuharamisha kwao Video na Picha ati haram kutizama video au kupiga picha,au kama vile kuharamisha kwao mwanamke wa Kiislam kusoma elimu ya Dunia kwamba ni haram kwake kuingia University kutafuta elimu ya Secular,au kama vile kuharamisha kwao Kufanya Tawassuli kwa Mtume (s.a.w.w) na kwa Mawalii wa Mweenyeezi Mungu (s.w),au kama vile kuharamisha kwao kuweka makochi ndani ya Nyumba ati ni Haram kwa kuwa Mtume (s.a.w.w) hakukalia makochi,au kama vile kuharamisha kwao Mwanamke kuwa Kiongozi,au kama vile kauli yao kwamba muislam asiyekata suruali au kanzu (kwa panga) na kuvaa kipisi cha kanzu au kipisi cha suruali basi huyo kwa mtazamo wao si muislam ni Kafiri, au yeyote yule anayepinga itikadi yoyote ile ya kiwahhabi ambapo humkafirisha sawa sawa awe Sunni au Shia......na na mengine mengi kuhusu fikra zao zilizo nje bali mbali kabisa na uislam.Tunapozitokomeza fikra kwa hoja na dalili maridadi basi huwa hawana hoja za kiakili wala kunakili zenye mashiko ili kukabiliana na hoja zenye nguvu wanazokumbana nazo hivyo siku hizi wamegundua njia ya kukabiliana na hoja wasizoziweza kuzibatilisha.Njia hiyo ni kusema kwao neno hili:HUU NI UNGOOOO! au utaskia wakisema: UMEDANGANYAAAAA!
Ushari wetu kwa Mawahhabi:
............................................
Ndugu Wahhabi ktk Maumbile:
Acha uwahhabi na fikra za Kiwahhabi za upotokaji ndio utaongoka,na ndio utakuwa
ukisoma post za Wafuasi wa Ahlul-Bait (a.s) na kuzielewa,kisha kufahamu na mwisho kujua ulichokisema.
Ama silaha yako hiyo dhaifu uliyoivumbua siku hizi ili kukabiliana na post zenye hoja kwa kusema HUU NI UONGO !!! Hiyo tunaichukulia sisi kama (kelele),kwa maana namna hiyo utahesabika kuwa (una_make noise),na kumake noise hiyo ni silaha ya Jahili,huyo ndiye hukabiliana na hoja kwa neno
hilo akisena Uongooooooo!!!
Ama Silaha ya mwenye elimu ni kutaja (hoja na dalili zake) ili kubatilisha dalili alizokumbana nazo,na sio kutumia muda wake kumake noise zilizo changanyika
na kelele.
Huu ni ushauri wa bure kwa Wafuasi wa Muhammad Bin Abdil Wahhabi wanaoitwa Mawahhabi ambao siku hizi wanajiita Sunni hali ya kuwa usunni Mwingine na Uwahhabi Mwingine tofauti kabisa kama vile JUA na MWEZI !.
Washukran.

Sunday, 25 May 2014

Swali langu kwa Mawahhabi na Matakfir wengine.

Je hivi mnasema kwa kujiamini kuwa, "Ni Kafiri asiyekubali Uimamu wa Yazidi ibn Muawiyyah ambaye uovu wake unaeleweka kwa Waislamu wote? Na itoshe uovu na udhalimu wa Yazidi kwa maelezo walioafikiana Waislamu wote kutokana na yeye kuruhusu kufanyika maasi kwenye mji Mtakatifu wa Madina kwa kutumia jeshi lake na askari wake kufanya wayatakayo mjini humo ili wachukuwe viapo vya utii (kutoka kwa watu) kwa nguvu kana kwamba (watu hao) ni watumwa wake. Si hivyo tu, bali askari wa Yazid waliwaua maelfu ya Masahaba watukufu na Tabiina, wakavunja heshima za wanawake na wasichana wa Kiislamu waliojihifadhi kiasi walizaliwa kutokana na uchafu huo idadi ya watoto ambao hakuna awezaye kuidhibiti isipokuwa Mwenyezi Mungu.
Na yamtosha Yazidi aibu mbaya mno na udhalimu wa kudumu kule kumuuwa Bwana wa vijana wa peponi na kuwateka Mabinti wa Mtume na kuyachokora meno ya Husein (a.s.) kwa kijiti kisha kuimba kwake beti za ushairi ambazo ni maarufu akasema, "Laiti wazee wangu (waliouawa) katika Badri wangeshuhudia..." Mpaka akafikia kusema: "Banu Hashim walichezea Ufalme, hakuna habari yeyote iliyokuja wala Ufunuo ulioshuka."
Ni wazi kabisa kwamba hakuamini utume wa Muhammad (s.a.w.w.) wala Qur'an Tukufu, basi je, ni kweli mnaafiki kumkufurisha anayejitenga na Yazid? Na baba yake Muawiyyah ambaye alikuwa akimlaani Ali (a.s) na huamuru alaaniwe, bali na (alikuwa) akimuuwa kila anayekataa kufanya hivyo miongoni mwa Masahaba wema kama alivyomfanyia Hujr ibn Adiyy Al-Kindi na jamaa zake, na (tendo la kumlaani Ali a.s.) aliliusia likawa ni sunna iliyofuatwa kwa miaka sabini hali ya kuwa (Muawiyyah) anaijua kauli ya Mtume (s.a.w.w.) aliposema "Yeyote atakayemtukana Ali, basi kanitukana mimi, na atakayenitukana mimi amemtukana Mwenyezi Mungu". Kama ambavyo zilivyoandika Sahih za Ahli-Sunnah kwa ziyada ya matendo aliyoyatenda miongoni mwa mambo yanayopingana na Uislamu kwa kuwauwa watu wema wasio na kosa ili achukue kwao kiapo cha utii kwa ajili ya mwanawe Yazid. Vilevile kumuua kwake, Hassani ibn Ali (a.s.) kwa kumtumia Ju'da binti Ash-ath, na maovu mengine mengi yanatajwa na historia kwa Masunni kama ambavyo pia yanashuhudiwa na wafuasi wa Imam Ali (a.s.).
Mim, sikudhani kwamba ninyi mnaafikiana na hayo, vinginevyo basi na tuyaache kama yalivyo, na ikifika hapo basi hapatabakia baada ya hayo kipimo wala akili, wala sheria na wala hekima pia dalili. Na Mwenyezi Mungu anasema: "Enyi mlioamini mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli." (Qur'an, 9:119)

MAOMBI YANGU KWA MAWAHHABI

Nakuiteni kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na sunna ya Mtume wake, semeni kweli wazi wazi kwa sauti kubwa japokuwa ni chungu itakushuhudieni mbele ya Mwenyezi Mungu.
Naapa kwa Mola wako hivi kwenu ninyi Mashia siyo Waislamu? Hivi kweli mnaitakidi kwamba wao ni makafiri? Je wafuasi wa Watu wa nyumba ya Mtume ambao wanampwekesha Mwenyezi Mungu na kumtukuza zaidi kuliko vikundi vyote kwa usemi wao wa kuwa hafanani na chochote kwa kumtakasa kutokana na kufanana, na kutokana na kuwa hana umbo na mwili. Si hivyo tu bali wanamuamini Mtume wake Muhammad (s.a.w.w.) na wanamuheshimu mno kuliko vikundi vyote wasemapo kuwa, "Yeye Mtume ni Maasum moja kwa moja hata kabla ya kupewa utume". Je, hawa ndiyo munaowahukumu kuwa ni makafiri?
Je, wale wanaomtawalisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini na wanawapenda kizazi cha Mtume na kuwatawalisha kama alivyowatambulisha Ibn Mandhur ndani ya "Lisanul-A'rab" katika mada ya Shia, basi je ninyi mwasema kwamba wao siyo Waislamu?
Je, Mashia hawa ambao wanatekeleza wajibu wa Sala kwa namna iliyo bora, na wanatoa Zaka na kuzidisha juu yake Khumsi ya mali zao kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wanafunga (saumu ya) mwezi wa Ramadhani na nyingine na wanahiji nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu na kuyatukuza mambo matukufu ya Mwenyezi Mungu, kadhalika wanawaheshimu Mawalii wa Mwenyezi Mungu na kujiepusha na maadui wa Uislamu, hivyo kwenu ninyi watu hawa ni washirikina?
Je, hivi watu wasemao kuwa Uimamu hasa ni (haki) wa Maimamu kumi na wawili kutoka katika watu wa nyumba ya Mtume ambao Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na amewatakasa sana sana, na Mtume wa Mwenyezi Mungu aliwataja kama alivyotoa Bukhari na Muslim na wengineo katika Sahihi za Ahlu-Sunnah, hivi watu hawa kwenu ninyi ni watu waliotoka nje ya Uislamu?
Je hivi kuna siku ambayo Waislamu wamekuwa hawautambui Uimamu na wala hawakubali sawa sawa liwe hilo katika uhai wa Mtume au baada ya kufa kwake mpaka kufikie kuihusisha nadharia ya Uimamu kwa Waajemi na Majusi?
Na je hivi mnasema kwa kujiamini kuwa, "Ni Kafiri asiyekubali Uimamu wa Yazidi ibn Muawiyyah ambaye uovu wake unaeleweka kwa Waislamu wote? Na itoshe uovu na udhalimu wa Yazidi kwa maelezo walioafikiana Waislamu wote kutokana na yeye kuruhusu kufanyika maasi kwenye mji Mtakatifu wa Madina kwa kutumia jeshi lake na askari wake kufanya wayatakayo mjini humo ili wachukuwe viapo vya utii (kutoka kwa watu) kwa nguvu kama kwamba (watu hao) ni watumwa wake. Si hivyo tu, bali wa Yazid waliwaua maelfu ya Masahaba watukufu na Tabiina, wakavunja heshima za wanawake na wasichana wa Kiislamu waliojihifadhi kiasi walizaliwa kutokana na uchafu huo idadi ya watoto ambao hakuna awezaye kuidhibiti isipokuwa Mwenyezi Mungu

KWA NINI WAISLAMU WANARUDI KWENYE ENZI YA UJINGA YAANI KABLA YA UISLAM.

"Katika karne ya kabla ya kuja Uislamu makabila yalitawanya nguvu zao zote katika vita vya kuviziana, wote dhidi ya wote."
(Classical Islam - A History 600-1258-1970)
Yale makabila ya wahamaji yalizunguka kwenye peninsula yote na kupora misafara na makazi madogomadogo. Misafara mingi na vijiji vilinunua kinga ya mashambulizi Haya kwa kulipa kiwango maalum cha fedha kwa watekanyara wa wahamaji.
Ni muhimu kuzingatia ule ukweli katika usiku wa kuzaliwa Uislamu hakukuwa na serikali katika ngazi yoyote katika Arabia, na ukweli huu unawezakuwa umeathiri kuinukia kwa Uislamu wenyewe. Ukosekanaji mzima wa serikali, hata katika hali ya kuanzishwa tu, ni kitu kisichokuwa cha kawaida kabisa kwamba kimeonwa na kutolewa maoni na mus-tashirik wengi, miongoni mwao ni:
"Arabia ingebakia ya kipagani angekuwapo mtu katika Makka ambaye angeweza kutoa pigo; ambaye angeweza kutenda. Lakini wengi wao, kama walivyokuwa wabaya wa Mohammed, hapakuwa na mmoja wao aliyekuwa na ujasiri wa namna hii; na (kama ilivyoonekana) hapakuwepo na mahakimu kwa ujumla ambao kwao angeweza kushitakiwa."
(Mohammed and the Rise of Islam, 1971).

Naye Maxime Rodinson asema:
"Mauaji ya halaiki yalibeba adhabu kubwa kwa mujibu wa sheria zisizoandikwa za jangwani. Katika utendaji waarabu huru walikuwa hawakufungwa na kanuni ya sheria zake kwa msaada wa jeshi la polisi. Ulinzi pekee wa maisha ya mtu ni ile hakika iliyowekwa na mila na desturi, ambayo ingenunuliwa kwa gharama kubwa. damu kwa damu na uhai kwa uhai. "
(Mohammed, 1971) Asema Herbert J. Muller:
"Katika Arabia ya Mohammed hakukuwa na dola kulikuwa tu na makabila huru yaliyotangaa na miji. Huyu Mtume (s.a.w.) aliunda dola yake mwenyewe, na aliipa sheria tukufu iliyoandikwa na Allah (s.w.t.)"
(The Loom of History, 1958)
Watu wa Arabia walitokana na makundi mawili, wenye maskani na wahamiaji. Hijazi na Arabia ya Kusini ilitapakaa miji mingi midogo na mikubwa michache. Nchi yote iliyobakia illikuwa na watu waliotapakaa wakitokana na Mabedui. Walikuwa nyuma katika dhana ya uraia na siasa lakini pia walikuwa ni chanzo cha wasiwasi na hofu kwa wale wenye maskani. Waliishi kama maharamia wa jangwani, na walikuwa na sifa mbaya kwa ubinafsi wao usiozuilika na vurugu zao za upambanuzi wa kikabila.
Yale makabila maarufu zaidi yalitumia kiwango maalum cha mamlaka katika maeneo yao husika. Katika Makka kabila lenye nguvu lilikuwa la Quraishi, katika Yathrib, makabila yenye nguvu yalikuwa ni yale makabila ya Kiarabu ya Aus na Khazraji, na makabila ya kiyahudi ya Nadhir, Qaynuqa'a na Quraydha. Maquraishi wa Makka walijiona wenyewe ni bora kuliko Mabedui lakini hawa Mabedui walikuwa na dharau tu juu ya hawa watu wa mjini ambao kwao wao walikuwa ni "Taifa la wauza maduka tu".
Waarabu wote walikuwa na sifa mbaya kwa namna fulani ya tabia kama vile majivuno, kiburi na majisifu, ulipizaji kisasi na kupenda kwingi uporaji. Kiburi chao kilihusika kwa namna fulani na kushindwa kwao kuanzisha dola yao wenyewe. Walikosa nidhamu ya kisiasa, na mpaka kuja kwa Uislamu, hawakutambua mamlaka yoyote kama ni yenye umuhimu mkubwa katika Arabia.
Walitambua mamlaka ya mtu aliyewaongoza kwenye uvamizi lakini angeweza kulazimisha utii wao ikiwa tu walikuwa na uhakika wa kupata mgao mzuri wa ngawira, na mamlaka yake yaliisha mara tu shughuli hiyo ilipokwisha.

CHA KUSHANGAZA KARNE 14 BAADA YA KUWA WAISLAMU, BAADHI YA WAISLAMU WANADESTURI ZILEZILE ZA UJIMA. HAWATAKI KUITII SERIKALI YOYOTE, VISASI NI IBADA KWAO, HAWANA UTII SI KWA VIONGOZI WA SERIKALI BALI HATA MASHEIKH WAO WENYEWE. SI AJABU KUSIKIA MWANAFUNZI AKIMKUFURISHA MWALIMU WAKE. HUU NI MSIBA MKUBWA KATIKA UMMA HUU WA KIISLAMU.

Friday, 16 May 2014

HALI YA KISIASA YA ARABIA KABLA YA UISLAMU

Sura inayoonekana sana ya maisha ya kisiasa ya Arabia kabla ya Uislamu ilikuwa ni kutokuwepo kabisa kwa mfumo wa kisiasa katika muundo wowote ule. Ukiiondoa Yemen iliyoko Kusini Magharibi, hakuna sehemu ya peninsula ya Arabia iliyokuwa na serikali kwa wakati wowote ule, na Waarabu kamwe hawakutambua mamlaka yoyote ile mbali na mamlaka ya machifu wao wa makabila yao. Haya mamlaka ya machifu wa kikabila hata hivyo, yaliegama, kwa namna nyingi, juu ya tabia na nafasi zao, na yalikuwa ya uungwana kuliko kisiasa.
Mwanafunzi wa kisasa wa historia anaona mshangao kwamba Waarabu wameishi, kizazi baada ya kizazi, karne baada ya karne, bila ya serikali ya aina yoyote ile. Kwa vile hapakuwa na serikali, hapakuwa na sheria na utulivu. Kanuni pekee ya nchi ilikuwa ni hali ya uhalifu. Kama inavyotokea, inapofanyika jinai, upande uliodhuriwa ulichukua hatua mikononi mwao, na ukajaribu kupitisha 'hukumu' kwa yule mwovu. Mtindo huu ulisababisha mara nyingi matendo ya ukatili wa kuogofya.
Kama Waarabu walifanya kiasi kidogo cha kujizuia, haikuwa ni kwa sababu ya wepesi wa hisia alizokuwa nazo juu ya maswali ya kweli na batili lakini ni kwa sababu ya kuhofia kuchochea visasi na mauaji ya kurithi kisasi. Mauaji ya kisasi cha kurithi yalimaliza vizazi vizima vya Waarabu. Kwa vile hakukuwepo na vitu kama polisi, mahakama au majaji, ulinzi pekee mtu alioweza kuupata kutokana na maadui zake, ulikuwa katika kabila lake mwenyewe.
Kabila lilikuwa na jukumu la kulinda watu wake hata kama walitenda maovu. Ukabila au 'asabiyya' (moyo wa kiukoo) ulichukua nafasi ya kwanza kabla ya maadili. Kabila lililoshindwa kulinda watu wake kutokana na maadui zao lilijihatarisha kwenye kebehi, kashfa na dharau. Maadili, kwa kweli hayakuingia kwenye picha mahali popote pale. Kwa vile Arabia haikuwa na serikali; na kwa vile waarabu walikuwa na utawala huria kwa silika yao, walifungana katika mapigano yasiyokwisha. Vita ilikuwa ni desturi ya kudumu ya jamii ya kiarabu. Jangwa liliweza kuchukua idadi ndogo tu ya watu, na hali ya vita vya kikabila ilidumisha uthibiti mkali juu ya ongezeko la watu. Lakini Waarabu wenyewe hawakuiona vita katika mwanga huu. Kwao wao, vita vilikuwa burudani au kiasi mchezo wa hatari, au aina ya tamthiliya ya kikabila, iliyofanywa na wenye weledi (ubingwa), kwa mujibu wa mfumo wa kanuni za zamani na ushujaa, ambapo "watazamaji" walishangilia.
Amani ya kudumu haikuwa na mvuto kwao na vita vilitoa fursa ya kukwepa kazi ngumu na kutokubadilika kwa mwenendo wa maisha katika jangwa. Wao kwa hiyo walichochea msisimko wa mapambano ya silaha. Vita viliwapa fursa ya kuonyesha vipaji vyao katika kutupa mishale, ufundi wa kurusha panga na upandaji wa farasi, na pia, katika vita, wangeweza kujipatia sifa kwa ushujaa wao na wakati huohuo kuleta fahari na heshima kwa makabila yao. Kwa mara nyingi, Waarabu walipigana ili kupigana tu, ama iwepo au isiwepo sababu ya kuchochea vita.
Kwa bahati mbaya mpaka leo kuna baadhi ya watu wanaojifanya waislamu wamekuwa na tabia za kupenda vita na kuuwa watu kama ilivyokuwa kabla ya Uislamu. Uislam haujafanikiwa kuwakomboa watu hawa wenye uchu wa kumwaga damu ya waislamu. Kiongozi wa wamwaga damu hawa ni Muhammad ibn Abdul-wahhab aliyeirithi tabia hii mbaya toka kwa Ibn Taimiyyah na Maswahhaba waovu kama Khalid ibn Walid.

Twin bomb blasts kill 10, injure 70 in Nairobi

         
Police work to control a crowd of onlookers at the scene of an explosion on May 16, 2014 on the outskirts of Nairobi's business district where twin explosions claimed at least 10 lives.


At least 10 people have been killed and over 70 others injured during twin bomb explosions in a busy market in the Kenyan capital Nairobi, officials say.

Police said a blast hit a 14-seater public minibus, known as matatu, while another bomb went off inside the Gikomba Market just east of Nairobi’s busy central business district, the National Disaster Operation Centre (NDOC) said Friday.
The two explosions were caused by improvised explosive devices and “were detonated simultaneously,” said Nairobi police chief Benson Kibue.
One suspect has been arrested over the attack on the second-hand clothes market in the city.
A spokesman at the Kenyatta National Hospital, Nairobi's main hospital, said at least 70 people have been injured in the incident, many of them in serious condition.

“Many of the injured are bleeding profusely. We need a lot of blood,” the spokesman, Simon Ithae, said as the hospital issued an appeal for donors.
Nairobi and the port city of Mombasa have been rocked by a series of explosions since September.
On April 13, four people, including two police officers, were killed in a car bomb explosion outside a police station in a poor neighborhood of Nairobi.
In September last year, an attack on the Westgate Mall in Nairobi killed at least 67 people.
Somali fighters have been blamed for the attacks.
Al-Shabab fighters said the raid on the mall was in retaliation for Kenya’s military presence in Somalia. The Kenyan forces along with troops from Uganda, Burundi, Djibouti, Sierra Leone, and Ethiopia are part of the African Union Mission in Somalia (AMISOM).