Friday, 30 May 2014

ARABIA KABLA YA UISLAMU 4 --------- HALI YA USTAWI WA JAMII

Arabia ilikuwa ni jamii iliyoshikiliwa na wanaume. Wanawake hawakuwa na hadhi ya aina yoyote zaidi ya kuwa bidhaa za ngono. Idadi ya wanawake mtu anayoweza kuoa haikukadiriwa. Mwanaume alipokufa, mwanae 'alirithi' wake zake wote isipokuwa mama yake mzazi tu. Tabia ya kikatili ya Waarabu ilikuwa ni kuwazika watoto wao wa kike wachanga wakiwa hai. Hata kama Mwarabu hakutaka kumzika binti yake akiwa hai, alikuwa bado lazima adumishe mila hii ya 'heshima' kwa vile hana uwezo wa kuhimili shinikizo la jamii.
Ulevi ullikuwa ni mazoea mabaya ya kawaida ya Waarabu. Ulevi wao ulifuatana na uchezaji kamari. Walikuwa walevi waliokithri na wacheza kamari waliokubuhu. Mahusiano ya jinsia zao yalikuwa yamelegea sana. Wanawake wengi waliuza mapenzi kupata maisha yao kwa vile kulikuwa na kidogo sana kingine ambacho wangeweza kufanya. Wanawake hawa walipeperusha bendera kwenye nyumba zao na waliitwa "mabibi wa bendera" Dhaat-ur-rayyat).
Sayyid Qutb wa Misri katika kitabu chake, Milestone kilichochapishwa na International Islamic Federation of student organizations, Salimiah, Kuwait mnamo 1978 (uk; 48,49), amemnukuu mpokezi wa Hadithi mashuhuri, Imam Bukhari, juu ya desturi ya ndoa katika Arabia kabla ya Uislamu kama ifuatavyo:
"Shihab (az-Zuhri) amesema: 'Urwah b. az-Zubayt alimfahamisha yeye kwamba Aisha, mke wa Mtume (s.a.w.) alimjulisha kwamba ndoa wakati wa Ujahilia zilikuwa za aina nne:
1.        Moja ilikuwa ni ndoa ya watu kama ilivyo hivi sasa, ambapo mtu anamfungia uchumba mtoto wa kulea au binti yake kwa mtu mwingine, na huyu mwingine anatoa mahari kwa binti kisha anamuoa.
2.        Aina nyingine ilikuwa pale ambapo mtu alimwambia mkewe akiwa ametakasika kutokana na hedhi, 'Nenda kwa N. (yaani fulani) na muombe kufanya ngono naye;' kisha mumewe anakaa mbali naye na hamgusi kabisa mpaka iwe wazi kwamba ana mimba kutoka kwa mwanaume mwingine aliyefanya naye ngono.
Inapodhihirika kwamba anayo mimba, mumewe anafanya naye ngono kama akipenda. Anafanya hivyo kwa sababu tu ya kutaka kupata mtoto mwenye daraja (mwema). Aina hii ya ndoa ilijulikana kama nikah al-Istibda (ndoa ya kutafuta ngono).
3.  Aina nyingine ilikuwa pale ambapo kikundi cha wanaume chini ya kumi walipomtembelea mwanamke mmoja na wote wakawa wamefanya ngono naye. Kama alipata ujauzito na kuzaa mtoto, wakati siku kadhaa kupita baada ya kumzaa, aliwaita wote, na hakuna mmoja wao angeweza kukataa. Walipofika wote mbele yake, huwaambia 'Ninyi' mnajua matokeo ya matendo yenu; nimezaa mtoto na ni mwanao wewe, akimtaja anayemtaka kwa jina lake. Mtoto wake anaambatanishwa kwa mwanaume huyo, naye hangeweza kukataa.
4.  Aina ya nne ni wakati ambapo wanaume wengi wanapomuendea mwanamke mmoja mara kwa mara, na haepukani na yeyote anayemjia. Wanawake hawa ni malaya (baghaya). Walitumia kuweka mabango milangoni kwao kama ishara. Yeyote aliyewataka wao aliwaingilia.
Kama mmoja wao alishika mimba na akazaa mtoto, walijikusanya (wanaume) wote kwake na kumuita mtaalamu wa utambuzi wa Sura (physiognomist). Kisha walimuambatanisha mtoto huyo kwa mwanaume ambaye wamemfikiria ndio baba, na mtoto alibakia ameambatanishwa kwake na aliitwa mwanae, hakuna pingamizi lolote kwa mwenendo huu lililoweza kufanyika.

Alipokuja Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuhubiri haki alivunja aina zote za ndoa za ujahilia isipokuwa ile watu wanayotumia leo. Hivyo tuendelee kufuata mafundisho sahihi ya Mtume huyu mtukufu kwani kinyume chake ni upotofu.

No comments:

Post a Comment