"Katika karne ya kabla ya kuja Uislamu makabila yalitawanya
nguvu zao zote katika vita vya kuviziana, wote dhidi ya wote."
(Classical Islam - A History 600-1258-1970)
Yale makabila ya wahamaji yalizunguka kwenye peninsula yote na
kupora misafara na makazi madogomadogo. Misafara mingi na vijiji vilinunua
kinga ya mashambulizi Haya kwa kulipa kiwango maalum cha fedha kwa watekanyara
wa wahamaji.
Ni muhimu kuzingatia ule ukweli katika usiku wa kuzaliwa Uislamu
hakukuwa na serikali katika ngazi yoyote katika Arabia, na ukweli huu
unawezakuwa umeathiri kuinukia kwa Uislamu wenyewe. Ukosekanaji mzima wa
serikali, hata katika hali ya kuanzishwa tu, ni kitu kisichokuwa cha kawaida
kabisa kwamba kimeonwa na kutolewa maoni na mus-tashirik wengi, miongoni mwao
ni:
"Arabia ingebakia ya kipagani angekuwapo mtu katika Makka
ambaye angeweza kutoa pigo; ambaye angeweza kutenda. Lakini wengi wao, kama
walivyokuwa wabaya wa Mohammed, hapakuwa na mmoja wao aliyekuwa na ujasiri wa
namna hii; na (kama ilivyoonekana) hapakuwepo na mahakimu kwa ujumla ambao kwao
angeweza kushitakiwa."
(Mohammed and the Rise of Islam, 1971).
Naye Maxime Rodinson
asema:
"Mauaji ya halaiki yalibeba adhabu kubwa kwa mujibu wa sheria
zisizoandikwa za jangwani. Katika utendaji waarabu huru walikuwa hawakufungwa
na kanuni ya sheria zake kwa msaada wa jeshi la polisi. Ulinzi pekee wa maisha
ya mtu ni ile hakika iliyowekwa na mila na desturi, ambayo ingenunuliwa kwa
gharama kubwa. damu kwa damu na uhai kwa uhai. "
(Mohammed, 1971) Asema Herbert J. Muller:
"Katika Arabia ya Mohammed hakukuwa na dola kulikuwa tu na
makabila huru yaliyotangaa na miji. Huyu Mtume (s.a.w.) aliunda dola yake
mwenyewe, na aliipa sheria tukufu iliyoandikwa na Allah (s.w.t.)"
(The Loom of History, 1958)
Watu wa Arabia walitokana na makundi mawili, wenye maskani na
wahamiaji. Hijazi na Arabia ya Kusini ilitapakaa miji mingi midogo na mikubwa
michache. Nchi yote iliyobakia illikuwa na watu waliotapakaa wakitokana na
Mabedui. Walikuwa nyuma katika dhana ya uraia na siasa lakini pia walikuwa ni
chanzo cha wasiwasi na hofu kwa wale wenye maskani. Waliishi kama maharamia wa
jangwani, na walikuwa na sifa mbaya kwa ubinafsi wao usiozuilika na vurugu zao
za upambanuzi wa kikabila.
Yale makabila maarufu zaidi yalitumia kiwango maalum cha mamlaka
katika maeneo yao husika. Katika Makka kabila lenye nguvu lilikuwa la Quraishi,
katika Yathrib, makabila yenye nguvu yalikuwa ni yale makabila ya Kiarabu ya
Aus na Khazraji, na makabila ya kiyahudi ya Nadhir, Qaynuqa'a na Quraydha. Maquraishi
wa Makka walijiona wenyewe ni bora kuliko Mabedui lakini hawa Mabedui walikuwa
na dharau tu juu ya hawa watu wa mjini ambao kwao wao walikuwa ni "Taifa
la wauza maduka tu".
Waarabu wote walikuwa na sifa mbaya kwa namna fulani ya tabia kama
vile majivuno, kiburi na majisifu, ulipizaji kisasi na kupenda kwingi uporaji.
Kiburi chao kilihusika kwa namna fulani na kushindwa kwao kuanzisha dola yao wenyewe.
Walikosa nidhamu ya kisiasa, na mpaka kuja kwa Uislamu, hawakutambua mamlaka
yoyote kama ni yenye umuhimu mkubwa katika Arabia.
Walitambua mamlaka ya mtu aliyewaongoza kwenye uvamizi lakini
angeweza kulazimisha utii wao ikiwa tu walikuwa na uhakika wa kupata mgao mzuri
wa ngawira, na mamlaka yake yaliisha mara tu shughuli hiyo ilipokwisha.
CHA KUSHANGAZA KARNE 14 BAADA YA KUWA WAISLAMU, BAADHI YA WAISLAMU
WANADESTURI ZILEZILE ZA UJIMA. HAWATAKI KUITII SERIKALI YOYOTE, VISASI NI IBADA
KWAO, HAWANA UTII SI KWA VIONGOZI WA SERIKALI BALI HATA MASHEIKH WAO WENYEWE.
SI AJABU KUSIKIA MWANAFUNZI AKIMKUFURISHA MWALIMU WAKE. HUU NI MSIBA MKUBWA
KATIKA UMMA HUU WA KIISLAMU.
No comments:
Post a Comment