Sunday 25 May 2014

MAOMBI YANGU KWA MAWAHHABI

Nakuiteni kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na sunna ya Mtume wake, semeni kweli wazi wazi kwa sauti kubwa japokuwa ni chungu itakushuhudieni mbele ya Mwenyezi Mungu.
Naapa kwa Mola wako hivi kwenu ninyi Mashia siyo Waislamu? Hivi kweli mnaitakidi kwamba wao ni makafiri? Je wafuasi wa Watu wa nyumba ya Mtume ambao wanampwekesha Mwenyezi Mungu na kumtukuza zaidi kuliko vikundi vyote kwa usemi wao wa kuwa hafanani na chochote kwa kumtakasa kutokana na kufanana, na kutokana na kuwa hana umbo na mwili. Si hivyo tu bali wanamuamini Mtume wake Muhammad (s.a.w.w.) na wanamuheshimu mno kuliko vikundi vyote wasemapo kuwa, "Yeye Mtume ni Maasum moja kwa moja hata kabla ya kupewa utume". Je, hawa ndiyo munaowahukumu kuwa ni makafiri?
Je, wale wanaomtawalisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini na wanawapenda kizazi cha Mtume na kuwatawalisha kama alivyowatambulisha Ibn Mandhur ndani ya "Lisanul-A'rab" katika mada ya Shia, basi je ninyi mwasema kwamba wao siyo Waislamu?
Je, Mashia hawa ambao wanatekeleza wajibu wa Sala kwa namna iliyo bora, na wanatoa Zaka na kuzidisha juu yake Khumsi ya mali zao kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wanafunga (saumu ya) mwezi wa Ramadhani na nyingine na wanahiji nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu na kuyatukuza mambo matukufu ya Mwenyezi Mungu, kadhalika wanawaheshimu Mawalii wa Mwenyezi Mungu na kujiepusha na maadui wa Uislamu, hivyo kwenu ninyi watu hawa ni washirikina?
Je, hivi watu wasemao kuwa Uimamu hasa ni (haki) wa Maimamu kumi na wawili kutoka katika watu wa nyumba ya Mtume ambao Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na amewatakasa sana sana, na Mtume wa Mwenyezi Mungu aliwataja kama alivyotoa Bukhari na Muslim na wengineo katika Sahihi za Ahlu-Sunnah, hivi watu hawa kwenu ninyi ni watu waliotoka nje ya Uislamu?
Je hivi kuna siku ambayo Waislamu wamekuwa hawautambui Uimamu na wala hawakubali sawa sawa liwe hilo katika uhai wa Mtume au baada ya kufa kwake mpaka kufikie kuihusisha nadharia ya Uimamu kwa Waajemi na Majusi?
Na je hivi mnasema kwa kujiamini kuwa, "Ni Kafiri asiyekubali Uimamu wa Yazidi ibn Muawiyyah ambaye uovu wake unaeleweka kwa Waislamu wote? Na itoshe uovu na udhalimu wa Yazidi kwa maelezo walioafikiana Waislamu wote kutokana na yeye kuruhusu kufanyika maasi kwenye mji Mtakatifu wa Madina kwa kutumia jeshi lake na askari wake kufanya wayatakayo mjini humo ili wachukuwe viapo vya utii (kutoka kwa watu) kwa nguvu kama kwamba (watu hao) ni watumwa wake. Si hivyo tu, bali wa Yazid waliwaua maelfu ya Masahaba watukufu na Tabiina, wakavunja heshima za wanawake na wasichana wa Kiislamu waliojihifadhi kiasi walizaliwa kutokana na uchafu huo idadi ya watoto ambao hakuna awezaye kuidhibiti isipokuwa Mwenyezi Mungu

No comments:

Post a Comment