Je hivi mnasema kwa kujiamini kuwa, "Ni Kafiri asiyekubali Uimamu wa Yazidi ibn Muawiyyah ambaye uovu wake unaeleweka kwa Waislamu wote? Na itoshe uovu na udhalimu wa Yazidi kwa maelezo walioafikiana Waislamu wote kutokana na yeye kuruhusu kufanyika maasi kwenye mji Mtakatifu wa Madina kwa kutumia jeshi lake na askari wake kufanya wayatakayo mjini humo ili wachukuwe viapo vya utii (kutoka kwa watu) kwa nguvu kana kwamba (watu hao) ni watumwa wake. Si hivyo tu, bali askari wa Yazid waliwaua maelfu ya Masahaba watukufu na Tabiina, wakavunja heshima za wanawake na wasichana wa Kiislamu waliojihifadhi kiasi walizaliwa kutokana na uchafu huo idadi ya watoto ambao hakuna awezaye kuidhibiti isipokuwa Mwenyezi Mungu.
Na yamtosha Yazidi aibu mbaya mno na udhalimu wa kudumu kule kumuuwa Bwana wa vijana wa peponi na kuwateka Mabinti wa Mtume na kuyachokora meno ya Husein (a.s.) kwa kijiti kisha kuimba kwake beti za ushairi ambazo ni maarufu akasema, "Laiti wazee wangu (waliouawa) katika Badri wangeshuhudia..." Mpaka akafikia kusema: "Banu Hashim walichezea Ufalme, hakuna habari yeyote iliyokuja wala Ufunuo ulioshuka."
Ni wazi kabisa kwamba hakuamini utume wa Muhammad (s.a.w.w.) wala Qur'an Tukufu, basi je, ni kweli mnaafiki kumkufurisha anayejitenga na Yazid? Na baba yake Muawiyyah ambaye alikuwa akimlaani Ali (a.s) na huamuru alaaniwe, bali na (alikuwa) akimuuwa kila anayekataa kufanya hivyo miongoni mwa Masahaba wema kama alivyomfanyia Hujr ibn Adiyy Al-Kindi na jamaa zake, na (tendo la kumlaani Ali a.s.) aliliusia likawa ni sunna iliyofuatwa kwa miaka sabini hali ya kuwa (Muawiyyah) anaijua kauli ya Mtume (s.a.w.w.) aliposema "Yeyote atakayemtukana Ali, basi kanitukana mimi, na atakayenitukana mimi amemtukana Mwenyezi Mungu". Kama ambavyo zilivyoandika Sahih za Ahli-Sunnah kwa ziyada ya matendo aliyoyatenda miongoni mwa mambo yanayopingana na Uislamu kwa kuwauwa watu wema wasio na kosa ili achukue kwao kiapo cha utii kwa ajili ya mwanawe Yazid. Vilevile kumuua kwake, Hassani ibn Ali (a.s.) kwa kumtumia Ju'da binti Ash-ath, na maovu mengine mengi yanatajwa na historia kwa Masunni kama ambavyo pia yanashuhudiwa na wafuasi wa Imam Ali (a.s.).
Mim, sikudhani kwamba ninyi mnaafikiana na hayo, vinginevyo basi na tuyaache kama yalivyo, na ikifika hapo basi hapatabakia baada ya hayo kipimo wala akili, wala sheria na wala hekima pia dalili. Na Mwenyezi Mungu anasema: "Enyi mlioamini mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli." (Qur'an, 9:119)
No comments:
Post a Comment