Tuesday, 27 May 2014

Maana ya Ahlu-sunna:

Kuna maana tatu zinazotafsiri kinachokusudiwa kunako neno Ahlu-sunna,na maana hizo zinapatikana katika vitabu vya wanazuoni wa Kisunni. Na zimekuwa maana tatu kutokana na tofauti iliyopo baina yao kuhusiana na uhakika wa Istilahi hii Ahlu-sunna, lini hasa imeenza na ni nani mwanzilishi wa Istilahi hii.Tunazitaja maana hizo za neno Ahku-sunna kama ifuatavyo:

1-Madh-hebu ya Ahlu-sunna maana yake: Ni kundi la watu wa Hasan Al-basri, walioshikamana na "dhahiri ya Nassu" hata kama dhahiri hiyo inakwenda kinyume au inapingana na akili.
Kwa muhtasari: Maana hii inasema hivi:Ahlu-sunna ni kundi lile la waislaam waliokuwa wakiongozwa na Hasan Al-Basri, ambao hukabiliana na Dhahiri ya Nasu (kama vile kushikamana na dhahiri ya  hadithi au Riwaya) pasina kufanya tafsiri wala Taawili, sawa sawa (dhahiri ya Nasu hiyo) iwe inaafikiana na akili au inapingana na kwenda kinyume na akili.

Rejea: Al-firqatun-najia: Juzuu ya 1, Ukurasa wa 405.

2-Madh-hebu ya Ahlu-sunna: Maana yake ni yale madh-hebu aliyoyaasisi Abu Hasan Al-Ash-ari.

3-Madh-hebu ya Ahlu-sunna: Maana yake ni wale waislaam wanaoamini uhalali  na haki ya Ukhalifa wa Abubakari na Umar, na Uthman, na kwamba hao watatu  ukhalifa wao ni halali na ni haki kutangulia ukhalifa wa Imam Ali bin Abi Talib (a.s). Zaidi ya hilo pia huitikadia kuwa: KHERI NA SHARI VYOTE HUTOKA KWA MWENYEEZI MUNGU (S.W).
Hao ndio huitwa Ahlu-sunna.Kwa maana ikiwa wewe si mwenye kuamini au kuitikadia kuwa Khalifa wa kwanza ni Abubakar, na wa pili ni Omar na wa tatu ni Othman na wa nne ni Ali, bali unaamini na kuitikadia kuwa Khalifa wa kwanza ni Imam Ali Bin Abi Talib (a.s) kwa mujibu wa Nasuu (Hadithi) za Mtume (s.a.w.w), basi wewe hutoitwa kuwa ni katika Ahlu-sunna, na pia ukiwa unaamini kuwa Kheri hutoka kwa Mwenyeezi Mungu (s.w) na Shari haitoki kwa Mwenyeezi Mungu (s.w) bali hiyo ni natija au matokeo ya matendo ya watu, basi pia hilo litakufanya usiitwe au usiwe miongoni wa Madh-hebu hii ya Ahlu-sunna maana utakuwa umeenda kinyume na maana kamili ya neno Ahlu-sunna kama ilivyotajwa katika sehemu hii (namba 3). Maana hii namba tatu ndio maana anayoita mwanazuoni maarufu wa kissuni katika kitabu chake, anayeitwa: Abu Zuhra, na kitabu chake kinaitwa: Tarikh Al-madhahibul-Islamiyya. Na hii ndio maana yenye uzito zaidi kuliko maana zile mbili zilizotangulia.

Rejea: Tarikh Al-madhahibul-Islamiyya: Juzuu ya 2;ukurasa wa 58.


No comments:

Post a Comment