Bi Fatumah Zahra (a.s) alifariki miezi mitatu tu baada ya kifo cha baba yake yaani Mtume Mohammad (S.A.W.W) na kuzikwa mahali pasipoeleweka na mpaka leo kaburi lake halijulikani liko wapi. Lakini Sayyidna Abubakar aliyefariki miaka miwili baada ya kifo cha mtume na sayyidna Umari aliyefariki miaka 20 baadaye walizikwa pembeni ya kaburi la Mtume. Kwa nini mabwana hao wawili wazikwe pembeni ya mtume na wala si bint wake wa pekee (bi Fatumah)? Je ni bint huyo mtukufu ndiye aliomba azikwe mbali na baba yake? Kwa nini? Au waislamu ndio waliozuia bint huyo kuzikwa pembeni ya baba yake?
(soma Sahih al Bukhari Arabic - English juzuu la 5 hadith ya 546 kwa majibu ya maswali hayo).
Wednesday, 23 April 2014
HUKUMU YA MAVAZI WAKATI WA SWALA
1. Vazi la mwanamume lazima lisitiri sehemu zake za siri, ikiwa hakuna au kuna mtu mwingine.
2. Ama mwanamke lazima asitiri viongo vyake vyote vya mwili ispokuwa viganja, nyayo za miguu mpaka vifundo vyake na paji la uso linalooshwa wakati wa kutawadha.
3. Kuhusu Vazi la kusalia ni lazima kuzingatia yafuatayo:-
a) Liwe tohara
b) Liwe la halali (si la unyang’anyi)
c) Lisitokane na wanyama haramu kuliwa.
d) Lisitokane na viungo vya mzoga.
e) Mwanaume haruhusiwi kuvaa dhahabu au mavazi yenye nakshi za dhahbu wala nguo zilizotengenezwa kutokana na hariri.
4. Katika Swala hairuhusiwi kubebe vitu vilivyo tokana na wanyama haramu kuliwa, vinginevyo swala itabatilika. Mfano, kuvaa saa au mkanda wa nyama za nyoka.
5. Ikiwa hatambui kuwa mwili wake au nguo zake si tohara na kubaini hivyo baada ya swala, swala yake itakuwa halali.
6. Ikiwa mtu atasahau kwamba mwili wake au nguo zake si tohara na kukumbuka wakati au baada ya sala, itmlazimu kujitoharisha na kusali tena. Ikiwa wakati wa sala uliobainishwa umepita, atalazimu kuitekeleza.
7. Ikiwa mwili au nguo zimekuwa si tohara kwa damu kwa kipimo chini ya dilhamu, Swala yake itakuwa halali.

ASILI YA USHIA
USHIA asili yake ni sawasawa na Uislamu (kwa maana Ushia ni Uislamu na Uislamu ni Ushia). Ushia ulitofautiana na Usunni tokea mwanzo wa Uislamu kuhusiana na Khalifa atakayeuongoza Uislamu baada ya Mtume kufariki dunia. Sunni huamini kwamba Abubakar ndiye aliyekuwa khalifa wa kwanza lakini Shia huamini kuwa Imam Ali ndiye khalifa wa kwanza.
Kama msomi asiyekuwa na chuki atachunguza matangazo ya Mtume kama yalivyoandikwa na wanachuoni wa kisunni katika tafsiri zao za Qur'an, hadith za Mtume, elimurijali na tarekh (Historia), atalazimika kukubali kwamba alikuwa ni Mtume mwenyewe ndiye muanzilishi wa Ushia. Tangazo la kwanza la kubaathiwa liliambatana kwa wakati mmoja na tangazo la ukhalifa wa Imam Ali. Tukio hilo linajulikana kama, “Karamu wa ndugu wa karibu”. Vifungu vinavyohusu karamu hiyo vimenukuliwa hapa kutoka kitabu cha tarekh cha Tabari.
Ali (a.s) alisema, “wakati aya Na uwaonye jamaa zako wa karibu, iliposhukwa kwa Mtume wa Allah, Mtume aliniita mimi na kuniamrisha kuandaa karamu na kuwakaribisha ukoo wa Abdul-Mutalib ili apate kuzungumza nao. Walifika watu takribani 40, miongoni mwao walikuwepo ami zake Mtume yaani Abutalib, Hamza, Abasi na Abu Lahab. Kisha Mtume alitoa hotuba ifuatayo:
Enyi watoto wa Abdul-Mutalib, simjui mtu yeyote katika Bara Arabu yote ambaye amewaletea watu wake kitu kilicho bora zaidi yangu. Nimekuleteeni mema ya hii dunia na akhera. Na Allah (S.W.T) ameniamrisha nikuiteni ninyi kwayo. Ni nani basi miongoni mwenu atakaye nisaidia katika jambo hili, ili awe ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu kwenu?
Ali aliendelea kusema kuwa hakuna hata mtu mmoja aliyejibu, hivyo mimi nilisema, “mimi, ewe Mtume wa Allah, nitakuwa msaidizi wako katika kazi hii. Basi Mtume akaweka mkono wake kwenye shingo yangu na kusema, “Hakika huyu ni ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu miongoni mwenu, msikilizeni na mumtii. Mkutano wote ukaamka huku wakicheka na kumuambia Abu Talib kwamba Muhammad amemuamrisha yeye kumsikiliza mtoto wake na kumtii.
Soma, Tafsiri Tabari, ya Mohammad bin Jariri, Tarekh, Juzuu ya 3 uk. 1882 - 1885

MAONI YA QUR’AN KUHUSU MASAHABA WA MTUME
Assalaam alaykum. Kwanza kabisa ninachukua nafasi hii kuwashukuru Masahaba wa Mtume waliokuwa wema na waliomsaidia katika ujumbe wake bila kuwa na ajenda za siri dhidi ya Uislamu. Bila shaka Qur’an imekuja na aya nyingi kuwasifu Masahaba hawa. Pamoja na kuwa na Masahaba wema, wapo vile vile Masahaba waliokuwa si wema na Qur’an imewalaumu katika aya zifuatazo:
1. Na Mohammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwishapita kabla yake mitume wengi. Je, akifa au akiuawa ndio mtageuka kurudi nyuma (kurtadi)? Na atakayegeuka na kurudi nyuma hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Na Allah atawalipa wanaoshukuru (Qur’an 3:144).
2. Wachache katika waja wangu ndio wenye kushukuru (Qur’an 34:13).
3. Enyi mlioamini mna nini mnapoambiwa: Nendeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia ni chache kuliko za akhera. Kama hamuendi atakuadhibuni adhabu chungu na atawaleta watu wengine wala ninyi hamtamdhuru chochote, na Allah ni Muweza wa kila kitu (Qur’an 9:38-39).
4. Na mkirudi nyuma, (Allah) atabadilisha (alete) watu wengine wasiokuwa ninyi kisha hawatakuwa kama ninyi (Qur’an 47:38).
5. Je, haujafika wakati kwa wale walioamini, nyoyo zao zinyenyekee kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kwa mambo ya haki yaliyotelemka, na wala wasiwe kama wale waliopewa kitabu hapo kabla na muda wao (wa kuondokewa na Mitume) ukawa mrefu, kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu na wengi wao wakawa waasi (57:16).
6. Na wawepo miongoni mwenu watu wanaolingania wema na kukataza maovu, na hao ndio watakaotengenekewa. Na wala msiwe kama wale waliofarikiana na kukhitilafiana baada ya kuwafikia dalili zilizo wazi, na hao ndio watakao kuwa na adhabu kubwa. Siku ambayo nyuso zitanawiri na nyuso zingine zitasawajika, wataambiwa: je mlikufuru baada ya kuamini kwenu? Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyokuwa mnakufuru. Ama wale ambao nyuso zao zitanawiri watakuwa katika rehema ya Allah. Wao humo watakaa milele (Qur’an 3: 104-106)
Ndani ya kitabu kiitwacho Ad-Durul Manthur cha Jalaludin As-Suyut imeandikwa: Pindi Masahaba walipofika Madina, wakapata maisha mazuri ambayo hawakuwa nayo kabla, wakazembea kutenda baadhi ya wajibu waliokuwa juu yao, hivyo wakakemewa kwa aya ya 5 iliyotangulia hapo juu.
Na katika riwaya nyingine itokanayo na Mtume Mohammad inasema kuwa Allah aliziona nyoyo za Muhajirina kuwa ni nzito (hata) baada ya miaka 17 ya tangu kushuka Qur’an, basi akateremsha kauli yake, “Je haujafika wakati kwa wale walioamini?
Aya hizi zinaonesha wazi kuwa kuna masahaba ambao hawakuwa wanyenyekevu mbele za Mwenyezi Mungu na Mtume wake, vinginevyo Mwenyezi Mungu asingewalaumu au kuwashauri wabadirike tabia zao.
Ama suala la Masahaba kukhitilafiana sidhani kama kuna mtu anaweza kupinga na kudai kuwa hawakukhitilafiana kwani walifikia mahala pa kupigana vita wao kwa wao. Mfano Sayyidina Uthuman aliuwawa na kundi la Masahaba. Imam Ally (a.s) akiwa na alipigana vita na kundi la Masahaba kama Aysha, Zuberi na Twalha. Vile vile alipigana vita na Muawiyyah bin Abusufian ambaye naye alikuwa sahaba wa Mtume.
Haiwezekani kwa makundi haya yenye kupigana kwamba yatakuwa yote katika haki. Hivyo kuna ulazima wa kutafuta haki iko wapi kabla ya kuliunga mkono kundi lolote miongoni mwa haya.
Kumbuka Mtume anasema pale watapokhitilafiana watu, tafadhali shikamaneni na Imam Ally kwani haki iko pamoja naye daima. Kwa mantiki hii kundi linalomfanya Imam Ally kuwa kiongozi wao wa kwanza baada ya Mtume kufariki tu huenda litakuwa katika njia sahihi zaidi. Kwani muda mfupi baada ya Mtume kufa ndio vurugu zilipoanza. Utakumbuka Sayyidna Umar alipotangaza kuwa Mtume hajafa hadi wakafiri waishe na kwamba atakayesema kuwa Mtume kafa atamkata kichwa. Hii sio imani ya kiislamu na khitilafu zilianzia hapa.

MASAHABA NA MSIBA WA ALKHAMISI
Ibn Abas anasema kuwa, “Siku ya Alhamis, hiyo siku ya Alhamis ilikuwa na tukio gani? Mtume wa Mwenyezi Mungu yalimzidia maumivu yake akasema, njooni nikuandikieni maandiko ambayo hamtapotea baada yake. Umar bin Khatab akasema Mtume anaweweseka kwa kuzidiwa na maradhi, nanyi mnayo Qur’an, Kinatutosha kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi hapo watu waliokuwepo ndani ya nyumba ya Mtume wakakhitilafiana na kuzozana juu ya kuandikiwa wosia. Wapo waliotaka wasogee ili Mtume awaandikie wosia na wapo waliopinga na kusema kama alivyosema Omar bin Khatab kuwa Qur’an inawatosha. Masahaba walipozidisha zogo Mtume akawafukuza”.
Ibn Abas anasema, huu ndio msiba mkubwa kuliko yote katika Uislamu kwani Masahaba walimzuia Mtume wao kuandika wosia.
Soma: Sahihi Muslim, Juz. 5 uk. 75 mwishoni wa kitabul-wasiyyah.
Mpaka hapa nashangazwa na msimamo wa Umar bin Khatab dhidi ya amri ya Mtume Mohammad (S.A.W) juu ya kuulinda umma usipotee na bila shaka maandishi hayo yangesaidia kuondoa khitilafu baina ya waislamu.
Hivi Omar anaposema kuwa ninyi mnayo Qur’an, nayo inatutosha anamaana gani? Je, Omar anafahamu Qur’an zaidi ya Mtume Mohammad (S.A.W.W)? Hili haliwekani bali tabia ya Omar ni kumpinga Mtume kwa kila maagizo ayatoayo kwa waislamu. Nadhani unakumbuka msimamo wa Masahaba katika sulhu ya Hudaibiyyah ambapo Omar aliongoza uasi dhidi ya Mtume wetu kwa mara nyingine.
Lakini kama kweli walifahamu kuwa Mtume anaweweseka, kwa nini alipowafukuza chumbani walitoka? Hii inamaana kuwa waligoma kumruhusu Mtume kuandika wosia kwa sababu walijua Mtume alitaka kuandika nini na hivyo wakaona wamzue kuandika ili wafanye wanavyotaka pindi atakapofariki dunia.
Matendo haya ya Omar bin Khatab yanapingana na Qur’an 49:2 isemayo, “Enyi mlioamini msipaze sauti zenu juu ya sauti ya Mtume na wala msisemezane naye kwa sauti ya nguvu kama mnavyosemezana ninyi kwa ninyi, visije vitendo vyenu vikakosa thawabu na hali ya kuwa hamtambui”.
Katika tukio hili walivuka mipaka ya kupaza sauti na kumsemesha kwa nguvu hadi wakamtuhumu Mtume kwa kuweweseka. Waislamu nakuombeni mjitenge mbali na watu walioongoza fitina ndani ya Uislamu na kumdhulumu Mtume wetu kwa kumzuia kuuongoza Uislamu kwa misingi aliyoagizwa na Mola wake. Pia jitengeni na watu wanaoongoza kwa kutenganisha watu kwa kuwasingizia waislamu wengine kuwa ni makafiri ili wapate sababu ya kuwaua.

HADITH YA MTUME KUHUSU MGAWANYIKO WA WAISLAM
Mtume wa Allah alisema, “Wana wa Israel walifarakana na kuwa makundi 71, Manaswara nao wamefarakana na kuwa makundi 72, na umati wangu utafarakana na kufikia makundi 73 na yote yataingia motoni, isipokuwa kundi moja tu.” Ebu niambieni kundi hilo enyi watu wenye akili.
Mimi nashangaa kuona waislamu wote na makundi yao wanaifahamu hadith hii lakini hawaifanyii kazi kwa kufanya utafiti na kubaini ni kundi gani lenye kuokoka na kuachana na makundi mengine yenye kupotoka.
Cha ajabu ni kuwa kila kundi linadai kuwa ndilo lenye kuokoka bila kuleta ushahidi uliosahihi.
Tafadhali tufanye utafiti ili tubaini kundi hili lenye kuokoka ili tujiunge nalo, vinginevyo tutaangamia. Mwenyezi Mungu anasema, “Na wale wanaojitahidi kwa ajili yetu, tutawaongoza kwenye njia zetu” Qur’an 29:69.
Na amesema tena, “Wale ambao husikiliza kauli (zisemwazo) wakafuata zile zilizo njema, hao ndio aliowaongoa Mwenyezi Mungu na hao ndio wenye akili”.
Bila shaka amesema kweli Mjumbe wa Mwenyezi Mungu pale aliposema kuwa fanya utafiti kuhusu dini yako mpaka isemwe kuwa wewe ni maj-nun.

NAMNA YA KUMSALIA MTUME MOHAMMAD (S.A.W.W)
Qur'an, 33:52 inasema, “Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Mtume, Enyi mlioamini msalieni na mpeni salamu bila kusita.”Wanazuoni wote yaani Sunni na Shia wameafikiana kwamba masahaba walikwenda kwa Mtume na kumuuliza, “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, sisi tumekwisha fahamu namna ya kukusalimia lakini hatufahamu ni namna gani tutakusalia?”Mtume akasema, “Semeni Allahumma swali alaa Mohammad wa aali Mohammad kamaa swalaita 'alaa Ibrahim wa aali Ibrahim fil'alamina, innaka hamidun majiid, yaani Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu Mohammad na aali zake Mohammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali zake Ibrahim katika walimwengu, hakika wewe ni mwenye sifa njema tena Mtukufu; na wala msinisalie sala iliyo katika.”
Masahaba wakauliza ni ipi sala iliyokatika ewe Mjumbe wa Allah?
Mtume akajibu, “sala iliyokatika ni kusema ewe Mwenyezi Mungu msalie Mohammad na kisha mkanyamaza, na fahamuni kuwa Mwenyezi Mungu ni mkamilifu, hakubali ila kitu kilichokamilika.
Kutokana na hili Imam Shafii anasema, “Enyi kizazi cha nyumba (Ahlulbayt) ya Mtume wa Mwenyezi Mungu mapenzi kwenu ni faradhi (wajibu) kutoka kwa Allah, ameyateremsha ndani ya Qur'an, yakutosheni ninyi heshima tukufu ya kwamba yeyote asiyekusalieni hana sala (sala yake ni batili).

UISLAM UMEHIMIZA USAWA WA BINADAMU
Mtume wetu (s.a.w.w.) amesema: “Waarabu wasijigambe kwamba wao ni bora kwa wasio Waarabu na kinyume chake; na weupe wasijigambe kwa ubora kwa weusi na kinyume chake. Ubora uko tu katika elimu na ucha Mungu.
Katika Qur’ani
Tukufu Allah (swt) anasema: “Enyi watu! Hakika tumekuumbeni ninyi mume na mke; na tumekufanyeni mataifa na makabila ili kwamba mpate kujuana; hakika aliye mbora sana miongoni mwenu mbele ya Allah ni yule amchae Allah zaidi…” (49:13).

BARUA YA WAZI
KWA MWANACHUONI WA INDIA, SAYYID ABUL-HASAN AN-NADAWI
Amani ya Mwenyezi Mungu ikushukieni na Rehema na Baraka zake
zikushukieni.
Amma Ba'ad:
Mimi Muhammad At-Tijani As-Samawi, Mtunisia, ambaye Mwenyezi Mungu
amenineemesha kwa uongofu na mafanikio, nayakubali Madh-hebu ya watu wa nyumba
ya Mtume baada ya uchunguzi (uliochukua muda) mrefu na kabla ya hapo nilikuwa
(mfuasi wa Madh-hebu ya) Malik. Si hivyo tu, bali nilikuwa miongoni mwa wafuasi
wa Tariqa mashuhuri ya Kisufi huko Afrika ya Kaskazini iitwayo "AT-TIJANIYYAH".
Hatimaye nikaufahamu ukweli wakati wa safari yangu iliyofana kwenda kwa
Wanachuoni wa Kishia, na niliandika kuhusiana na safari hiyo kitabu
nilichokiita, "THUMMAH-TADAITU", kilikamilika kuchapishwa huko kwenu
India kwa lugha nyingi kutokana na ukarimu wa Majimau Al-ilmiyyi Al islamiyyi,
na kwa ajili ya munasaba (huu) niliitwa kuitembelea India.
Ewe Bwana wangu mpendwa, nilifika India kwa matembezi mafupi, na matarajio
yangu yalikuwa ni kukutana nanyi kutokana na sifa zenu ninazozisikia na
kutokana na kufahamu kwangu kwamba ninyi ndio mategemeo kwa AH-LISSUNNAT
WAL-JAMA'A. Lakini nilishindwa kufanya hivyo kutokana na umbali na kukosa muda,
na nikatosheka kwa kuzuru Bombay,
Puna, Jabal Pur na miji mingine iliyoko Gujarat.
Nilihuzunika sana kutokana na mambo niliyoyaona huko India (hasa) kutokana na uadui na bughudha
iliyoko baina ya Ahli-Sunnah Wal-Jama'a, na ndugu zao Waislamu wa Kishia. Kwa
hakika nilikuwa nikisikia kwamba wao hupigana na hupata wakati mwingine
wakauana na kumwaga damu za watu wasio na kosa lolote kutoka pande mbili hizi
eti kwa niaba ya (kutetea) Uislamu.
Mimi nilikuwa siamini (haya) huku nikiitakidi kuwa habari hizo
zimepewa mno sura isiyo yake, lakini niliyoyaona na kuyasikia wakati wa ziyara
yangu kwa kweli yanashangaza na nimeyakinisha kwamba huko kuna makusudio mabaya
na ushauri wa hatari unaoundwa dhidi ya Uislamu na Waislamu ili kuwamaliza wote
Masunni na Mashia. Miongoni mwa mambo yaliyozidisha uwazi wa yakini yangu na
kuimarisha ufahamu wangu (juu ya hayo) ni ule mkabala uliopita baina yangu na
kundi la wanachuoni wa Kisunni wakiongozwa na Sheikh Azizur -Rahman Mufti wa
Al-Jamaatul-Islamiyyah, na mkutano wetu ulikuwa ndani ya Msikiti wao huko Bombay
na wao ndiyo walioniita.
Baada tu ya kufika, dharau, tuhuma na matusi na kuwalaani Mashia
(Wafuasi) wa kizazi cha nyumba ya Mtume vilianza, na walikuwa wamekusudia
kunitisha na kuniudhi kwa kuwa walikuwa wanajua kwamba mimi nimeandika kitabu
kinachotoa wito wa kushikamana na Madh-hebu ya Ahlul-Bait (a.s.). Lakini mimi
nilifahamu makusudio yao na nikaimiliki nafsi yangu na
nilitabasamu hali ya kuwa nikisema: "Mimi ni mgeni kwenu ninyi, nanyi
ndiyo mlioniita na nimekuja kwa haraka kuitika wito, basi je mumeniita ili
mnitukane na kunishutumu, na Je, hii ndiyo tabia ambayo Uislamu
umekufundisheni.
Basi walinijibu kwa kujiamini
kabisa kwamba, mimi hata siku moja sijapata kuwa Muislamu kwa sababu mimi ni
Shia na Mashia hawana Uislamu wowote, na waliapa kuthibitisha jambo hilo.
Mimi nilisema, "Mcheni Mwenyezi Mungu enyi ndugu zangu, Mola
wetu ni mmoja na Mtume wetu ni mmoja na Kitabu chetu ni kimoja na Qibla chetu
ni kimoja, na Mashia wanampwekesha Mwenyezi Mungu na wanautumikia Uislamu kwa
kumfuata Mtume na Watu wa nyumba yake, wanasali Sala (Tano) wanatoa zaka na
wanahiji kwenye nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, basi vipi inajuzu kwenu ninyi
kuwakufurisha wao?
Walinijibu, "Ninyi Hamuamini Qur'ani, ninyi ni WANAFIKI
mnatumia TAQIYYAH, na Imam wenu amesema: "Taqiyyah ni Dini yangu na ni
Dini ya wazazi wangu" Nanyi ni kikundi cha Kiyahudi alichokianzisha
Abdallah ibn Saba'a Myahudi."
Niliwaambia hali ya kuwa nikitabasamu, "Hebu tuwaache Mashia
na zungumzeni nami binafsi, kwani mimi nilikuwa (wa Madhehebu ya) Malik kama
ninyi, na baada ya uchunguzi wa muda mrefu niliyakinisha kwamba Watu wa nyumba
ya Mtume ndiyo wenye haki na ndiyo bora kuwafuata. Basi Je, mnayo hoja ya
kunijadili au kuniuliza ni ipi dalili yangu na hoja yangu ili pengine tuweze
kuelewana miongoni mwetu?"
Walisema: "Ahlul-Bait (Watu wa Nyumba ya Mtume) ni wakeze
Mtume na wewe huna ukijuacho ndani ya Qur'ani." Nikasema: "Bila shaka
Sahih Bukhar na Sahih Muslim zinafundisha kinyume cha mlivyotaja!
Wakasema: "Yote yaliyomo ndani ya Bukhari na Muslim na vitabu
vingine vya Kisunni miongoni mwa hoja mnazozitoa ni katika uzushi wa Mashia
waliouweka vitabuni kwetu."
Niliwajibu hali ya kuwa nacheka; "Ikiwa Mashia wamefikia
kiasi cha kuingiza uzushi ndani ya vitabu vyenu, basi vitabu hivyo havina maana
tena na pia Madhehebu yenu ambayo yamesimama juu ya vitabu hivyo!!"
Walinyamaza wakakosa hoja, lakini mmoja wao alikusudia kuleta fujo
na chuki kwa mara nyingine akasema: "Ye yote asiyeamini Ukhalifa wa
Makhalifa waongofu (ambao ni) Sayyidina Abu Bakri, Sayyidna Umar na Sayyidna
Uthman, Sayyidna Ali, Sayyidina Muawiyyah na Sayyidna Yazid (r.a.) basi huyo
siyo Muislamu.
Nilishangaa kwa maneno haya ambayo sijasikia mfano wake maishani
mwangu nayo ni kumkufurisha asiyeamini Ukhalifa wa Muawiyyah na Yazid, na nilisema
kimoyo moyo: "Ni jambo linaloingia akilini Waislamu kumuombea radhi
Abubakar, Omar na Uthman jambo hili limezoeleka, ama kumuombea radhi Yazid
kabisa sijasikia (popote) isipokuwa India na niliwageukia nikawauliza: "Je
mnakubaliana na huyu juu ya maoni yake?
Wote kwa pamoja wakajibu "Ndiyo".
Hapo ndipo nilipofahamu ya kuwa hakuna faida ya kuendeleza
mazungumzo, na nikafahamu pia kwamba hakuna kingine isipokuwa wanataka kuniudhi
(nikasirike) ili wapate kunishambulia na pengine waniuwe kwa madai ya kuwatukana
Masahaba, nani ajuaye (nia zao)?
Niliona machoni mwao (ishara ya) shari, nikamuomba rafiki yangu
aliyenileta kwao anitoe haraka, akanitoa huku akisikitika na kunitaka radhi kwa
yaliyotokea. Mtu huyu hakuwa na kosa alikuwa akifuatilia mkutano huo kwa kutaka
kufahamu ukweli, ni kijana
mwenye heshima (akiitwa) Sharafud-Din ambaye anamiliki
Maktaba na Kiwanda cha uchapishaji cha Kiislamu mjini Bombay. Basi yeye ni shahidi wa yote
yaliyopita baina yetu katika majadiliano yaliyotajwa, na hakuficha kutoridhika
kwake na watu hawa ambao yeye alikuwa akiamini kwamba wao ni miongoni mwa
Wanachuoni wakubwa.
Niliwaacha hali ya kuwa nimechukia na kusikitika juu ya hali
ambayo imewafikia Waislamu na hasa wale wanaosimamia vituo vya uongozi na
kujiita kuwa ni Wanachuoni, na nilisema moyoni kuwa, ikiwa hali ya Wanachuoni
iko kwenye kiwango hiki cha ung'ang'anizi wa upofu, basi hali itakuwaje kwa
watu wa kawaida na wale wasiojua kitu?
Hapo ndipo nilipofahamu ni vipi yamekuwa yakizuka mapambano na
vita ambavyo ndani yake damu iliyoharamishwa humwagwa na kuvunja heshima na
utukufu (wa watu) kwa jina la kuutetea Uislamu, na nililia juu ya hatima ya
umma huu uliogawanyika na kuangamia, umma ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu
ameubebesha jukumu la uongofu na Mtume wa Mwenyezi Mungu vile vile ameubebesha
jukumu la kuifikisha nuru kwenye nyoyo zenye kiza zinazohitaji kupata nuru
inayong'ara na kwa wakati huo huo katika India peke yake kuna watu wapatao
milioni mia saba wanaabudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na wanamtukuza
Ng'ombe na Masanamu. Badala ya juhudi za Waislamu kuunganika ili wawaongowe na
kuwaongoza na kuwatoa kwenye kiza watu hao na kuwapeleka kwenye nuru ili
wasilimu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mola wa Walimwengu, tunawaona Waislamu leo
hii hasa India wao ndiyo wenye haja ya uongofu na kujisahihisha.
Kwa sababu hii wewe Bwana wangu (Sayyid Abul-Hasan An-Nadawi)
ninaleta kwenu barua yangu nikikulinganieni kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi
wa Rehma Mwenye kurehemu na kwa jina la Mtume wake Mtukufu na kwa jina la Uislamu Mtukufu na kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu (Aliposema)
"Shikamaneni katika Dini ya Mwenyezi Mungu na wala msifarakane."
(Qur'an 3:103)
Nakulinganieni msimame
msimamo wa Muislamu shujaa ambaye haogopi kutekeleza la Mwenyezi Mungu na (haogopi)
lawama ya mwenye kulaumu na wala ubinafsi haumchukui wala vikundi (havimchukui)
kumpeleka namna apendavyo shetani na wafuasi wake.
Nakulinganieni msimame msimamo safi ulio wazi, kwani ninyi ni miongoni mwa
wale ambao Mwenyezi Mungu amewabebesha jukumu (la uongozi) muda wote mtakaokuwa
mkizungumza kwa niyaba ya Uislamu katika nchi hiyo. Mwenyezi Mungu
hatakuridhieni iwapo mtasimama msimamo wa mtazamaji mwenye kuridhika na yale
yanayotokea huku na huko miongoni mwa misiba inayosababisha kupoteza (maisha ya
watu) wasio na makosa miongoni mwa Waislamu wa Kisunni na Kishia. Mwenyezi
Mungu atakuulizeni siku ya Qiyama kwa kila dogo na kubwa, na atakuhesabuni
kutokana na kila linalopita na linalokuja kwa kuwa Hawawi sawa wale wanaojua na
wale wasiojua, kwani kwa kiwango cha bidii mtu afanyacho ndivyo yatavyokuwa
mafanikio, na kwa kadiri ya kiwango cha utukufu ndivyo yajavyo mambo matukufu.
Na maadam ninyi ndiyo mnaowaongoza wanachuoni wa India, basi jukumu lenu ni
kubwa na bila shaka neno litokalo kwenu huenda ndani yake kukawa na mafanikio
kwa umma (wa Kiislamu) nchini India kama ambavyo huenda kukawa na maangamivu ya
mali na watu (likitumika vibaya), basi mcheni Mwenyezi Mungu enyi watu wenye
akili! Na kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewapa Wanachuoni daraja ya kwanza baada ya
Malaika akasema: "Mwenyezi Mungu ameshuhudia ya kwamba, hapana aabudiwaye
kwa haki ila yeye tu na Malaika na wenye elimu (wameshuhudia hivyo), (Yeye) ni
Mwenye kusimamia uadilifu." (Qur'an, 3:18).
Na ikiwa Mwenyezi Mungu anatuamuru sote kwa kusema: "Na
pimeni kipimo kwa haki na wala msipunguze kipimo". (Qur'an, 55:9).
Iwapo wafasiri wanaona umuhimu wa kufanya uadilifu katika vipimo
vya kimaadda ambavyo vina viwango maalum, basi mwaonaje hali ya kufanya
uadilifu katika mambo ya kiitikadi, ambayo yanamvutano baina ya haki na batili
na kwa mambo hayo ya kiitikadi ndipo mahala unapotegemea uongofu wa watu na
uokovu wa watu wote?
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema; "Na mtakapohukumu basi
hukumuni kwa uadilifu". Na amesema tena; "Ewe Daud bila shaka sisi tumekufanya
uwe Khalifa (msimamizi) katika nchi, basi hukumu baina ya watu kwa haki na wala
usifuate matamanio yatakupotosha kutoka njia ya Mwenyezi Mungu."
Hapana shaka Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "Sema kweli
japokuwa ni dhidi ya nafsi yako, sema kweli japokuwa ni chungu."
Ewe Bwana wangu Mtukufu, nakuiteni kwenye Kitabu cha Mwenyezi
Mungu, na sunna ya Mtume wake, semeni kweli wazi wazi kwa sauti kubwa japokuwa
ni chungu itakushuhudieni mbele ya Mwenyezi Mungu.
Naapa kwa Mola wako hivi kwenu ninyi Mashia siyo Waislamu? Hivi
kweli mnaitakidi kwamba wao ni makafiri? Je wafuasi wa Watu wa nyumba ya Mtume
ambao wanampwekesha Mwenyezi Mungu na kumtukuza zaidi kuliko vikundi vyote kwa
usemi wao wa kuwa hafanani na chochote kwa kumtakasa kutokana na kufanana, na
kutokana na kuwa hana umbo na mwili. Si hivyo tu bali wanamuamini Mtume wake
Muhammad (s.a.w.w.) na wanamuheshimu mno kuliko vikundi vyote wasemapo kuwa,
"Yeye Mtume ni Maasum moja kwa moja hata kabla ya kupewa utume". Je,
hawa ndiyo munaowahukumu kuwa ni makafiri?
Je, wale wanaomtawalisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale
walioamini na wanawapenda kizazi cha Mtume na kuwatawalisha kama alivyowatambulisha
Ibn Mandhur ndani ya "Lisanul-A'rab" katika mada ya Shia, basi je
ninyi mwasema kwamba wao siyo Waislamu?
Je, Mashia hawa ambao wanatekeleza wajibu wa Sala kwa namna iliyo
bora, na wanatoa Zaka na kuzidisha juu yake Khumsi ya mali zao kwa ajili ya
kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wanafunga (saumu ya) mwezi wa Ramadhani
na nyingine na wanahiji nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu na kuyatukuza mambo
matukufu ya Mwenyezi Mungu, kadhalika wanawaheshimu Mawalii wa Mwenyezi Mungu
na kujiepusha na maadui wa Uislamu, hivyo kwenu ninyi watu hawa ni washirikina?
Je, hivi watu wasemao kuwa Uimamu hasa ni (haki) wa Maimamu kumi
na wawili kutoka katika watu wa nyumba ya Mtume ambao Mwenyezi Mungu
amewaondolea uchafu na amewatakasa sana sana, na Mtume wa Mwenyezi Mungu
aliwataja kama alivyotoa Bukhari na Muslim na wengineo katika Sahihi za
Ahlu-Sunnah, hivi watu hawa kwenu ninyi ni watu waliotoka nje ya Uislamu?
Je hivi kuna siku ambayo Waislamu wamekuwa hawautambui Uimamu na
wala hawakubali sawa sawa liwe hilo katika uhai wa Mtume au baada ya kufa
kwake mpaka kufikie kuihusisha nadharia ya Uimamu kwa Waajemi na Majusi?
Na je hivi mnasema kwa kujiamini kuwa, "Ni Kafiri asiyekubali
Uimamu wa Yazidi ibn Muawiyyah ambaye uovu wake unaeleweka kwa Waislamu wote?
Na itoshe uovu na udhalimu wa Yazidi kwa maelezo walioafikiana Waislamu wote
kutokana na yeye kuruhusu kufanyika maasi kwenye mji Mtakatifu wa Madina kwa
kutumia jeshi lake na askari wake kufanya wayatakayo mjini humo ili wachukuwe
viapo vya utii (kutoka kwa watu) kwa nguvu kama kwamba (watu hao) ni watumwa
wake. Si hivyo tu, bali wa Yazid waliwaua maelfu ya Masahaba watukufu na
Tabiina, wakavunja heshima za wanawake na wasichana wa Kiislamu waliojihifadhi
kiasi walizaliwa kutokana na uchafu huo idadi ya watoto ambao hakuna awezaye
kuidhibiti isipokuwa Mwenyezi Mungu.
Na yamtosha Yazidi aibu mbaya mno
na udhalim wa kudumu kule kumuuwa Bwana wa vijana wa peponi na kuwateka Mabinti
wa Mtume na kuyachokora meno ya Husein (a.s.) kwa kijiti kisha kuimba kwake
beti za ushauri ambazo ni maarufu akasema, "Laiti wazee wangu (waliouawa)
katika Badri wangeshuhudia..." Mpaka akafikia kusema: "Banu Hashim
walichezea Ufalme, hakuna habari yeyote iliyokuja wala Ufunuo ulioshuka."
Ni wazi kabisa kwamba hakuamini utume wa Muhammad (s.a.w.w.) wala
Qur'an Tukufu, basi je, ni kweli mnaafiki kumkufurisha anayejitenga na Yazid?
Na baba yake Muawiyyah ambaye alikuwa akimlaani Ali (a.s) na huamuru alaaniwe,
bali na (alikuwa) akimuuwa kila anayekataa kufanya hivyo miongoni mwa Masahaba
wema kama alivyomfanyia Hujr ibn Adiyy Al-Kindi na jamaa zake, na (tendo la
kumlaani Ali a.s.) aliliusia likawa ni sunna iliyofuatwa kwa miaka sabini hali
ya kuwa (Muawiyyah) anaijua kauli ya Mtume (s.a.w.w.) aliposema "Yeyote
atakayemtukana Ali, basi kanitukana mimi, na atakayenitukana mimi amemtukana
Mwenyezi Mungu". Kama ambavyo zilivyoandika Sahih za Ahli-Sunnah
kwa ziyada ya matendo aliyoyatenda miongoni mwa mambo yanayopingana na Uislamu
kwa kuwauwa watu wema wasio na kosa ili achukue kwao kiapo cha utii kwa ajili
ya mwanawe Yazid. Vilevile kumuua kwake, Hassani ibn Ali (a.s.) kwa kumtumia
Ju'da binti Ash-ath, na maovu mengine mengi yanatajwa na historia kwa Masunni
kama ambavyo pia yanashuhudiwa na wafuasi wa Imam Ali (a.s.).
Mimi, ewe Bwana wangu, sikudhani kwamba ninyi mnaafikiana na hayo,
vinginevyo basi na tuyaache kama yalivyo, na ikifika hapo basi
hapatabakia baada ya hayo kipimo wala akili, wala sheria na wala hekima pia
dalili. Na Mwenyezi Mungu anasema: "Enyi mlioamini mcheni Mwenyezi Mungu
na kuweni pamoja na wakweli." (Qur'an, 9:119)
Namuapa Mwenyezi Mungu, bila shaka mwanachuoni wa Kipakistan Abul-A'ala Al-Maududi, Mwenyezi Mungu amrehemu amesema kweli alipotaja katika kitabu chake kiitwacho, "Ukhalifa na lifetime" katika ukurasa wa 106 akimnukuu Al-Hasan Al-Basri aliposema, "Mambo manne alikuwa nayo Muawiyyah, lau angekuwa na jambo moja miongoni mwa hayo lingetosha kumuangamiza.
1) Kuchukua ukhalifa bila ya mashauriano ya Waislamu
na hali wamo miongoni mwao waliobakia Masahaba na wenye nuru ya ubora.
2) Kumpa Ukhalifa baada yake mwanawe mlevi ambaye alikuwa
akivaa hariri na kupiga magitaa.
3) Kumfanya Ibn Ziyad kuwa ni mwana wa baba yake na hali Mtume
(s.a.w.) amesema "Mtoto ni wa kitanda na mzinifu mwanaume atapata
jiwe."
4) Kumuua kwake Hujr na Jamaa za Hujr, basi ole wake kwa kumuua
Hujr na jamaa zake Hujr (akakariri mara tatu).
Basi Mwenyezi Mungu amrehemu Abu A'ala Al-Maududi, aliyepasua
ukweli, na lau angetaka angeongeza zaidi ya mambo haya manne yakawa mambo
arobaini lakini aliona kwamba hayo yanatosheleza kumuangamiza Muawiyyah.
Huenda Maududi alikuwa akichelea hisia za watu ambao wamejifunza
kwa watangulizi wao kumtukuza Muawiyya, kumuheshimu na kumuombea radhi, bali
hata mwanawe Yazid vile vile (kutukuzwa n.k.) kama nilivyosikia mimi mwenyewe
binafsi toka kwa Wanachuoni wenu huko India.
Lahaula wala Quwwata Illa Billahil-l-'Aliyyil-Adhim.
Kutokana na yote hayo mimi pia nilichelea hisia za wale watu
walioniita wasije wakanivamia, basi sikuwatajia chochote katika matukio hayo.
Kwa hiyo ewe bwana wangu, ninakulinganieni muwe na msimamo ulio
wazi mkitafuta radhi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa msimamo huo, kwani Mwenyezi
Mungu haichelei haki, na wala sikutakeni mkiri makosa ya watu hawa wala
kuisambaza aibu yao kwa kuwa historia inatutosheleza sisi
na ninyi kutuhadharisha juu ya hayo.
Lakini kinachotakiwa kutoka kwenu ni kukiri na muwafahamishe
wafuasi wenu kwamba, "Watu ambao hawaukubali Uimamu wa watu hawa (Muawiyya
Yazid, Abubakr, Omar na Uthman) na wala hawawatawalishi, wao ni Waislamu
wanaostahiki heshima na jambo hilo halina shaka, museme ya kwamba Mashia ni
wenye kudhulumiwa siku zote kwani wao hawakuufuata na kuukubali Uimamu wa mti
uliolaaniwa ambao Mwenyezi Mungu ameupigia mfano ndani ya Qur'ani.
Basi ni lipi kosa la Mashia kwa Mola wenu, ikiwa Mtume (s.a.w.)
anawaamuru Waislamu kuwafuata Watu wa nyumba yake baada yake, mpaka akawafanya
wao kuwa ni kama Safina ya Nuh, anaokoka mwenye kupanda
ndani yake na anaangamia anayeikwepa.
Na ni lipi kosa la Mashia ikiwa walitekeleza amri ya Mtume
aliposema: "Nimekuachieni vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na
Kizazi changu, vitu ambavyo mkishikamana navyo kamwe hamtapotea baada
yangu." Kama ambavyo zinashuhudia Sihah za Sunni
ukiachilia mbali vitabu vya Kishia.
Badala ya kuwashukuru (Mashia) na kuwatanguliza na kuwaboresha juu
ya wengine kwa kufuata kwao maamrisho ya Mtume (s.a.w.w.), tunawashutumu na
kuwakufurisha na kujitenga nao, jambo hili siyo uadilifu wala haliingii
akilini.
Ewe Bwana wangu, hebu tuachane na kauli za kijinga na za uongo
ambazo haziwezi kusimamisha dalili wala hoja na hazina uzito kwa wanataaluma
miongoni mwa watoto wa umma wetu kwamba, "Eti Mashia wanayo Qur'ani yao, au eti wao wanasema kwamba
aliyepewa Utume ni Ali, au kwamba Abdallah ibn Sabaa' Myahudi ndiye muanzilishi
wa Ushia."Na mengineyo miongoni mwa kauli dhaifu ambazo Mwenyezi Mungu
anashuhudia kuwa hayo ni miongoni mwa uzushi wa maadui wa Uislamu na maadui wa
Ahlul-Bait na wafuasi wao. Na hayo ni mambo hayakuzushwa isipokuwa ni kutokana
na ubinafsi mpotovu na ujinga wenye kero iliyopita kipimo.
Ewe Bwana wangu mpendwa mimi nauliza, "Wana daraja iliyoje
wanachuoni wa India kuliko ile ya wanachuoni wa Az-Har
Tukufu waliotoa Fat-wa inayoruhusu kufanya Ibada kwa mujibu wa Madhehebu ya
Shia Imamiyyah tangu miaka thelathini iliyopita? Na miongoni mwa Wanachuoni wa
Az-Har kuna aonaye kuwa fiqihi ya Mashia ya Jaa'fari ambayo wanaitumia Mashia
ni pana yenye manufaa na iko karibu mno na Roho ya Uislamu kuliko Madhehebu
nyinginezo ambazo zinaitegemea. Na anayewaongoza Wanachuoni hawa (kwa fikra
hii) ni Mtukufu Marehemu Sheikh Mahmud Shal-Tut Mwenyezi Mungu amrehemu, ambaye
aliiongoza Az-har katika uhai wake.
Je hivi wanachuoni kama hawa hawaujui Uislamu na Waislamu? Au
wanachuoni wa India ni wajuzi mno kuliko wanachuoni hao?
Mimi siwadhanieni kabisa kwamba ninyi mnasema namna hiyo...!!
Ewe Bwana wangu Mtukufu, mategemeo yangu kwenu ni thabiti na moyo
wangu kwenu uko wazi kwa mapenzi na huruma, na hapo zamani nilikuwa kama ninyi
nimefunikwa sioni haki wala Ahlul-Bait (a.s.) na wafuasi wao. Mwenyezi Mungu
akaniongoza kuelekea kwenye haki ambayo hapana baada yake ila upotovu, na
nikawa huru kutokana na minyororo ya ung'ang'anizi na kufuata kama kipofu, na
nilifahamu kwamba wengi wa Waislamu bado wamefunikwa na habari zisizo na ukweli
na za uzushi. Kampeni zilizoandaliwa kuwapa baadhi ya watu utukufu wasiostahili
zinawazuwia (Waislamu) kuufikia ukweli ili wote wapate kupanda meli ya uokovu
na washikamane na kamba imara ya Mwenyezi Mungu, na hakuna tofauti kama mjuavyo
baina ya Sunni na Shia isipokuwa ni katika yale waliyotofautiana kwa ajili ya
Ukhalifa baada ya Mtume, na msingi wa tofauti ni itikadi yao kuhusu Masahaba,
nao Masahaba (r.a.) walitofautiana kati yao mpaka wakalaaniana, kupigana na
kuuana wao kwa wao. Ikiwa kutofautiana kati yao ni kutoka katika Uislamu basi Masahaba
ndiyo wa mwanzo kutuhumiwa kwa tuhuma hii na Mwenyezi Mungu apishe mbali.
Mimi siitakidi kwamba ninyi mnayaridhia hayo, na uadilifu
unakulinganieni msiridhiye Mashia kutolewa nje ya Uislamu, kama ambavyo
Mashia wana desturi ya kuwatukuza Ahlul-Bait (a.s.) na kuwaheshimu vile vile
Masunni wanayo desturi ya kuwatukuza Masahaba wote, na misimamo hii miwili iko
mbali mbali.
Basi ikiwa Mashia kwa desturi yao hiyo wanakosea, basi Masunni ndiyo
watakaokuwa wanakosea zaidi (katika desturi yao)
kwani Masahaba wote wanawatanguliza Ahlul-Bait (a.s.) kuliko nafsi zao, na
huwatakia rehma kama wamtakiavyo rehma Mtume (s.a.w.w.). Na
hatumfahamu yeyote miongoni mwa Masahaba (r.a.) aliyeitanguliza nafsi yake au
aliyejitukuza juu ya watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) katika elimu au matendo
mema.
Basi wakati umefika kuliondosha giza la kihistoria kwa wafuasi wa
Ahlul-Bait (a.s.), kushirikiana nao, kuunga udugu, kusaidiana
kwa mema na kumcha Mwenyezi Mungu na
imetosha kwa umma huu kumwaga damu na kusambaza fitna.
Huenda Mwenyezi Mungu Mtukufu akaunganisha kupitia kwenu kauli (ya
umoja) na kuuondoa utengano, akalitibu jeraha hili na akauzima moto wa fitina
na kumdhalilisha shetani na kundi lake na mtakuwa ninyi mbele ya Mwenyezi Mungu
ni wenye kufaulu hasa kwa kuwa ninyi mnatokana na kizazi kitukufu kama
ninavyosikia.
Basi fanyeni hayo ili mpate kufufuliwa pamoja nao. "Na hakika
umma wenu ni mmoja nami ndiye Mola wenu. " "Na waambie, fanyeni
Mwenyezi Mungu ataona matendo yenu na Mtume wake na waumini".
Mwenyezi Mungu akuwafikisheni ninyi na sisi kwa mambo ambayo
ndani yake kuna kheri ya nchi na waja, Mwenyezi Mungu akujaalieni ninyi na sisi
kuwa miongoni mwa wenye kutenda (mema) wenye utakaso kwa ajili ya Mwenyezi
Mungu Mtukufu.
Nakutumieni kwa heshima yenu pamoja na barua hii nakala ya kitabu
changu "Thummah-Tadaitu" ambacho nilikitunga maalumu kuhusiana na
maudhui haya, hiyo ni zawadi yangu kwenu huenda kikapata kukubalika mbele yenu.
Was-salaam Alaikum Warahmatullahi Taala wa Barakatuh.
Muhammad Tijani As-Samawi At-Tunisi
Sunday, 20 April 2014
MAMBO MENGINE YA WAJIBU KATIKA SWALA NA AMBAYO NI RUKNI ZA NGUZO ZA SWALA
6-
Qira’a: (Kusoma Suratul Fatiha, yaani: Al-Hamdu, kisha Sura yoyote).
Sura
unayoisoma lazima uisome kuanzia mwanzo hadi mwisho, hairuhusiwi kusoma sura
nusu, rakaa ya kwanza kisha kusoma nusu iliyobaki katika rakaa ya pili. Bali
inatakiwa isomwe sura kamili mwanzo hadi mwisho.
Hapa
lazima tuweke wazi: Ukichunguza swala za walio wengi ktk madh-hebu ya
Ahlus-sunna, utakuta baada ya kusoma Al-hamdu, basi mtu anasoma sura yoyote
ndefu kama Suratul-Baqarah kama Aya kumi kisha anarukuu, kisha anarudi rakaa ya
pili anasoma Aya zingine kama ishirini au kumi na tano au zozote atakazoweza
kutoka sura nyingine kama vile Suratun-Nisaa kisha anarukuu! Lakini kwa mujibu
wa mafunzo sahihi tunayofundishwa au iliyofundishwa na Maimam wetu watukufu
(a.s) kutoka Nyumba ya Mtume (s.a.w.w) ambao hakuna shaka yoyote (wala chembe
ya shaka kwamba) wanaijua vizuri zaidi swala ya Mtume (s.a.w.w), swala sahihi
lazima ktk QIRAA isomwe sura kamili ana sio nusu sura au robo yake au nusu
robo. Na hivyo ni bora mwenye kuswali au kuswali kama Imam asome sura fupi ktk
swala ambazo atakuwa na uwezo wa kuzisoma mwanzo hadi mwisho na sio kusoma sura
ndefu wakati anajua anawaongoza watu ambao wanatofautiana hali zao za kiafya
7-Dhikr
8-Tashahhud
9-Salam
10-Tartib:
(Kwa maana kwamba: Swala lazima iswaliwe kwa kufuata utaratibu huu: kuanzia Takbiratul-Ihram,
Qira’a, kisha Rukuu, kisha sujud, kisha ukae ktk rakaa ya pili baada ya sajda
usome TASHAHUD, ukimaliza ndio usimame kwa kwa ajili ya rakaa ya tatu,kisha
ukae ktk rakaa ya mwisho usome TASHAHUD, na baada ya Tashahud umalizie
kwa Salam, swala inatakiwa iwe ktk utaratibu huo au tuseme ifuate utaratibu
huo, sio unaanza na Takbiratul-Ihram, kisha unaingia sajda, unaacha qira’a na
rukuu, namna mwenye kuswali atakuwa hajafuata utaratibu, na atahesabika
anaswali anavyotaka na sio inavyotakiwa).
11-
Muwalaat: Yaani: Lazima mwenye kuswali ahakikishe anaswali swala yake
kwa kufuatanisha vitendo pasina kuacha gape au nafasi baina aya kitendo na
kitendo. Mfano: Baada ya Takbiratul-ihram, unaingia moja kwa moja kwenye Qira’a
na baada ya Qira’a Al-hamdu na sura na baada ya hapo unaingia moja kwa moja
kwenye Rukuu, namna hiyo. Hivyo haitakiwi kutoa Takbiratul-Ihram kisha kukaa
kama dakika tano kama haupo kwenye swala kisha ndio usome Al-hamdu na sura
kisha baada ya kurukuu unakaa kama dakika kumi ndio unaamua kurukuu, namna hiyo
utakuwa hujafatanisha vitendo ktk swala, bali kwa kuachanisha vitendo namna
hiyo maana ya swala inapotea kabisa na utatoka nje ya swala na kubatilisha
swala yako. Na hata kusoma sura ndefu kama vile suratul-baqara ukiig’ang’ania
mpaka uimalize hatua hiyo inaondoa kabisa ufuatanishaji wa vitendo ktk swala, na
ndio ikawa ni bora kusoma sura fupi ktk swala kwa kuzikamilisha na sio nusu
yake.
Nguzo za swala ni tano:
1- NIA
Nia si lazima utamke kwa maneno kwamba, nina swali swala ya dhuhri yenye rakaa nne, kurbatan ila llah, si lazima uimbe nia namna hiyo bali nia inatosha kile ulichokiazimia moyoni mwako, maana ile kuchukua maji, ukatia udhu, tayari ushajenga nia katika moyo wako na katika akili yako kwamba sasa naelekea kwenye swala fulani. Nia maana yake ni ile azma yako kunako unachotaka kukitenda, si sharti uanze kuitaja kwa maneno. Mfano; Msafiri anayetaka kuelekea sehemu fulani, huwa anatia nia kuwa kesho au sasa hivi ninasafiri kuelekea sehemu fulani, nia hiyo huwa ipo moyoni, na ile kutoka kuelekea kituo cha basi hutosha kabisa kudhihirisha nia yake ya safari yake.
Hivyo nia hutimia pasina kutamkwa na ile kutakwa sio sharti katika Nia, bali unaweza kuitamka tu kwa ulimi na isitimie, maana kutimia kwa nia ni pale inapohudhuria moyoni kiasi kwamba akili ya mwenye kuswali inakuwa haiwazi kitu kingine tofauti na swala na kwamba sasa yupo mbele ya Mwenye-enzi Mungu (s.w). Hiyo ndiyo nia ambayo unatakiwa kuileta mwanzo wa swala na iendelee kuwepo hadi mwisho wa swala. Hivyo nia sio mwanzo wa swala tu bali iwepo hadi mwisho kabisa wa swala yako.
2- QIYA’M (Kusimama wima).
3- TAKBIRATUL-IHRAM(Takbir ya kuhirimia swala na ambayo inaashiria mwanzo wa swala kwamba sasa swala imeanza).
4- RUKUU (Kurukuu).
5 - SUJUD (Kusujudu)

MAMBO YA WAJIBU KATIKA SWALA
Mambo ya wajibu
katika swala ni kumi na moja (11). Lazima mwenye kuswali ahakikishe mambo hayo
kumi na moja ameyatenda kama inavyotakiwa. Katika mambo haya kumi na moja (11)
ya wajibu kuna matano (5) ni RUKNI (Yaani: Ni nguzo za Swala) na mengine sita
(6) yaliyobaki si RUKNI katika swala.
Na inaposemwa “RUKNI ZA SWALA”, humaanishwa NGUZO ZA SWALA, kwa maana kwamba: Swala imesimama katika nguzo hizo tano, ikitokea nguzo moja ikaharibika au isitendeke kama inavyotakiwa au ikasahaulika katika swala basi swala itakuwa si sahihi, mwenye kuswali atatakiwa kurudia swala yake.
Ama yale mambo sita (6) ambayo sio nguzo za swala, ikitokea moja wapo kati ya hayo (sita) ikasahaulika ktk swala au kutendeka isivyotakiwa basi swala haitaharibika au tuseme: Haitakuwa batili, bali itakuwa ni swala sahihi, maana kukosea au kusahau katika hayo mambo sita ambayo si nguzo ktk swala hakuharibu swala wala kuibatilisha, isipokuwa makosa hayo au kusahau huko kukitokea ktk moja wapo ya nguzo za swala ambazo tutazitaja hivi punde.

MAULID (MAJLIS) YA KUZALIWA KWA BI FATUMA ZAHRAH
Assalaam alaykum warahmatullah wabarakatuh:
Jumuiya wa waislamu wa madhehebu ya Shia Kigoma inawakaribisha watu wote kuhudhuria sherehe za kukumbuka kuzaliwa kwa bint pekee wa Mtume Mohammad (S.A.W.W) aitwaye Fatuma bint Rasulillah. Hapa chini kuna maelezo kamili ya Historia ya bint huyu mtukufu:

Kimeandikwa na
Mwalimu Kabavako, Rajabu Shaban
BSc. Applied
Agriculrural Extension (SUA)
© 2014
Wasifu wa Bi Fatima Zahra (a.s.)
this topic
Jina lake: Fatima bint Rasulillah (a.s)
Cheo chake: Kiongozi wa wanawake wa peponi
Majina (sifa) yake mengine:
az- Zahra (Mzuri)
Al- Mardhiah (Aliyeridhiwa na Allah (S.W))
Al- Mubarakah (Aliyebarikiwa)
At- Taherah (Aliyetakaswa na Allah yaani asiye na dhambi)
Az- Zakiyah (Muadilifu)
Ar- Radhiah (aliyeridhika)
Al- Batoul (Msafi)
Ummu 'l-A'immah (Mama wa Maimamu)
Jina la baba yake: Muhammad ibn 'Abdillah (S.A.W.W.)
Jina la mama yake: Khadijah bint Khuwaylid
Mahali na tarehe ya kuzaliwa: Makkah, 20 Jumada ' th-Thaniyah mwaka wa 5 baada ya kutangazwa Utume (615 AD).
Kufa: 14th Jumada ' l-ula 11 hijiria (632 AD);

Kuzikwa: Jannatu 'l-Baqi' huko Madina
Umri wakati anafariki dunia: miaka 18
Kuolewa: mwaka 2 hijiria
Watoto wa Fatima Zahra (A.S.) ni kama ifuatavyo:
(a) Imam Hassan (A.S.)
(b) Imam Hussain (A.S.)
(c) Bi Zainab (A.S.)
(d) Bi Um Kulthum (A.S)
(e) Mohsin (A.S)
(a) Imam Hassan (A.S.)
(b) Imam Hussain (A.S.)
(c) Bi Zainab (A.S.)
(d) Bi Um Kulthum (A.S)
(e) Mohsin (A.S)
Bi Khadija mama wa Fatuma alifariki dunia wakati bint huyu
mtukufu akiwa na umri wa miaka 5. Hivyo akabaki analelewa na baba peke yake.
Moja
ya sifa nyingine ya Bibi Fatma ni kuishi maisha ya kawaida na yasiyo na fakhari
hasa za kidunia. Siku moja Salman Farsi alifuatana na Bibi Fatimah hadi
nyumbani kwa Bwana Mtume. Walipokuwa
njiani kuelekea nyumbani kwa Bwana Mtume, Salman alisema: Samahani! Mabinti wa
Kaisari na Qasir wanavaa nguo za Hariri lakini binti wa Muhammad (S.A.W.W),
mwanaadamu bora kabisa amevaa abaa lililochakaa. Wakati walipofika nyumbani kwa
Bwana Mtume SAW, Bibi Faatimah alimwambia baba yake kwamba: Baba yangu mpenzi!
Salman amestaajabishwa na mavazi yangu. Bwana Mtume (SAW) akamwelekea Salman na
kumwambia: Salman! Binti yangu (si binti wa Kaisari na wafalme wanaopenda fakhari
za kidunia, bali binti yangu ni miongoni mwa walio mstari wa mbele katika mbio
za kwenda kwa Mwenyezi Mungu.
Bwana Mtume Muhammad (SAW) alinukuliwa akisema:
"Faatimah ni kipande cha mwili wangu, ni nuru ya jicho langu, ni tunda la
moyo wangu, ni moyo na ni roho yangu. Yeye ni hurulaini katika sura ya mwanadamu...
kila anaposimama kufanya ibada, Mwenyezi Mungu anawaambia malaika Wake: Mwangalieni
mja wangu aliye bora - Faatimah - amesimama mbele Yangu na dhati yake yote
inatetemeka kutokana na unyenyekevu wake mkubwa Kwangu na amesimama kuniabudu
kwa moyo wake wote."
Bibi
Fatimatuz Zahra SA ni bibi mtukufu ambaye sira na mienendo yake itabakia hai
milele na itaendelea kuwa ruwaza njema kwa kila mpigania haki. Bibi Fatima SA
hakuishi kwa zaidi ya miaka 18, lakini alikusanya fadhail na matukufu yote ya
kibinadamu. Mtukufu huyo alifikia daraja kubwa ya kumtambua Muumba wake kiasi
kwamba hadi leo hii amekuwa ni kigezo bora cha maisha yaliyojaa ufanisi. Dhati
yake yote ilijaa welewa na utambuzi wa Muumba wake kadiri kwamba, hakuwa
akifikiria kitu chochote katika maisha yake yote isipokuwa kumridhisha Muumba
wake. Bwana Mtume Muhammad SAW anatoa ushahidi wa mapenzi hayo ya kweli
aliyokuwa nayo Fatima (a.s) kwa Muumba wake kwa kumwambia mmoja wa masahaba
wake wakubwa Salman kwamba: Ewe Salman! Mwenyezi Mungu amemimina na kutia imani
thabiti katika moyo na roho na dhati yote ya Fatima ya kumuabudu Muumba wake
kiasi kwamba hakujabakia sehemu hata ndogo tupu ya kuingia kitu kingine
chochote katika moyo wake ghairi ya kumuabudu Mola wake.
Roho
tukufu ya Fatima haikupenda kabisa mapambo na urembo wa dunia. Nyumba ya Ali na
Fatima SA haikuwa kabisa na vifaa vya nyongeza na vya thamani kubwa. Lakini
badala yake ilikuwa ni nyumba iliyojaa imani, mapenzi na unyofu wa moyo hali
ambayo iliongeza moyo wa kutekeleza vizuri majukumu, kupigania uadilifu na
kusimamisha haki. Fatima alikuwa mbora wa wanawake wacha Mungu, lakini si kwa
maana ya kuachana kikamilifu na dunia bali kwa maana ya kwamba dunia haikuiteka
roho yake na wala kuifanya mtumwa wake. Kwa kweli hakuna mwanamke aliyemfikia
Fatima kwa ubora.
Chochote
alichokipata alikitumia katika njia ya Mwenyezi Mungu na alikuwa mstari wa
mbele wakati wote kujitolea kwa ajili ya kutafuta radhi za Muumba wake.
Maneno
na matendo ya Fatima yalipambika kwa adabu na heshimu kiasi kwamba mmoja wa
watu waliokuwa wakimhudumia mtukufu huyo anayejulikana kwa jina la Asmaa anasema:
Mimi sijawahi kumuona mwanamke mwenye adabu na heshima kama Fatima. Yeye
amejifunza adabu na heshima kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Wakati Mwenyezi Mungu
aliposhusha aya na kuwataka Waislamu na waumini wasimwite Bwana Mtume kwa jina
lake, Bibi Fatima (a.s) naye aliacha kutumia neno "baba" kumwita baba
yake, bali alianza kumwita Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hadi Bwana Mtume
akalazimika kusema, aya hiyo haimuhusu mwanangu Fatima.
Katika
maisha yake ya kifamilia pia, heshima na adabu pamoja na mapenzi ya Fatima
yalijenga mfungamano mkubwa na mtukufu sana kati yake na mumewe Ali (a.s).
Katika
muda wote wa uhai wa baba yake Bwana Mtume Muhammad (S.A.W.W) na baada ya
kutangulia mbele ya haki baba yake mtukufu, akawa pamoja na mumewe Ali AS,
Fatima wakati wote alikuwa bega kwa bega na watukufu hao katika kupigania haki,
kueneza uadilifu na kuhakikisha kuwa nuru ya Uislamu haizimi. Mtukufu huyo
alikuwa na moyo wa hali ya juu wa kutekeleza vilivyo majukumu yake.
Mtukufu
huyo alikuwa akihimiza kwamba mtu mwenye ufanisi ni yule ambaye anatekeleza
vizuri majukumu yake mema. Muhimu ni kwamba mtu huyo ajue wajibu wake na
autekeleze inavyopasa. Kutekeleza vizuri jukumu lake mtu kunahitajia welewa na
maarifa pamoja na muono wa mbali. Na ndio maana wakati wote mtukufu huyo alikuwa
akifanya juhudi kutumia nguvu zake zote katika kutekeleza mambo yanayomridhisha
Mola wake. Pamoja na kwamba alijua kuwa angeliweza kukaa pembeni na kutumia
muda wake wote kufanya ibada na kunong'ona na Mola wake, lakini alitambua vyema
pia kuwa, jukumu la mtu ni zaidi ya kufanya ibada, kwani siku ya Kiyama watu
wote wataulizwa walitekeleza vipi majukumu yao yote.
Mtukufu
huyo, kutokana na muono wake wa mbali na mtazamo wake wa kina wa mambo aliona
hatari kubwa ya kurejea watu kwenye zama za ujahilia hasa baada ya kufariki
dunia Bwana Mtume Muhammad (SAW). Alitumia hekima ya hali ya juu kuwalingania
watu haki na hakumuogopa mtu yeyote katika kubainisha mafundisho ya Bwana Mtume
(SAW) na kuulinda Uislamu.
Miongoni
mwa urithi wenye thamani kubwa uliobakishwa na Bibi Fatimatuz Zahra (a.s) ni
hotuba yake yenye umuhimu mkubwa aliyoitoa baada ya kufariki dunia baba yake
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW). Aliitoa hotuba hiyo baada ya kuhisi kuzuka
mipasuko na kupotoshwa mambo katika jamii ya Waislamu mara baada ya kufariki
dunia Mtume. Ndani ya hotuba hiyo, Bibi Fatima ametaja sifa za Waislamu wa
kweli. Hotuba hiyo ilikuwa mithili ya nuru inayowaangazia njia wapenda haki na
wanaotafuta njia sahihi. Bibi Fatimatuz Zahra (a.) anataja njia ya kuweza
kumwokoa mwanadamu kuwa ni kushikamana na haki na kuwa mtiifu mbele ya amri za
Mwenyezi Mungu.
Katika
sehemu moja ya hotuba hiyo yenye thamani kubwa Bibi Fatimatuz Zahra (a.s)
anasema: Enyi watu! Kumbukeni mlipokuwa ukingoni mwa shimo la moto! Kumbukeni
mlivyokuwa duni na mkidharauliwa, na wakati wote mlikuwa mnaogopa wasije maadui
kukushambulieni na kukutekeni! Hadi Mwenyezi Mungu alipomtuma Mtume Wake
Muhammad (SAW) kwenu. Mtume wa Mwenyezi Mungu ameingiza nuru katika kiza cha
kufru na shirki, akaondoa ugomvi na mizozo kati yanu na kufuta kwa nuru, vumbi
lililokuwa limeyafunika macho yenu.
Tunamuomba
Mwenyezi Mungu atupe taufiki ya kufuata njia ya haki, njia iliyooneshwa na waja
wema wa Mwenyezi Mungu, njia ya watu Wake wateule na watoharifu.
Assalaamu
Alayki Yaa Fatimatuz Zahra, Sayyidatu Nisail L'aalamin.
Amani
iwe juu yako Ewe Fatima, Mbora wa wanawake wote duniani.
Wassalaamu
Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.
8 killed, 27 injured since Friday in Chicago shootings
Chicago is one of the most dangerous cities in the US with very high gun deaths.
Sun Apr 20, 2014 11:16PM GMT
4
128
18
At least eight people have lost their lives and 27 others have sustained injuries in several shootings since Friday across Chicago, one of the most dangerous cities to live in the United States.
At least 10 shooting incidents took place in the city on Easter Sunday alone, according to police officials.In the latest incident, one person was killed and another was injured in the 2800 block of South Sawyer Avenue at around 1 p.m. Sunday.
The victims were a 33-year-old man who was fatally shot in the head and a 19-year-old teenage boy who was shot in the chest. The teenager is said to be in critical condition.
Police say they have found the lifeless bodies of two men with gunshot wounds in a Garfield Ridge home after 5 a.m. Sunday. One of the victims, Javier Acevedo, was Corrections officer at Cook County Department.
Police say the two were killed in a murder-suicide.
Chicago is one of the most dangerous cities in the US with very high gun deaths. An FBI crime statistics, released in late 2013, said the city registered more homicides in 2012 than New York City.
The FBI report said there were 500 murders in Chicago and 419 in New York in 2012. Chicago’s population is one third of that of New York.
The United States has more guns and more gun related deaths than any other developed country in the world, according to a new study by US doctors.
Anti-gun campaigners maintain more than thirty Americans shot dead, and scores more treated for gun-related injuries in hospitals every day.
Critics blame the notoriously liberal gun control laws in the United States for the high rate of gun violence in the country.
The United States is using assassination drones in other countries in line with its self-declared right to kill, an analyst tells Press TV in an interview.
“It’s a flagrant violation of international law. It is establishing unilaterally by one nation, the United States, the right to kill at will,” Rick Rozoff said.
The analyst made the comments following a report by UN special rapporteur Christopher Haines that the US policy of using assassination drones presents a major challenge to the system of international law that has endured since WWII.
Rozoff said the US has been involved in “slaughter from the air” for a decade.
“They’re aerial assassins. If they offend international law, they certainly offend human morality,” he said.
Rozoff said it would be “simply ludicrous” to believe that thousands of Pakistanis killed in the US drone strikes have all been “high-profile al-Qaeda commanders.”
“This is no excuse in the war crimes tribunal. It certainly won’t be if the US is ever held accountable for its actions,” said Rozoff.
The analyst said the US unnamed aerial vehicles, known as ‘hunter, killers’, “have accounted already for conservatively five to six thousand deaths in the last 10 years.”
Washington claims its drone strikes target militants, although casualty figures show that civilians often fall victim to the attacks.
Over the past several years, Washington has been launching drone attacks on Muslim countries, including Pakistan, Somalia, and Yemen
Je Abubakar ni kweli kuwa alikuwa ndiye ndugu wa karibu zaidi kwa Mtume kuliko wengine
Miongoni mwa Maswahaba, Sayyidna
Abubakar hudaiwa kuwa ndiye bora kuliko wengine kwa sababu ya ukaribu wake kwa
Mtukufu Mtume (S.A.W.W). Kama habari hii ni ya kweli kwa nini Mtume Mtukufu
hakumchagua yeye kuwa ndugu yake wakati Mtume alipowapanga Maswahaba katika
makundi ya wawili wawili na kuwafanya kuwa ndugu, muda mfupi baada ya Hijra,
wakati ambapo Mtume Mohammad (S.A.W.W) alimtangaza Imam Ally (a.s) kuwa ndugu
yake, akimwambia, “wewe ni ndugu yangu katika ulimwengu huu na ulimwengu ujao”.
Kwa vigezo gani ninyi Masunni
mnasema kuwa Abubakar alikuwa ndugu wa karibu zaidi kwa Mtume kuliko wengine?
Angalia Historia ya Makhalifa, cha
Jalaludin Suyuti, Tafsir ya Abdassamad Clarke ya English, ukurasa wa 177 (Taha
Publishers)
Swali kwa Ahlul-Sunnah wal-Jamaa
Bi Fatumah Zahra (a.s) alifariki miezi mitatu tu baada ya
kifo cha baba yake yaani Mtume Mohammad (S.A.W.W) na kuzikwa mahali
pasipoeleweka na mpaka leo kaburi lake halijulikani liko wapi. Lakini Sayyidna
Abubakar aliyefariki miaka miwili baada ya kifo cha mtume na sayyidna Umari
aliyefariki miaka 20 baadaye walizikwa pembeni ya kaburi la Mtume. Kwa nini mabwana hao wawili wazikwe pembeni
ya mtume na wala si bint wake wa pekee (bi Fatumah)? Je ni bint huyo mtukufu
ndiye aliomba azikwe mbali na baba yake? Kwa nini? Au waislamu ndio waliozuia
bint huyo kuzikwa pembeni ya baba yake?
(soma Sahih al Bukhari Arabic - English juzuu la 5 hadith
ya 546 kwa majibu ya maswali hayo).
SHIDA ZILIZOWAPATA WAISLAMU WA
MWANZO.
Historia inaonesha kuwa Mheshimiwa Mtume Mohammad (S.A.W.W)
alipotangaza tu kuwa yeye ni Mtume, Maquraishi waliwawekea vikwazo Bani Hashim
(ukoo wa Mtume). Vikwazo hivyo vilihusu kuzuia kununua na kuuza kwa Bani Hashim
na pia kuwazuia kuishi ndani ya mji wa Makah.
Mzee Abu Talib (a.s) aliuchukua ukoo huo na kuupeleka katika eneo
liitwalo Shib Abi Talib na walikaa kule kwa miaka mitatu wakiwa na shida nyingi
kiasi cha kula viatu vyao na majani ya miti pori. Mzee huyu Mtukufu alikuwa
halali mpaka ahakikishe kuwa Mtume amelala eneo salama.
Je Abubakar na Umar alikuwa wapi kipindi hiki? Watu hawa wanaodai kuwa
ni watukufu zaidi walikuwa Makah akiponda raha na wala hawakumsaidia Mtume na
ukoo wake katika kipindi hiki cha hatari na shida. Wale wapenzi wao walete
ushahidi wa, kwa namna gani mabwana hawa walitoa msaada kwa Uislamu katika
kipindi hiki, kwa mfano chakula au nguo na hivyo kwenda kinyume na vikwazo vya
Maquraish.
Katika kipindi hiki Maquraish walikuwa wameandika mkataba baina
yao na kuutundika ndani ya Qaaba ili kuzuia watu wasiuze, kununua wala kuoleana
na koo za Bani Hashim na bani Al Muttalib. Huu mkataba ndio uliowatesa waislamu
na ukoo mzima wa Bani Hashim na Bani Mutalib na kuwanufaisha makafiri na
vibaraka wao. Abu Lahab aliachana na
Bani Hashim wenziwe na kujiunga na Maquraish ambao ndani yao walikuwepo
Abubakar bin Quhafah na Umar bin Khatab na wala hawakutoa mchango wowote katika
kuwasaidia waislamu. Wakati Abubakar na Umar wakitanua kuna baadhi ya Maquraish
walikuwa wakipeleka chakula kwa waislamu kwa siri na mmoja wa hawa watu ni kaka
wa Khadija bint Khuwalid (kaka wa mke wa Mtume). (1. al-Tabari juzu 6 uk. 81,
2. Siratun Nabi cha Shibli Numani juzu 1 uk 218).
Cha kushangaza zaidi, mpaka leo kuna watu ambao wamekaa pembeni na
kushuhudia waislamu wakiteseka bila kuwasaidia na badala ya kuwasaidia huwaita
waislamu hao kuwa ni makafiri au wamejitakia wenyewe. Watu hawa utawakuta
wakipita huku na huko kuwashawishi waislamu kuwachukia waislamu wenzao.
Uislamu ni dini moja, dini ya upendo na umoja hairuhusu tabia hizi
mbaya za kijifanya waislamu, huku wakiwasaliti au kuwaua waislamu wenzio.
Subscribe to:
Posts (Atom)