Sunday, 20 April 2014

Nguzo za swala ni tano:

1- NIA
Nia si lazima utamke kwa maneno kwamba, nina swali swala ya dhuhri yenye rakaa nne, kurbatan ila llah, si lazima uimbe nia namna hiyo bali nia inatosha kile ulichokiazimia moyoni mwako, maana ile kuchukua maji, ukatia udhu, tayari ushajenga nia katika moyo wako na katika akili yako kwamba sasa naelekea kwenye swala fulani. Nia maana yake ni ile azma yako kunako unachotaka kukitenda, si sharti uanze kuitaja kwa maneno. Mfano; Msafiri anayetaka kuelekea sehemu fulani, huwa anatia nia kuwa kesho au sasa hivi ninasafiri kuelekea sehemu fulani, nia hiyo huwa ipo moyoni, na ile kutoka kuelekea kituo cha basi hutosha kabisa kudhihirisha nia yake ya safari yake.
Hivyo nia hutimia pasina kutamkwa na ile kutakwa sio sharti katika Nia, bali unaweza kuitamka tu kwa ulimi na isitimie, maana kutimia kwa nia ni pale inapohudhuria moyoni kiasi kwamba akili ya mwenye kuswali inakuwa haiwazi kitu kingine tofauti na swala na kwamba sasa yupo mbele ya Mwenye-enzi Mungu (s.w). Hiyo ndiyo nia ambayo unatakiwa kuileta mwanzo wa swala na iendelee kuwepo hadi mwisho wa swala. Hivyo nia sio mwanzo wa swala tu bali iwepo hadi mwisho kabisa wa swala yako.
2- QIYA’M (Kusimama wima).
3- TAKBIRATUL-IHRAM(Takbir ya kuhirimia swala na ambayo inaashiria mwanzo wa swala kwamba sasa swala imeanza). 
4- RUKUU (Kurukuu).
5 - SUJUD (Kusujudu)

No comments:

Post a Comment