Sunday 20 April 2014

SHIDA ZILIZOWAPATA WAISLAMU WA MWANZO.
Historia inaonesha kuwa Mheshimiwa Mtume Mohammad (S.A.W.W) alipotangaza tu kuwa yeye ni Mtume, Maquraishi waliwawekea vikwazo Bani Hashim (ukoo wa Mtume). Vikwazo hivyo vilihusu kuzuia kununua na kuuza kwa Bani Hashim na pia kuwazuia kuishi ndani ya mji wa Makah.
Mzee Abu Talib (a.s) aliuchukua ukoo huo na kuupeleka katika eneo liitwalo Shib Abi Talib na walikaa kule kwa miaka mitatu wakiwa na shida nyingi kiasi cha kula viatu vyao na majani ya miti pori. Mzee huyu Mtukufu alikuwa halali mpaka ahakikishe kuwa Mtume amelala eneo salama.
Je Abubakar na Umar alikuwa wapi kipindi hiki? Watu hawa wanaodai kuwa ni watukufu zaidi walikuwa Makah akiponda raha na wala hawakumsaidia Mtume na ukoo wake katika kipindi hiki cha hatari na shida. Wale wapenzi wao walete ushahidi wa, kwa namna gani mabwana hawa walitoa msaada kwa Uislamu katika kipindi hiki, kwa mfano chakula au nguo na hivyo kwenda kinyume na vikwazo vya Maquraish.

Katika kipindi hiki Maquraish walikuwa wameandika mkataba baina yao na kuutundika ndani ya Qaaba ili kuzuia watu wasiuze, kununua wala kuoleana na koo za Bani Hashim na bani Al Muttalib. Huu mkataba ndio uliowatesa waislamu na ukoo mzima wa Bani Hashim na Bani Mutalib na kuwanufaisha makafiri na vibaraka wao.  Abu Lahab aliachana na Bani Hashim wenziwe na kujiunga na Maquraish ambao ndani yao walikuwepo Abubakar bin Quhafah na Umar bin Khatab na wala hawakutoa mchango wowote katika kuwasaidia waislamu. Wakati Abubakar na Umar wakitanua kuna baadhi ya Maquraish walikuwa wakipeleka chakula kwa waislamu kwa siri na mmoja wa hawa watu ni kaka wa Khadija bint Khuwalid (kaka wa mke wa Mtume). (1. al-Tabari juzu 6 uk. 81, 2. Siratun Nabi cha Shibli Numani juzu 1 uk 218).
Cha kushangaza zaidi, mpaka leo kuna watu ambao wamekaa pembeni na kushuhudia waislamu wakiteseka bila kuwasaidia na badala ya kuwasaidia huwaita waislamu hao kuwa ni makafiri au wamejitakia wenyewe. Watu hawa utawakuta wakipita huku na huko kuwashawishi waislamu kuwachukia waislamu wenzao.

Uislamu ni dini moja, dini ya upendo na umoja hairuhusu tabia hizi mbaya za kijifanya waislamu, huku wakiwasaliti au kuwaua waislamu wenzio. 

No comments:

Post a Comment