Wednesday 23 April 2014

HUKUMU YA MAVAZI WAKATI WA SWALA

1. Vazi la mwanamume lazima lisitiri sehemu zake za siri, ikiwa hakuna au kuna mtu mwingine.
2. Ama mwanamke lazima asitiri viongo vyake vyote vya mwili ispokuwa viganja, nyayo za miguu mpaka vifundo vyake na paji la uso linalooshwa wakati wa kutawadha.
3. Kuhusu Vazi la kusalia ni lazima kuzingatia yafuatayo:-
a) Liwe tohara
b) Liwe la halali (si la unyang’anyi)
c) Lisitokane na wanyama haramu kuliwa.
d) Lisitokane na viungo vya mzoga.
e) Mwanaume haruhusiwi kuvaa dhahabu au mavazi yenye nakshi za dhahbu wala nguo zilizotengenezwa kutokana na hariri.
4. Katika Swala hairuhusiwi kubebe vitu vilivyo tokana na wanyama haramu kuliwa, vinginevyo swala itabatilika. Mfano, kuvaa saa au mkanda wa nyama za nyoka.
5. Ikiwa hatambui kuwa mwili wake au nguo zake si tohara na kubaini hivyo baada ya swala, swala yake itakuwa halali.
6. Ikiwa mtu atasahau kwamba mwili wake au nguo zake si tohara na kukumbuka wakati au baada ya sala, itmlazimu kujitoharisha na kusali tena. Ikiwa wakati wa sala uliobainishwa umepita, atalazimu kuitekeleza.
7. Ikiwa mwili au nguo zimekuwa si tohara kwa damu kwa kipimo chini ya dilhamu, Swala yake itakuwa halali.

No comments:

Post a Comment