Bi Fatumah Zahra (a.s) alifariki miezi mitatu tu baada ya
kifo cha baba yake yaani Mtume Mohammad (S.A.W.W) na kuzikwa mahali
pasipoeleweka na mpaka leo kaburi lake halijulikani liko wapi. Lakini Sayyidna
Abubakar aliyefariki miaka miwili baada ya kifo cha mtume na sayyidna Umari
aliyefariki miaka 20 baadaye walizikwa pembeni ya kaburi la Mtume. Kwa nini mabwana hao wawili wazikwe pembeni
ya mtume na wala si bint wake wa pekee (bi Fatumah)? Je ni bint huyo mtukufu
ndiye aliomba azikwe mbali na baba yake? Kwa nini? Au waislamu ndio waliozuia
bint huyo kuzikwa pembeni ya baba yake?
(soma Sahih al Bukhari Arabic - English juzuu la 5 hadith
ya 546 kwa majibu ya maswali hayo).
No comments:
Post a Comment