Wednesday 23 April 2014

NAMNA YA KUMSALIA MTUME MOHAMMAD (S.A.W.W)

Qur'an, 33:52 inasema, “Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Mtume, Enyi mlioamini msalieni na mpeni salamu bila kusita.”Wanazuoni wote yaani Sunni na Shia wameafikiana kwamba masahaba walikwenda kwa Mtume na kumuuliza, “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, sisi tumekwisha fahamu namna ya kukusalimia lakini hatufahamu ni namna gani tutakusalia?”Mtume akasema, “Semeni Allahumma swali alaa Mohammad wa aali Mohammad kamaa swalaita 'alaa Ibrahim wa aali Ibrahim fil'alamina, innaka hamidun majiid, yaani Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu Mohammad na aali zake Mohammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali zake Ibrahim katika walimwengu, hakika wewe ni mwenye sifa njema tena Mtukufu; na wala msinisalie sala iliyo katika.”

Masahaba wakauliza ni ipi sala iliyokatika ewe Mjumbe wa Allah?

Mtume akajibu, “sala iliyokatika ni kusema ewe Mwenyezi Mungu msalie Mohammad na kisha mkanyamaza, na fahamuni kuwa Mwenyezi Mungu ni mkamilifu, hakubali ila kitu kilichokamilika.

Kutokana na hili Imam Shafii anasema, “Enyi kizazi cha nyumba (Ahlulbayt) ya Mtume wa Mwenyezi Mungu mapenzi kwenu ni faradhi (wajibu) kutoka kwa Allah, ameyateremsha ndani ya Qur'an, yakutosheni ninyi heshima tukufu ya kwamba yeyote asiyekusalieni hana sala (sala yake ni batili).

No comments:

Post a Comment