Miongoni mwa Maswahaba, Sayyidna
Abubakar hudaiwa kuwa ndiye bora kuliko wengine kwa sababu ya ukaribu wake kwa
Mtukufu Mtume (S.A.W.W). Kama habari hii ni ya kweli kwa nini Mtume Mtukufu
hakumchagua yeye kuwa ndugu yake wakati Mtume alipowapanga Maswahaba katika
makundi ya wawili wawili na kuwafanya kuwa ndugu, muda mfupi baada ya Hijra,
wakati ambapo Mtume Mohammad (S.A.W.W) alimtangaza Imam Ally (a.s) kuwa ndugu
yake, akimwambia, “wewe ni ndugu yangu katika ulimwengu huu na ulimwengu ujao”.
Kwa vigezo gani ninyi Masunni
mnasema kuwa Abubakar alikuwa ndugu wa karibu zaidi kwa Mtume kuliko wengine?
Angalia Historia ya Makhalifa, cha
Jalaludin Suyuti, Tafsir ya Abdassamad Clarke ya English, ukurasa wa 177 (Taha
Publishers)
No comments:
Post a Comment