6-
Qira’a: (Kusoma Suratul Fatiha, yaani: Al-Hamdu, kisha Sura yoyote).
Sura
unayoisoma lazima uisome kuanzia mwanzo hadi mwisho, hairuhusiwi kusoma sura
nusu, rakaa ya kwanza kisha kusoma nusu iliyobaki katika rakaa ya pili. Bali
inatakiwa isomwe sura kamili mwanzo hadi mwisho.
Hapa
lazima tuweke wazi: Ukichunguza swala za walio wengi ktk madh-hebu ya
Ahlus-sunna, utakuta baada ya kusoma Al-hamdu, basi mtu anasoma sura yoyote
ndefu kama Suratul-Baqarah kama Aya kumi kisha anarukuu, kisha anarudi rakaa ya
pili anasoma Aya zingine kama ishirini au kumi na tano au zozote atakazoweza
kutoka sura nyingine kama vile Suratun-Nisaa kisha anarukuu! Lakini kwa mujibu
wa mafunzo sahihi tunayofundishwa au iliyofundishwa na Maimam wetu watukufu
(a.s) kutoka Nyumba ya Mtume (s.a.w.w) ambao hakuna shaka yoyote (wala chembe
ya shaka kwamba) wanaijua vizuri zaidi swala ya Mtume (s.a.w.w), swala sahihi
lazima ktk QIRAA isomwe sura kamili ana sio nusu sura au robo yake au nusu
robo. Na hivyo ni bora mwenye kuswali au kuswali kama Imam asome sura fupi ktk
swala ambazo atakuwa na uwezo wa kuzisoma mwanzo hadi mwisho na sio kusoma sura
ndefu wakati anajua anawaongoza watu ambao wanatofautiana hali zao za kiafya
7-Dhikr
8-Tashahhud
9-Salam
10-Tartib:
(Kwa maana kwamba: Swala lazima iswaliwe kwa kufuata utaratibu huu: kuanzia Takbiratul-Ihram,
Qira’a, kisha Rukuu, kisha sujud, kisha ukae ktk rakaa ya pili baada ya sajda
usome TASHAHUD, ukimaliza ndio usimame kwa kwa ajili ya rakaa ya tatu,kisha
ukae ktk rakaa ya mwisho usome TASHAHUD, na baada ya Tashahud umalizie
kwa Salam, swala inatakiwa iwe ktk utaratibu huo au tuseme ifuate utaratibu
huo, sio unaanza na Takbiratul-Ihram, kisha unaingia sajda, unaacha qira’a na
rukuu, namna mwenye kuswali atakuwa hajafuata utaratibu, na atahesabika
anaswali anavyotaka na sio inavyotakiwa).
11-
Muwalaat: Yaani: Lazima mwenye kuswali ahakikishe anaswali swala yake
kwa kufuatanisha vitendo pasina kuacha gape au nafasi baina aya kitendo na
kitendo. Mfano: Baada ya Takbiratul-ihram, unaingia moja kwa moja kwenye Qira’a
na baada ya Qira’a Al-hamdu na sura na baada ya hapo unaingia moja kwa moja
kwenye Rukuu, namna hiyo. Hivyo haitakiwi kutoa Takbiratul-Ihram kisha kukaa
kama dakika tano kama haupo kwenye swala kisha ndio usome Al-hamdu na sura
kisha baada ya kurukuu unakaa kama dakika kumi ndio unaamua kurukuu, namna hiyo
utakuwa hujafatanisha vitendo ktk swala, bali kwa kuachanisha vitendo namna
hiyo maana ya swala inapotea kabisa na utatoka nje ya swala na kubatilisha
swala yako. Na hata kusoma sura ndefu kama vile suratul-baqara ukiig’ang’ania
mpaka uimalize hatua hiyo inaondoa kabisa ufuatanishaji wa vitendo ktk swala, na
ndio ikawa ni bora kusoma sura fupi ktk swala kwa kuzikamilisha na sio nusu
yake.
No comments:
Post a Comment