Sunday 6 August 2017

Bi KHADIKA KAMA MALKIA WA MAQRAISHI

Bi KHADIKA KAMA MALKIA WA MAQURAISHI
Assalaam Alaykum.
Khadija alikuwa mtu wa nyumbani, pia ndugu zake na binamu zake hawakupenda kusafiri na misafara. Kwa hiyo, alimuajiri wakala wakati wowote msafara ulipotoka kwenda nje (ya Hijazi), na kumfanya wakala huyo kuwa na madaraka ya kupeleka bidhaa zake kwenye masoko ya nje kuziuza huko. Kwa uwezo mzuri wa kuteua mawakala, na kununua na kuuza wakati na mahali muafaka aliweza kupata faida kubwa sana, na baadaye, akawa mfanyabiashara tajiri sana wa Makka.
Ibn Sa'ad anasema kwenye Tabqaat yake kwamba misafara ya wafanya biashara wa Makka ilipoanza safari, mzigo wa Khadija peke yake ulikuwa sawa na mizigo ya wafanyabishara wengine wote wa Qurayish katika msafara huo. Alikuwa dhahiri kwa kila mtu ni kama msemo "golden touch" ("mguso wa dhahabu") yaani kila atakacho kigusa hata kama ni vumbi litageuka kuwa dhahabu. Watu wa Makka, katika hali hiyo, walimpa jina la Malkia wa Qurayish. Aidha walimwita Malikia wa Makka.

MUBAHALA (MAAPIZANO KATI YA MTUME NA WAKRISTO)

MUBAHALA (MAAPIZANO KATI YA MTUME NA WAKRISTO)
Assalaam Alaykum.
Kabla hatujaingia ndani kuzungumzia suala la Mubahala, kwanza ni vizuri tufahamishe maana ya Mubahala. Muhabala ni: Kuapizana. Ujumbe wa Kikristo kutoka Najran ulifika kwa Mtume kujadili suala la Nabii Isa (a.s.). Mtume aliwajulisha kuwa: Hakika mfano wa Isa mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam, aliumbwa kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa naye akawa. (3:59).
Kwa kuwa Nabii Isa alizaliwa bila baba, Wakristo wamedhani kuwa baba yake ni Mwenyezi Mungu. Aya hii inaondoa dhana hiyo ambayo inapingana na utukufu wa Mwenyezi Mungu, na inawapigia mfano wa ajabu zaidi katika kuumbwa Adam bila ya baba wala mama. Aliumbwa kwa udongo kisha akaambiwa: kuwa naye akawa, na kwa neno hilo hilo Nabii Isa (a.s) ndivyo alivyoumbwa.
Ujumbe huo ulipokuwa haukukubaliana na hoja hii, Mwenyezi Mungu akateremsha Aya:- "Na atakayehojiana nawe (Muhammad) katika hili baada ya ujuzi uliokufikia, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa kunyenyekea tuijaalie laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uongo." (3:61).
Hili lilikuwa tarehe ishirini na nne mfungo tatu mwaka wa kumi. Mtume akawaita ili waanze kuapizana. Wakajibu:- "Ngojea tujadiliane". Walipokwenda faragha, wakamuuliza Askofu Abdul Masih; ana Maoni gani katika suala hili? Akajibu:- Enyi Wakristo: Wallahi nyinyi mnajua kuwa Muhammad ni Nabii aliyeletwa na amekuja na ushahidi ulio wazi juu ya jambo la huyu (Yesu a.s.). Wallahi hakuna watu walioapizana na Nabii wakasalimika, ikiwa mtaapizana naye mtaangamia".
Askofu Peter yeye aliwaambia: "Enyi Wakristo: Mimi naziona nyuso hizi (kundi la Mtume) kama zitamuomba Mwenyezi Mungu auondoe mlima kutoka mahala pake, Wallahi atauondoa. Msiapizane naye mtaangamia, na hatabaki Mkristo ye yote hapa duniani mpaka siku ya Kiama".
Alipoulizwa Ahtam, akawaambia: Niacheni nikamuulize Muhammad, alipomkabili Mtume akamuuliza, "Ewe Abulqasim'! Unatoka na kina nani kwa ajili ya maapizano haya?" Mtume (s.a.w.) akamjibu: "Ninaapizana nanyi nikiwa na watu bora hapa duniani na watukufu mno mbele ya Mwenyezi Mungu, nao ni hawa (akawaonyesha) Ali, Fatima, Hasan na Husein."
Taarifa ya kikosi hicho cha Mtume (s.a.w) ilipowafikia wakaogopa kuapizana na Mtume, na badala yake wakaomba sulhu kwa Mtume (s.a.w.) kwa kutoa dirham arobaini elfu.
TAZAMA: 
Tarikh Ibn Athir J.2 Uk. 200 
Tafsirul Qurtubi J.4 Uk. 104 
Tafsirul Ibn Kathir J.1 Uk. 376-379 
Tafsirul Khazin J.1 Uk. 359-360 
Tafsirul Maragh J.3 Uk. 175 
Tafsirul Kabir J.8 Uk. 81 
Zadul Masir J.1 UK. 399
Katika Ayatul Mubahala, iliposema:- "Tuwaite watoto wetu" Mtume (s.a.w.) alimwita: Hasan na Husein. Iliposema: "Na wanawake wetu" Mtume (s.a.w.) alimwita: "Fatima bint Muhammad". Iliposema: "Na nafsi zetu" mtume akamwita: "Ali". Kwa hivyo Ali bin Abi Talib ni nafsi ya Mtume Muhamad (s.a.w.).
Tukio hili Ia Mubahala tukilitazama kwa upande wa pili, linatukumbusha lile tukio la "KlSAA" Iliposhuka Ayatut Tat'hir:- Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kukutakaseni sana sana" (33:33). Iliposhuka Aya hii Mtume alimchukua Ali na Fatima na Hasan na Husein, akawafunika nguo kisha akasema: "Ee Mola! Hawa ni watu wa nyumba yangu, basi waondolee uchafu na uwatakase sana sana." Mama Ummu Salama (mke wa Mtume) alipotaka kuingia humo, Mtume (s.a.w.) akamzuia:
Kama ambavyo kwenye tukio la Mubahala ulipofika wakati wa kuomba maombi maalumu kwa ajili ya maapizano kati yake na Wakristo wa Najran, Mtume alimchukua Ali na Fatima na Hasan na Husein tu. Ingawa wakati huo Mtume (s.a.w.) alikuwa nao wakeze, na Masahaba ambao ni marafiki zake pia, lakini hapa hawakuingia. Wake za Mtume na Masahaba hawakuingia katika "KISAA" na hawakusimama katika uwanja wa Mubahala, kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwahusisha darja hii Ahlul Bait tu peke yao.
TAZAMA: 
Tafsirul Khazin J.3 Uk. 259 
Tafsirul Ibn Kathir J.3 Uk. 494 
Tafsirul Qurtubi J.14 Uk. 183 
Zadul Masir J.6 Uk. 381

MNAJIMU

MNAJIMU
Kiongozi wa Waumini, Ali mwana wa Abu Talib (a.s) na jeshi lake juu ya migongo ya farasi walikuwa wakaribia kuelekea Nahrwan.
Ghafla mmoja katika wafuasi wake maarufu alimjia na bwana mwingine akisema: “Ewe kiongozi wa waumini, huyu bwana ni mtabiri na ana jambo la kukueleza.” Mtabiri huyo akasema: “Ewe kiongozi wa waumini, si vizuri nyinyi kusafiri wakati huu, tafadhali subirini masaa mawili au matatu ya siku yapite kisha muendelee na safari yenu”.
“Kwa nini?”
“Kwa sababu nyota zinatuambia kuwa mtu yeyote ambaye atasafiri nyakati hizi atashindwa na adui yake. Yeye na wafuasi wake watapata shida kubwa. Lakini mkisafiri wakati ambao nimependekeza mtashinda na mtafaulu katika kufikia lengo lenu.”
Imam akasema, “Farasi wangu anatarajiwa kupata mtoto unaweza kuniambia atakayezaliwa atakuwa farasi wa kiume au wa kike?”
“Nikifanya hesabu naweza kueleza”
“Unasema uwongo, kwa wewe haiwezekani, kwa sababu imeandikwa katika Qur’an, ‘Hakuna yeyote isipokuwa Allah anayejua kuhusu mambo yaliyofichikana, na pia ni Mwenyezi Mungu peke Yake ambaye anaejua ni nini kilichobebwa (kiume ama kike) katika tumbo la mama.’ Hata Mtume wa Mungu (Muhammad (s.a.w.w) hakuwahi kudai jambo kama hili unalodai. Unadai kuwa una elimu yote kuhusu dunia hii? Na je, unajua wakati mtu ana bahati nzuri ama mbaya katika majaaliwa yake? Kama mtu yeyote anakuamini na kuamini mambo yako, basi hamhitajii Mwenyezi Mungu kabisa.”
Baada ya hayo yote imam Ali (a.s) aliwaambia wale watu wengine waliobaki: “Tambueni! Msifuate mambo kama haya, yanamfanya mtu kuamini yasiyoonekana na ni kama mtabiri ama mchawi. Na mchawi ni kafiri na kafiri ni wa motoni.”
Baada ya hayo aliziangalia mbingu na akasema maneno machache ambayo yalikuwa yanahusu imani yake kwa Allah (s.w.t).
Kisha alimwangalia yule mtabiri na akasema “Kwa makusudi nitakwenda kinyume na ushauri wako na tutaondoka sasa hivi bila kuchelewa.” Mara baada ya maneno hayo aliwaamuru wafuasi wake waanze safari.
Waliondoka kuelekea kwa maadui. Kama ilivyolinganishwa na vita vya jihad vingine, katika Jihad hii, Imam (a.s) alifaulu ajabu na kupata ushindi mkubwa.

Friday 14 July 2017

FIKRA YA KISUNNI: KHALIFA ACHAGULIWA NA WAISLAM. HIYO NDIO NJIA YA KUMPATA KHALIFA

FIKRA YA KISUNNI: KHALIFA ACHAGULIWA NA WAISLAM. HIYO NDIO NJIA YA KUMPATA KHALIFA:
SWALI KWAO:
IKIWA KHALIFA ANAPATIKANA KWA KUCHAGULIWA NA WAISLAM NA KWAMBA MTUME (S.A.W.W) AMEWAACHIA WAISLAM WACHAGUE WENYEWE WAMTAKAYE. BASI TUNAOMBA MTWAMBIE KHALIFA WENU WA PILI NI NANI ALIMCHAGUA NA KWA KIBALI GANI AU NI WAISLAM WEPI WALIOMCHAGUA. TUPENI HISTORIA YENU KUHUSU HILO?!
NDIO; TUNAKUBALI KHALIFA WENU WA KWANZA WAISLAM WALIMCHAGUA KATIKA UKUMBI WA SAQIFA KUPITIA MSHIKE MSHIKE KANGA KUCHANIKA NA KAMA MSEMAVYO KUWA HIYO NDIO NJIA SAHIHI KWENU NYINYI MNAVYOONA YA KUPATIKANA KWA KHALIFA WENU BAADA YA MTUME (S.A.W.W)!!!!. LAKINI HATUKUBALI HIVI HIVI BALI TUNAKUBALI ILI TUKUULIZENI SWALI LA KIMANTIKI: JE, HUYO KHALIFA WENU WA PILI NA WA TATU HIZO NJIA ZILIZOTUMIKA KUWATEUA KAMA MAKHALIFA ZIMEELEZWA WAPI KATIKA HISTORIA YA MAISHA YA MTUME S.A.W.W?!.
MNATIA HURUMA NDUGU ZETU, YAANI MAMBO YAPO WAZI TU LAKINI HAKUNA WA KUJIULIZA NA HAMTAKI KUJIULIZA MASWALI YA KUDADISI WALA KUJENGA FIKRA ZA KIAKILI MNAPANDIKIZWA ELIMU FEKI BILA KUJITAMBUA KUHUSIANA NA MATUKIO YA KIHISTORIA.
HEBU JIULIZENI: NI UISLAM GANI HUO AMBAO HAUNA MFUMO MMOJA WA KUPATIKA KHALIFA (YAANI YAANI KIONGOZI) WA KUWAONGOZA WAISLAM?!. MARA MNASEMA KHALIFA ANACHAGULIWA NA WAISLAM. ILI MRADI TU MTETEE UKHALIFA WA KHALIFA WENU WA KWANZA.
LAKINI KHALIFA WA PILI HAJACHAGULIWA NA WAISLAM NA MKIULIZWA NANI ALISEMA ABUBAKAR AMTEUE OMARI NDIO JAMBO ZURI KUMPATA KHALIFA. KISWAHILI KINAINGIA MFUKONI !!! MAANA TUNAWAULIZA ABUBAKAR ALIYEMTEUA SWAHIBA WAKE OMAR AWE KHALIFA (BAADA YA KUJIONA YEYE ABUBAKAR AKARIBIA KUANGAMIA) HILO LINAMFANYA AWE BORA KULIKO MTUME (S.A.W.W), MAANA YEYE KWA MTAZAMO WENU ALIUACHA UMMA HUU BILA KUUTANGAZIA NANI KHALIFA NA WASII WAKE BAADA YAKE...!!
HIVYO MNATOA MESEJI KWA KUJUA AU KWA KUTOJUA KUWA ABUBAKAR, KHALIFA WENU WA KWANZA KWA HESABU YENU NYINYI NI BORA ZAIDI YA MTUME WETU MUHAMMAD (S.A.W.W) ?! KWA KUWA KAFANYA JAMBO BORA ZAIDI, LA KUMTEUA SWAHIBA WAKE OMAR BIN KHATTABI KAMA MTU ATAKAYETAZAMA NA KUONGOZA UMMA HUU WA KIISLAM BAADA YAKE NA HILO MTUME (S.A.W.W) HAKULIONA?!!!
SUBHANNALLAH MNAMDHALILISHA MTUME WETU (S.A.W.W) NAKUMPA SIFA YA KUTOJALI WALA KUWA NA MAPENZI NA UMMA HUU NA HII IKIWA NI MATOKEO YA UJUHA WENU NA KUENDEKEZA TAASUBI ZENU MPAKA MMEKUWA VIPOFU MNAMUONA ABUBAKAR BORA KULIKO MTUME WA UISLAM (S.A.W.W)!!.
TUKIMCHUNGUZA KHALIFA WA TATU, TUNAKUTA ALIPATIKANA KWA KUTEULIWA NA WATU SITA KWA NIABA YA UMMA WA KIISLAMU. HIVI KWELI KILA KIONGOZI ANA UTARATIBU WAKE WA KUPATIKANA? JE UISLAMU HAUNA UTARATIBU WA KUPATIKANA VIONGOZI.
SISI MASHIA TUNASEMA FIKRA YENU NI POTOFU KWANI MTUME ALIACHA AMEWAPANGA SAFI NZIMA YA MAKHALIFA AMBAO NI KUMI NA MBILI, WA KWANZA WAO AKIWA NI IMAM ALLY (A.S)

USHIRIKINA NA AINA ZAKE:

USHIRIKINA NA AINA ZAKE:
Assalaam Alaykum.
Ushirikina ni wa aina mbili: Ushirikina wa wazi na ushirikina uliofichika. Ushirikina wa wazi una maana ya kumshirikisha mtu au kitu na Nafsi Kamili ya Allah au kumshirikisha na sifa Zake. Kumfanyia Allah washirika maana yake kushirikisha kitu na Upweke Wake na kuukiri ushirikishaji huu kwa ulimi, kama Sanamiyya (waabudu sanamu) au Mazorostania, ambao wanaamini katika kanuni mbili:
Nuru na giza. Wakristo pia wanafanya hivyo. Wanaamini katika utatu na kuugawanya uungu katika sehemu tatu - Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Wanaamini katika tabia tofauti za kila mmoja, na mpaka watatu hawa waungane, bila hivyo uungu wenyewe hautakuwa kamili.
Qur’ani Tukufu inakataa imani hii, na Allah (s.w.t.) anaelezea upweke wake katika maneno haya:
“Kwa hakika wamekufuru wale waliosema: Hakika Allah ni Mmoja katika watatu; hali hakuna mungu ila Allah Mmoja….” (5:73).
Kushirikisha vitu na sifa za Uungu, maana yake ni kuamini kwamba sifa Zake, kama elimu Yake au nguvu ziko tofauti na, au ni nyongeza katika Nafsi Yake Kamilifu.
Ashariyya wa Abu’l-Hasani Ali bin Ismail Ashari Basari, wanaelezewa na Maulamaa wenu wakubwa, kama Ali bin Ahmad katika kitabu chake Al-Kashf na Minhaju’l-Adilla fi Aqa’idi’l-Mila, Uk. 57 kuwa wanaamini kwamba Sifa za Allah ni nyongeza katika Nafsi Yake kamilifu, na kwamba ni za milele. Hivyo yeyote mwenye kuamini kwa njia yeyote ile kwamba tabia au sifa yeyote ya Allah ni nyongeza katika Nafsi yake kamilifu, huyo ni mshirikina.
Kila sifa Yake ni yenye asili kwake.
Ushirikina katika matendo ya mtu, ina maana kumshirikisha mtu mwingine katika Dhati Yake Yenye kujitosheleza Daima dumu.
Mayahudi wanaamini kwamba Allah aliumba viumbe na kisha akajiweka mbali na viumbe Wake. Katika kuwalaumu watu hawa, aya ifuatayuo iliteremshwa:
“Na Mayahudi wanasema: Mkono wa Allah umefungwa! Mikono yao itafungwa (kwa pingu) na watalaaniwa kwa yale wanayoyasema. Bali, mikono yake yote iwazi; Hutoa apendavyo…” (5:64).
Ghullat wanaunda kundi lingine la washirikina. Pia wao wanaitwa Mufawwiza. Wanaamini kwamba, Allah ameweka au kuaminisha Mamlaka ya mambo yote kwa Maimam watukufu. Kwa mujibu wao, Maimam ni waumbaji na pia hutupatia sisi riziki. Kwa uwazi, wale wanaomuona mtu kuwa mshirika katika Mamlaka ya Uungu ni mshirikina.
Ushirikina Katika Swala:
Ushirikina katika Sala, ina maana ya mtu kugeuza mazingatio yake wakati wa swala kwa makusudi kuelekea kwa kiumbe aliyeumbwa badala ya kuelekea kwa Allah. Kama mtu akikusudia kuomba kwa kiumbe aliyeumbwa, huyo ni mshirikina. Qur’ani Tukufu inakataza haya katika maneno haya.
“…Anayetarajia kukutana na Mola Wake, naafanye vitendo vizuri, na asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake.” (18:110).
Aya hii inaonyesha kwamba sharti la msingi wa imani ni kwamba mtu lazima afanye lolote lile ambalo ni zuri na asije kumshirikisha yeyote pamoja na Allah katika kutoa utii na ibada Kwake. Kwa maneno mengine, yule ambaye anasali au kutekeleza Hija, au kufanya kitendo chochote kizuri kwa ajili tu ya kujionyesha kwa watu uzuri wake, ni mshirikina.
Amewashirikisha wengine pamoja na Allah katika jambo la kutekeleza vitendo vyake. Kuonyesha kujikinai kwa matendo mazuri ni ushirikina mdogo, ambao hutangua vitendo vyetu vizuri.
Imepata kuelezwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Jiepusheni na ushirikina mdogo.” Watu wakamuuliza, “Ewe, Mtume wa Allah, ni nini ushirikina mdogo? Akajibu: “Al- riya wa’s-sama” (yaani, kuonyesha watu au kuwafanya wasikie juu ya ibada yako kwa Allah).
Vile vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kitu kibaya mno ninachokuhofieni kwenu ni ushirikina uliofichika; hivyo kuweni na hadhi ya juu yake kwa kuwa miongoni mwa wafuasi wangu ushirikina ni wa siri mno kuliko kutambaa kwa mdudu chungu juu ya jiwe gumu katika usiku wa giza.”
Tena alisema: “Mtu ambaye anatekeleza ibada ya Sala kwa njia ya majivuno, ni mshirikina. Mtu ambaye anafunga au kutoa sadaka au kutekeleza Hija au kumuachia mtumwa huru ili kuonyesha kwa watu uadilifu wake au kujipatia jina zuri, ni mshirikina.”
MAWAHHABI NA MASALAFI NI WASHIRIKINA KWA SABABU
1. Saudi Arabia, Israel na Marekani ni wafadhili wakubwa wa Mawahhabi na masalafi
2. Wanategemea misaada ya katika juhudi zao za kuwafitinisha waislamu, hivyo humwomba asiye kuwa Mwenyezi Mungu.
3. Katika ibada zao hufikilia namna ya kuwadhuru wanadamu badala ya kumwelekea Muumba

UBORA WA MTU MBELE YA ALLAH (S.W) UNATEGEMEA UCHAMUNGU NA SIO UKARIBU WA MTU KWA MTUME (S.A.W.W)

UBORA WA MTU MBELE YA ALLAH (S.W) UNATEGEMEA UCHAMUNGU NA SIO UKARIBU WA MTU KWA MTUME (S.A.W.W)
Kuna watu wanasema kuwa masahaba wote wa Mtume (s.a.w.w) walikuwa ni wachamungu. Sielewi labda ni kutokujua Historia yao au kutokufahamu maana ya sahaba.
Sahaba ni Mtu yeyote aliyezaliwa au kusilimu wakati Mtume (s.a.w.w) akiwa hai awe alimuona kwa macho au hakumuona kwa sababu ya upofu au umbali wa kutoka eneo analoishi huyo na eneo alilokuwa akiishi Mtume (s.a.w.w) na hivyo kusababisha wasionane kwa macho, lakini bado ni sahaba. Hii itakuwa na maana kuwa malaki ya watu waliokuwa wakiishi Uarabuni kipindi hicho walikuwa Masahaba. Wale waliozaliwa au kusilimu baada ya Mtume kufariki wanaitwa Tabiin, na kizazi kilichopatikana baada ya tabiin huitwa tabitabiin. Sasa hakuna uwezekano wa kuwasema wote kuwa wachamungu bila kuwatofautisha kulingana na matendo yao.
Jee wake wa Mtume Muhammad (s.a.w.w); hawakuwa Waislamu? Hawakuwa ma mama wa waumini? Mbona Mwenyezi Mungu amewawekea sharti ya ucha-Mungu (Sura 33:32) ndipo wapate daraja yao, kwa kuwaambia: 'Enyi wake wa Mtume! Nyinyi si kama yeyote kati ya wanawake, kama mtamcha Mwenyezi Mungu...' Hili ni kutuonyesha kwamba kama hawatakuwa na mwendo mwema (hawatamcha Mola wao), basi ile kuwa ni wake wa Mtume tu hakutawafaa kitu. Bali ikizidi, kama watafanya machafu yoyote, inatakikana adhabu yao iwe maradafu kama inavyoelezwa kwenye Sura 33:30. Na hivyo ndivyo inavyotakikana tuwe kwa masahaba.
Ili tupate mafunzo toka kwa Masahaba tunatakiwa tuchunguze mienendo yao, tutakao ona kuwa wana mienendo mizuri tuwafuate na tutakao ona kuwa wana mienendo mibaya tuambizani kukwepa kuwafuata.
Maana kama wao-waliokaa na Bwana Mtume (s.a.w.w.) na kupokea kwake maadili yote hawatatuwekea ruwaza njema, nani mwingine atatufanyia hilo? Na jee, kama hatutawatuhumu kwa yale maovu waliyoyatenda, watu wengine si watayachukulia kuwa ni mema kwa sababu tu yamefanywa na sahaba wa Mtume (s.a.w.w.), hasa kwa hivi ambavyo, Kisunni, mwendo wa baadhi ya sahaba [1] wa Bwana Mtume (s.a.w.w.) huhesabiwa kuwa ni sunna?!
Kutokana na aya mbili tatu tulizozitaja hapo juu, nataraji nimeweza kuthibitisha kwamba ule mtazamo wa kuwa sahaba wote ni waadilifu, baada ya kuambiwa kwamba sahaba ni yule aliyemwona Mtume (s.a.w.w) japo kwa mbali-na akafa ni Mwislamu, ni mtazamo unaopingana na Qur'ani Tukufu na mafunzo ya Bwana Mtume (s.a.w.w.).
Nitaendelea kutoa mada hii kuonesha kuwa imani ya kuwa Masahaba hawakosei na kwamba wote ni wachamungu unavyopingana na ukweli wa maisha yao wenyewe Masahaba. Kwa mfano masahaba walipingana vita na kuuana, hivi ni kweli kwamba aliyeua na aliyeuawa wote walikuwa wachamungu? Haitoshi baadhi ya ndugu wa Mtume ndio waliokuwa makafiri wakubwa na wakimpiga vita Mtume (s.a.ww.).
Marejeo:
[1] - Taz. uk. 74 wa Juzuu ya Nne ya al-Muwafaqat ya Shatibi.

MGOMO WA MWALIMU

MGOMO WA MWALIMU
Sayyid Jawad Amuli, alikuwa Aalimu (Faqih) mashuhuri sana, ambaye ndiye aliandika kitabu Miftahul Karamah (Kitabu maarufu sana).
Siku moja alikuwa akishughulika na kula chakula wakati aliposikia mlango ukibishwa. Mara alipojua kuwa alikuwa mfanyakazi wa mwalimu wake - Sayyid Mahdi Bahrul Uluum - haraka alifungua mlango. Mfanyakazi alimwambia, “Bwana, Mwalimu anakuita upesi. Chakula tayari kimeandaliwa mbele yake lakini hawezi kukigusa hadi ufike huko.”
Hakukuwa na muda wa kupoteza; hata kabla ya kumaliza chakula chake, Sayyid Jawad aliharakisha kwenda nyumbani kwa Sayyid Baharul-Uluum.
Punde tu mwalimu alipomwona Sayyid Jawad kwa hasira na huzuni kubwa alimwambia: “Ewe Sayyid Jawad! Wewe humwogopi Allah? Na huoni haya mbele ya Allah?”
Sayyid Jawad alipatwa na mshangao mkubwa. Alifikiria hata hivyo, ni nini kimetokea na ni tukio gani limejitokeza? Hadi kufikia wakati huu jambo kama hilo halijawahi kutokea kwamba mwalimu wake angemkaripia kiasi hicho. Alishughulisha akili yake kuweza kugundua sababu yake. Bila msaada wowote aliuliza: “Bwana wangu, kama inawezekana tafadhali nijulishe makosa yangu.”
Alijibiwa, Jirani yako fulani hakuweza kupata mchele na ngano kwa siku saba zilizopita na katika hizi siku amekuwa akila tende za kukopa kutoka kwa muuza duka ambaye yuko mwisho wa njia. Leo alipokwenda kuchukua mkopo, kabla hajauliza chochote, muuza duka alimhuzunisha kwa kumwambia: “Sasa hivi una deni kubwa sana.”
“Kwa kusikia hayo aliona haya na bila kunyanyua kichwa aliondoka na kurudi nyumbani bila ya kitu. Leo yeye na familia yake wana njaa.”
Sayyid Jawad Amuli akasema: “Wallahi naapa kuwa sikujua kuhusu jambo hili. Kama ningejua hivyo mimi bila shaka ningewasaidia.”
Mwalimu alisema: “Huzuni na hasira yangu vyote ni kwa sababu ya kutojua kwako. Zaidi ya hayo kwa nini hujui hali ya jirani yako? Na ni kwa nini wamemaliza siku saba usiku na mchana katika hali hiyo bila ya wewe kujua jambo hilo. Na kama ulijua jambo hili na ukawa hukuchukua hatua yoyote, haungechukuliwa kama Mwislamu, bali kama Myahudi.”
Sayyid Jawad akasema, “ Nieleze nifanye nini?”
Mwalimu akamjibu: “Mfanyakazi wangu atabeba sinia iliyojaa chakula. Wewe nenda naye kwenye nyumba ya yule bwana. Mfanyakazi atarudi afikapo mlangoni. Baada ya hapo utabisha mlango na uwaombe ule pamoja nao chakula chao cha usiku. Chukua hizi pesa na uziweke chini ya zulia au mkeka. Na umuombe akusamehe kwamba kwa kuwa jirani yao, hukuweza kuwajali. Iwache hii sinia hapo hapo na urudi hapa. Naketi hapa na siwezi kula chakula hiki hadi urudi na unieleze kuhusu huyo bwana mcha Mungu. “
Mfanyakazi akachukua hiyo sinia iliyojaa chakula kizuri na kufatana na Sayyid Jawad.
Walipofika karibu na mlango, mfanyakazi alirudi.
Baada ya kubisha hodi, aliingia ndani. Mwenye nyumba akamsikiza Sayyid Jawad akiomba msamaha na kwa maombi yake alikichukua chakula kutoka mikononi mwake.
Baada ya tonge la kwanza tu, aligundua kuwa hakikuwa chakula cha nyumba ya Sayyid Jawad. Mara moja aliacha kula na kusema: “Hiki chakula hakitengenezwi na mwarabu yeyote. Hivyo basi hakijatoka kwenye nyumba yako. Hadi wakati ambapo utanieleza chakula hiki kimetoka wapi ndio tutakila.
“Makisio ya yule bwana yalikuwa sawa. Chakula hicho kilikuwa kimetengenezwa nyumbani kwa Bahrul Uluum na alikuwa Muirani kutoka Burujard.
Sayyid Jawad alisisitiza kwa kusema, “Kwanini unajisumbua kutaka kujua kilipotayarishwa chakula hiki, wewe endelea chukua kula. “Lakini Bwana huyo hakukubaliana naye na akasema: “Mimi sitagusa chakula hiki hadi uniambie ukweli.”
Sayyid Jawad aliona hakuna kitakachowezekana hadi aseme ukweli. Hivyo basi akaeleza hadithi yote kutoka mwanzo hadi mwisho. Baada ya kumsikiliza Sayyid Jawad, bwana huyo alikila hicho chakula lakini alishangaa. Akasema: “Sisi hatukumueleza mtu yeyote siri hii. Bali hata hatukukubali jirani yetu wa karibu ajue kuhusu jambo hili, sijui ni vipi Sayyid alivyokuja kulijua hili.”

SABABU ZA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) KUMLEA IMAM ALLY (A.S)

SABABU ZA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) KUMLEA IMAM ALLY (A.S)
Mtume Muhammad (a.s) na mama yetu bibi Khadija (a.s) walimchukua Imam Ali (a.s) baada ya kufa kwa watoto wao wenyewe wa kiume. Kwa hiyo imam Ali aliziba uwazi katika maisha yao na kuwa kama mtoto wao wa kumzaa hasa.

Sababu nyingine ya kumchukua imam Ali na kumlea ni kumuelimisha na kumuandaa kwa ajili ya takdir kubwa iliyokuwa ikimngojea katika nyakati zijazo. Hapa ninakusudia kumwandaa kuwa kiongozi wa baadaye wa Uislam.

Kiongozi wa Uislamu ni lazima aandaliwe kiislamu, katika mazingira ya Uislamu hasa. Ni tofauti na kukurupuka na kumpa uongozi mtu asiyeandaliwa vyema. Kumpa mtu uongozi wa jambo asilolijua vyema ni kulidumaza jambo lenyewe.

Dr. Taha Hussein wa Mirsi anasema kwamba Mtume wa Allah (s.w.t.) mwenyewe alikuwa kiongozi wa Ali, mwalimu na mwelekezaji, na hii ni sifa moja nyingine zaidi ambayo anayo Ali, na ambayo hakuna mwingine yeyote anayeshirikiana naye kwayo.

 “Uislamu unaweka tamasha la maendeleo ya dini ya ulimwengu katika mwanga wa historia.” (Uislamu, 1969)
Kadhalika, inaweza kusemwa kwamba kati ya marafiki na Masahaba wote wa Muhammad, Mtume wa Uislamu, Ali ndiye pekee aliyekua katika mwanga kamili wa historia.

Hakuna sehemu ya maisha yake, ama katika uchanga wake, utoto wake, uvulana wake ujana wake, uanaume wake au kupevuka, ambayo imefichikana kutoka kwenye mwangaza wa historia. Alikuwa ndio kivutio kikuu cha macho yote tangu kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake. Kwa upande mwingine maswahaba waliobakia wa Mtume (s.a.w.) wanakuja kwenye mvuto wa nadhari ya mwanafunzi wa historia baada tu walivyokubali Uislamu, na kidogo, kama kipo, kinajulikana mpaka kufikia hapo.

Imam Ali alijaaliwa kuwa mkono wa kuume wa Uislamu, na ngao na kingio la Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) Takdira au maajaliwa yake yalikuwa kiungo kisichotenganishwa na takdira ya Uislamu, na maisha ya Mtume wake. Alikuwepo katika kila hali ya mambo katika historia ya harakati hii mpya, na alishika nafasi ya kuwa nyota ndani yake. Ilikuwa, kwa dharura, ni nafasi ambayo yeye pekee ndiye angeweza kuishika.
Aliakisi “taswira” ya mtume Muhammad (s.a.w.w). Kitabu cha Allah (s.w.t.) chenyewe kimemuita “nafsi” au mwandani (nafsi ya pili) ya Mtume Muhammad katika Aya ya 61 ya Sura ya tatu, na alionyesha jina lake maarufu toka upande mmoja hadi mwengine, wa historia.


Muundo wa ufanyaji kazi pamoja wa mtume Muhammad na imam Ali - amir na mfuasi – ulikuja kuweka “Ufalme wa Mbinguni” katika ramani ya dunia.

Monday 18 April 2016

BI KHADIJA, MADHULUMU WA HISTORIA

BI KHADIJA, MADHULUMU WA HISTORIA
Bibi Khadija alikuwa ndiye mke wa kwanza wa Mtukufu Mtume. Bibi huyu alikuwa tajiri miongomi mwa matajiri wakubwa wa Makka. Mtume alikuwa na miaka 25 alipomuoa bibi huyu, aliopofikisha miaka 40, alitoa tangazo la kwanza la utume wake, mtu wa kwamza kuamini utume wake alikuwa ni bibi Khadija, na hivyo kuamini Upweke (tawhid) wa Allah swt. Na kuwa Mwislamu wa kwanza ulimwenguni.


Waabudu masanamu wa Makka hawakufaurahishwa na tangazo hili, ukazuka uadui mkubwa sana kati ya Mtukufu Mtume na waabudu masanamu hawa. Kutokana na hali hii ilibidi Khadija atumie utajiri wake wote kuuhami Uislamu chini ya hifadhi kubwa ya ami yake Mtume, Abu Talib. Mchango wa bibi huyu ni mkubwa sana katika Uislamu, lakini bahati mbaya yeye na Bwana Abu Talib wamekuwa ni madhulumu wa historia ya Uislamu. Si wanahistoria Mustashirik tu, bali hata wanahistoria wa Kiislamu wamekwepa kuandika wasifu wake kwa ukamilifu kama ambavyo wamekwepa kuandika kwa ukamilifu wasifu wa Bwana Abu Talib na kumsingizia ukafiri.

Katika makala zangu nitakuwa nikiandika angalau kwa kiasi cha kuridhisha wasifu wa Bibi Khadija. Wasifu huu umeanzia kabla ya kuolewa na Mtukufu Mtume na baada ya kuolewa naye. Nitayaandika  matukio muhimu yanayohusiana na bibi huyu, kwa kutumia vyanzo sahihi vya Kiislamu. 

Tuesday 16 February 2016

MWENYEZI MUNGU ALIE TAKASIKA NA KUTUKUKA AMEEPUKIKA NA SIFA ZA UPUNGUFU:

MWENYEZI MUNGU ALIE TAKASIKA NA KUTUKUKA AMEEPUKIKA NA SIFA ZA UPUNGUFU: 

Mwenyezi Mungu si mwenye kiwiliwili na wala si murakkab (yaani hakuunganika kwa sehemu tofauti) hana sehemu wala mahala maalum. 

Na haiwezekani kumuona Mwenyezi Mungu mtukufu, si katika Dunia wala Akhera, na wala hatokewi na mabadiliko, hapatwi na kiu, hashikwi na njaa, hazeeki hamaliziki, hashikwi na mghafala wala kulala. Na hana mshirika wala mwenza, bali yeye ni mmoja na wa pekee, mmoja mwenye kutegemewa, hana mke wala mtoto. Na sifa zake ndio dhati yake yenyewe, hakuna uwili kati yake na sifa zake, yeye ni muweza mjuzi hadi mwisho wa sifa zake njema kuanzia tangu na tangu, si kama sisi, kwani tulikuwa ni wajinga kisha tukajifunza na hatukuwa ni wenye uwezo kisha tukawa ni wenye uwezo. 

Na yeye ni ghanii (tajiri na mwenye kujitosheleza) na hakihitajii chochote na yeyote, hahitaji ushauri wa yeyote, au msaidizi au waziri, au askari na mfano wa hayo.

ITIKADI YA KISHIA KUHUSU MUUMBA

ITIKADI YA KISHIA KUHUSU MUUMBA

Mashia wanaamini kuwepo kwa Mungu Mmoja, Mwumba wa Ulimwengu, Mwenye Kuruzuku, Mwenye Kuhuisha, Mjuzi, Muweza, Hai, Mdiriki, Mwenye enzi, Asiye na Mwanzo wala Mwisho, Msemi, Mkweli, Asiye na mwili, Asiyeonekana, Asiyebadilika, Asiye na mshirika,

Naye ni Mwadilifu katika vitendo, maamrisho na uumbaji, kama Anavyosema Mwenyewe katika Qur’an: “Hakika Mola wako si dhalimu kwa waja wake.” (Qur’an, 3:181).

MATENDO MATUKUFU KWA MUISLAMU {2}

MATENDO MATUKUFU KWA MUISLAMU {2}

Kama kweli wewe ni mwislamu wa kweli jilazimishe kuwa na matendo yafuatayo.
{1} Unyenyekevu:-
Mtume Mtukufu {s.a.w.w.} amesema: "Kwa hakika unyenyekevu humzidishia kiumbe daraja na cheo kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo nyenyekeeni, Mwenyezi Mungu atawahurumieni.

{2}Huruma na upole:
Mtukufu Mtume {s.a.w.w.} amesema: "Mwenye Imani, imechanganyika elimu yake na upole, kwani elimu bila kuwa na upole haina faida yoyote".


{3} Kukaa vyema na watu:
Amesema Imam Jaffer As-Sadiq {a.s.}:- "Muislamu ni ndugu wa Muislamu, asimdhulumu, asimdanganye, asimtupe na kumuacha, asimsengenye, asimfanyie hiyana wala asimnyime".

UMUHIMU WA MTOTO KATIKA UISLAMU KABLA YA KUZALIWA

UMUHIMU WA MTOTO KATIKA UISLAMU KABLA YA KUZALIWA

Kutilia maanani kwa Uislamu kuhusu malezi ya mtoto hakuanzii baada ya kuzaliwa tu, bali hata kabla hajaanza kupata umbo (tumboni) kwani Uislamu unamuamuru mtu kuoa mke mcha Mungu na mtulivu. Mtume (s.a.w.w) amesema: “Jitahidi umpate mke mwenye kushikamana na dini, basi furaha zote ni zako.”
Uzuri, na utajiri si sifa pekee za kutosha kuchagua mke, sambamba na sifa hizo, pia mke ni lazima awe na sifa zingine, kwa mfano kumpata aliye na dini, na awe ametoka kwenye nyumba yenye mema.
Kwa sababu watoto wake atakaowazaa mke huyo watarithi tabia, adabu na mwenendo wake. Mwenyezi Mungu amekataza kuoa mwanamke mzuri tu asiye na tabia nzuri na nidhamu. Mtume (s.a.w.) amekataza: “Jihadharini na wanawake wazuri wenye sifa mbaya.”
Mtume (s.a.w.) pia ameweka mwongozo kwa mwanamke ambaye yu tayari kuolewa: atafute mume mcha Mungu, mwenye tabia za kidini, atakayeangalia jamii yake kwa ukamilifu, kutekeleza haki za mke, na kusimamia malezi ya watoto. Mtume (s.a.w.) amesema: “Atakapowajia mtu mtakayeridhishwa na jinsi alivyoshika dini, na tabia yake, basi muozeni, ama msipofanya hivyo, mtaleta fitina na ufisadi mkubwa duniani.”
Mtume (s.a.w.) ameonya pia kuhusu kuoana na ndugu wa karibu, ili watoto wasizaliwe wadhaifu, akasema: “Oeni walio nje ya jamii yenu, msiwadhoofishe watoto wenu.”
Qur’an imetaja ya kwamba, mwanadamu ameumbwa kutokana na tone la manii lililochanganyika: “Hakika tumemuumba mwanadamu kutokana na tone la manii lililochanganyika…” (76:2).
Hii inaonyesha kwamba, mtoto azaliwaye na wazazi ambao si ndugu wa karibu atakuwa na uwerevu, utambuzi na mwenye nguvu za kimwili kuliko mtoto aliyezaliwa na wazazi wenye uhusiano wa karibu.
Hii inaweza kuonekana kwamba Uislamu umezitangulia (kwa uvumbuzi) kanuni za kisayansi na elimu ya ‘tabia zinazorithishwa’ (Heredity) kwa kuonyesha umuhimu ulioko katika sehemu ya urithi wa tabia, na namna gani uteuzi mzuri wa watu wawili wanaooana utakavyopelekea kupata watoto ambao ni tuzo la Mwenyezi Mungu na furaha ya maisha.
Kwa kuwa mtoto atachukua mwenendo wa wajomba na shangazi zake, asili ya undani ya baba yake na mama yake, na akajifunza kupitia kwa urathi ambao umepitia kutokana kwa muungano wa baba yake na mama yake, na ndipo Uislamu ukazitengeneza asili hizi kwa njia hiyo ili kumhifadhi mtoto awe ni kiumbe mwenye heshima na nidhamu, na hivyo kuepukana na upungufu wowote.
Hivyo ninawahimiza wanadamu waingie katika Uislamu makundi kwa makundi kwa sababu ndio dini pekee duniani inayokubaliana na sayansi na teknolojia. Uvumbuzi wowote uujuao umo ndani ya Qur’an, kama hujasikia masheikh wakielezea haina maana kuwa kitu hicho hakipo bali itamaanisha kuwa masheikh hawajapata uwezo wa kulifafanua jambo hilo.
Ama mtoto ni muhimu sana katika kila jamii kwa sababu ndiye atakayeshika mikoba ya kuiongoza jamii. Endapo kama mtoto huyu asipoandaliwa vyema jamii nzima huharibika na kupoteza uelekeo.

Monday 15 February 2016

MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU

MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
Assalaam alaykum:
Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika uislamu inaonekana katika maeneo yafuatayo:
Kwanza, Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.Tunajifunza katika Qur’an kuwa jambo la kwanza alilotunukiwa Adam (a.s) mara tu baada ya kuumbwa kwake ni kupewa elimu. "Na (Mwenyezi Mungu) akamfundisha Adam majina ya vitu vyote..." (2:31) "Majina ya vitu vyote" katika aya hii inaashiria fani zote za elimu ambazo anahitajia mwanaadamu hapa duniani ili afikie kwa ufanisi lengo la kuumbwa kwake. Pia tunajifunza katika Quran kuwa mwenye elimu na hekima amepewa kheri nyingi. (Mungu) humpa hekima amtakaye, na aliyepewa hekima bila shaka amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili. (2.269).

Kutafuta elimu (kusoma) ni amri ya kwanza kwa mwanaadamu. Tunajifunza kutokana na historia ya kushushwa Qur’an kuwa Wahay wa kwanza kumshukia Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambao ndio ulimtawazisha rasmi kuwa mtume ni ule unaopatikana katika aya tano za mwanzo za Suratul-'Alaq:
"Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba. Ambaye amemuumba mwanaadamu kwa 'Alaq (kitu chenye kuning'inia). Soma na Mola wako ni mkarimu sana. Ambaye amemfundisha mwanaadamu kwa kalamu. Amemfundisha mwanaadamu (chungu ya) mambo aliyokuwa hayajui".(96:1-5)
Kutokana na aya hizi, kwa muhtasari, tunajifunza yafuatayo:
1. Kusoma kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni jambo la kwanza waliloamrishwa wanaadamu na Mola wao.
2. Kusoma kwa jina la Mola wako ni kusoma kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu au ili kuweza kumwabudu Allah(s.w) inavyostahiki na kusimamisha Uislamu katika jamii.
3. Radhi za Mwenyezi Mungu zitapatikana pale mwanaadamu atakapoweza kufikia lengo la maisha yake la kumuabudu Allah (s.w) kwa kuzingatia maamrisho na mipaka ya Mwenyezi Mungu katika kila kipengele cha maisha.
4. Amri hii ya kusoma hailengi fani maalumu tu ya elimu; bali kila fani itakayomuwezesha mwanaadamu kufikia lengo la maisha yake kwa ufanisi.
5. Chanzo au chimbuko la fani zote za elimu ni Allah (s.w). Hivyo kwa Muislamu mlango wa kwanza wa elimu ni kusoma kwa mazingatio Qur’an na hadithi sahihi za Mtume (s.a.w) na kusoma maarifa ya Uislamu kwa ujumla kutokana na vyanzo hivi viwili.

Hivyo basi ninawahimiza waislamu wasome elimu zote tena kwa pupa kwa sababu hiyo ni moja ya ibada kubwa zitakazo tupelekea kuzawadia pepo ya milele kama malipo yetu ya kutenda mema hapa duniani.


Kwa hiyo tuwapuuzie wale wote wanaodai kuwa ni masheikh halafu kazi zao ni kuwazuia waislamu kujifunza elimu kadhaa wakidai kuwa ni za kimagharibi na zisizo na faida. Watu hawa ni wapotoshaji walio na lengo la kuwafanya waislamu tubaki nyuma kimaendeleo.

MATENDO YA MASAHABA KUHUSU SUNNAH

MATENDO YA MASAHABA KUHUSU SUNNAH
Ni jambo maarufu pia kwamba mengi katika matendo ya Masahaba baada ya Mtume (s.a.w.) yalikuwa kinyume cha Sunna yake, kwa hiyo imma Masahaba hawa walikuwa wanaifahamu Sunna ya Mtume (s.a.w.) na waliikhalifu kwa makusudi kutokana na ijtihadi zao dhidi ya Nassi (matamko, matendo na iqrari) za Mtume (s.a.w.), na kwa ajili hiyo Masahaba hawa inawakumba kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu pale aliposema: "Haiwi kwa Muumini wa kiume wala Muumini wa kike Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapoamua jambo wao wawe na hiyari katika jambo lao, na yeyote mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotevu ulio wazi." (Qur'an, 33:36)

Na labda (tuseme) walikuwa hawaijui Sunna ya Mtume (s.a.w.), kwani haistahiki kabisa kwa Mtume (s.a.w.) katika hali kama hii kuwaambia Masahaba wake nimekuachieni Sunna yangu hali yakuwa yeye Mtume anajua kwamba Masahaba wake ambao ni watu wa karibu mno kwake hawaifahamu Sunna yake, basi hali itakuwaje kwa watakaokuja baada yao wakati hata Mtume hawakumfahamu na wala hawakumuona?

Inafahamika pia kwamba Sunna ya Mtume haikuandikwa isipokuwa katika zama za dola ya Bani Abbas, na kwamba kitabu cha mwanzo kilichoandikwa kuhusu hadithi ni "Muwataa" cha Imam Malik, na hiyo ni baada ya fitna kubwa (kupita) baada ya tukio la Karbala na kushambuliwa mji wa Madina, kisha kuuawa kwa Masahaba hapo mjini Madina. Basi ni vipi baada ya matukio hayo mtu atakosa kuwatilia mashaka wasimulizi wa hadithi (za Mtume) ambao walijipendekeza kwa watawala ili waipate dunia? Kwa ajili hiyo hadithi za (Mtume) zimevurugika na kupingana zenyewe kwa zenyewe, nao umma wa Kiislamu umegawanyika kwenye Madhehebu mengi (kiasi kwamba) jambo ambalo limethibiti kwenye madhehebu haya, kwenye madhehebu mengine halikuthibiti, na kitu ambacho kwa hawa wanakiona ni sahihi, wale wanakipinga.
Ni vipi tutaamini kamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema kuwa "Nimekuachieni kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna yangu, na hali ya kuwa yeye anafahamu kwamba wanafiki na wapinzani watakuja mzulia?

Hapana shaka Mtume (s.a.w.) alipata kusema,"Wako wengi wenye kunizulia, basi yeyote mwenye kunizulia na ajiandalie makazi yake motoni".
Hivyo basi iwapo wazushi walikuwa wengi katika zama za uhai wake, ni vipi Mtume aulazimishe umma wake kufuata Sunna yake na hali hawaifahamu Sunna iliyo sahihi kutokana na ile isiyo sahihi na dhaifu kutokana na ile yenye nguvu?

Katika hali hii endapo kama Mtume angekuwa ametuachia Qur’an na Sunnah pekee ndio miongozo yetu, basi tungeangukia pua kwa sababu licha ya Qur’an kuwa haina shaka lakini mwenziwe amesheheni uongo na uzushi kiasi kwamba hatuwezi kutofautisha kati ya Sunnah na uongo.
Alhamdulillah baadhi ya waislamu tumeligundua hilo na kuchukua hatua, nayo sio nyingine bali kushikamana na Ahlulbayt wa Mtume ili watuonyeshe Sunnah sahihi kwa sababu Mtume amesema watu hawa wako pamoja na haki na haki iko pamoja nao. 

Monday 16 November 2015

BINTI WA NABII MUHAMMAD (s.a.w.w.)

BINTI WA NABII MUHAMMAD (s.a.w.w.)

Yeye  ni  Fatima  Zahra; Baba yake ni Rasulullah (Mjumbe na Mtume wake Mwenyezi Mungu) Muhammad bin Abdullah (s.a.w.w.); na mama yake ni Bibi Mtukufu Khadija Mama wa Waislamu, na mumewe ni bwana wa mawasii Ali Ameerul-Muuminiin, na watoto wake na wajukuze ni maimam watoharifu (juu yao Rehma na Amani).
Alizaliwa Bibi Fatima (a.s.) siku ya mwezi ishirini, mwezi wa mfungo tisa, mwaka wa arobaini na tano toka alipozaliwa Mtume (s.a.w.w).
Na akafa bibi huyo siku ya Jumanne mwezi tatu, mfungo tisa, mwaka wa kumi na moja wa Hijiria [5]. Na umri wake ni miaka kumi nanane.
Na akasimamia matendo ya kifo chake Amirul Muminiin Ali (a.s.), akamzika Madina Munawwara (Mji wenye nuru, mji wake Mtume, uliopo katika Saudia Arabia), na akalificha kaburi lake kama alivyo usia mwenyewe Bibi Fatima.
Alikuwa bibi huyo kama baba yake kwa ibada na kumcha Mungu na ubora, na zimeshuka katika sifa zake aya nyingi za Qur'ani al-Hakim.
Alikuwa Mtume (s.a.w.w.) akimwita "Bibi wa wanawake wa Ulimwenguni", na akimpenda mapenzi mazuri mpaka yeye akiwa anaingia kwa Mtume (s.a.w.w.) humkaribisha na kusimama na kumkalisha mahali pake, pengine humbusu mikono yake.
Na Mtume (s.a.w.w.) akasema: "Mungu huridhika analoridhika nalo Fatima na hukasirika Unalo mkasirisha Fatima."
Pia Mtukufu Mtume amesema: "Wabora wa wanawake wa peponi ni wanne: Mariam Binti Imrani, na Khadija Binti Khuwailid, na Fatima Binti Muhammad (s.a.w.w.) na Asia Bint Muzaahim.
Mtu mmoja akamwuliza bibi Aaisha "Mtu gani alikuwa mpenzi mno wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Akajibu: Fatima.
Kisha akamwuliza: Ni gani kutokana na wanaume? Akajibu: Mume wake Bibi Fatima, yaani Ali bin Abi Talib (as.).
Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) akasema: "Hakika, Mwenyezi Mungu ameniamrisha mimi nimwoze Fatima kwa Ali (a.s.).
Kazaa bibi huyo kwa Amirul Muuminiin Ali (a.s.): Imam Hassan (a.s.), Imam Hussein (a.s.), Bibi Zainab (a.s.), Bibi Ummu Kulthum (a.s.) na Muhsin (a.s.)- Lakini bwana Muhsin kafa tumboni zama alipopata mama yake msukosuko wa maadui. Kwa hiyo jumla ya watoto wa bibi Fatima ni 5.
Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) amesema: "Kila mtoto huchukuwa ukoo wa baba yake isipokuwa vizazi vya Fatima, kwani mimi ndiyo walii wao na nasaba wao (yaani, vizazi vya Fatima wote ukoo wao unatokana kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Pia Mtume Mtukufu amesema:- "Kila ukoo na uhusiano utafutika siku ya qiyama isipokuwa ukoowangu na uhusiano wangu.

JANNAT AU PEPO

JANNAT AU PEPO
Assalaam alaykum.
Jannat ni mahala pema kabisa ambapo Allah (s.w) amewaandalia watendao mema na kujiepusha na maovu.
Katika ukurasa wa 279, juzuu 13 ya kitabu Lisan al-'Arab, twaambiwa kuwa pepo inaitwa Jannat 'Adan ikimaanisha kuwa ni "Mahala pa milele", Bustani ya Kati (al-awsat)."
Kitabu hichohicho kinatutambulisha katika uk.427, juzuu ya 7 kuwa al-awsat inaweza kumaanisha kuwa: iliyo Bora. Hakuna shaka kuwa tutaweza kuona na kupata maelezo na mafafanuzi zaidi juu ya Jannat 'adan kuliko kusema tu al-firdows, Jannat au Peponi, katika Qur'an Tukufu. Hali hii inatuacha sisi kwa kudadisi kuwa mahala bora kabisa, na iliyokuu, inayolengwa katika Jannat zote ni Jannat 'Adan.
Peponi, au al-Firdows kama vile inavyoitwa katika Kiarabu, ni neno la kuazimwa. Waarabu aliowatokezea Mtume Muhammad (s.a.w.w.) walikuwa hawana itikadi ya maisha baada ya kufa, na Jannat na Jahannam. Na kwa hakika swala hili lilikuwa gumu kwake Mtume (s.a.w.w.) alipoanza kuhubiri. Sura-i-Yasin, 36, Ayah ya 78 inatuelezea, 'Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake - akasema: "Nani atakayeihuisha mifupa na hali imesagika?"
Vile vile Qur'an inatujibu katika, Sura Ya-Sin, 36; Ayah 79: Sema: "Ataihuisha yule aliyeiumba mara ya kwanza, naye ni Mjuzi wa kila (namna ya) kuumba"
Hata mwandishi wa kazi nzuri kabisa za Kiarabu, Lisan Al-'Arab, hana uhakika iwapo neno hili la Firdaws limeazimwa kutoka Kilatini au Kiajemi, au ni al-Majlisi, kama mwandishi huyo anavyokubali katika uk. 91, Juzuu ya 8 kati ya Juzuu 110 ya Encyclopedia - bila ya kuihesabu Juzuu ya Sifuri - ijulikanayo kwa jina la Bihar al-Anwar. Wazo la tatu, ambalo linaweza kuwa sahihi zaidi ni kwamba inawezekana uasili wake ukawa Babilonia.
Neno lingine lililotumika katika Qur'an Tukufu ni Jannat au Bustani. Lakini kwetu sisi Jannat inamaanisha sana kuliko kutaja Bustani au shamba la miti ya matunda. Waarabu kamwe hawakuwa na tabia ya kuishi katika mshamba yao ya miti ya matunda.
Mtume (s.a.w.w) anasema, "Wakati Allah (sw) aliponiruhusu kwenda Jannat, Jibrail a.s. aliniambia, "Mimi nimeamrishwa kukutembeza na kukuonyesha yote yaliyomo ndani mwa Jannat na Jahannam." Hivyo mimi niliiona Jannat na baraka na mema yote yaliyokuwamo na vile vile nimeiona Jahannam pamoja na mateso yote yaliyomo. Jannat inayo milango minane, kila mlango unayo misemo minne, ambayo kila mojawapo ni bora kuliko ulimwengu mzima na kile ambacho kipo ndani mwake ni kwa ajili ya wale wanaotafakari na kufuatilia kwa kutenda kimatendo.
Na Jahannam inayo milango saba, na kila mlango inayo misemo mitatu, ambapo kila msemo ni afadhali kuliko dunia yetu hii na kilichomo ndani mwa kila msemo ni kwa ajili ya kutafakari na kuyatendea kazi. Malaika Jibraili (a.s.) aliniambia, "Ewe Muhammad! Soma yaliyoandikwa katika milango hii!" Na hivyo mimi niliyasoma yote.
Ufafanuzi zaidi utakujia baadaye Insha – Allah

Thursday 12 November 2015

HALI NA HAKI ZA MTOTO KATIKA UISLAMU

HALI NA HAKI ZA MTOTO KATIKA UISLAMU
Umoja wa mataifa umeanza kuonyesha kuvutiwa na suala la watoto kwa kufanya maadhimisho ya ‘Siku ya Watoto’ katika mwezi wa Novemba kila mwaka, ambayo inalingana na maadhimisho ya kutangazwa kwa haki za mtoto.
Ukweli ni kuwa mazingatio ya Uislamu kwa watoto yameanza zamani na yanarejea nyuma zaidi ya miaka elfu moja na mia nne.
Uislamu kwa mfululizo unaadhimisha na kuonyesha huruma yake kwa mtoto, si baada ya kuzaliwa tu, bali hata kabla ya kuzaliwa, na umeelezewa kwa makini haki zake.
Wakati wa utoto katika Uislamu umepewa picha ya ulimwengu mzuri wa furaha, uzuri, ndoto, mapenzi na ndoto njema.
Na aya za Qur’ani zinaonyesha mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa watoto, na ndipo akaapa Mwenyezi Mungu: “Naapa kwa mji huu, (wa Makkah).  Na wewe utahalalishwa katika mji huu. Na (kwa) mzazi na alichokizaa.” (90:1-3).
Watoto wameelezwa katika Qur’ani kuwa ni bishara njema. Amesema Mwenyezi Mungu:
 “Ewe Zakaria tunakupa habari njema ya (kupata) mtoto jina lake ni Yahya….” (19:7).
Pia watoto ni kiburudisho cha macho yetu. Amesema Mwenyezi Mungu:
 “Ewe Mola wetu, tupe katika wake zetu na watoto wetu watakaoyaburudisha macho yetu….”(25:74).
Na watoto ni pambo la maisha katika ulimwengu huu: “Mali na watoto ni pambo la maisha ya duniani….” (18:16).
Mtume (s.a.w.) anatudhihirishia ya kuwa ulimwengu wa utoto ni kama pepo, pale aliposema: “Watoto ni vipepeo vya Peponi.”
Kuwatunza watoto ni jambo la lazima, na kuwapenda humleta mtu karibu na Mwenyezi Mungu. Mtume (s.a.w.) amesema: “Lau kama si watoto wanyonyeshwao, na wazee wanaorukuu (kwa kuswali) na wanyama walishwao mashambani, basi mngelipatwa na adhabu kali.”
Inaonyesha wazi kwamba huruma na uangalifu wa Mwenyezi Mungu kwa watoto ndiyo uliofanya Mwenyezi Mungu kuzuia adhabu juu ya watu wake.
  1. Mapenzi Ya Mtume Kwa Watoto
Mapenzi ya Mtume (s.a.w.) kwa watoto yalijaa ndani ya moyo wake mwema, imeelezwa katika Hadith: “Siku moja Mtume (s.a.w.) alipanda juu ya mimbari akiwahutubia watu, (mara) akawaona Hasan na Husein (a.s.) wanakimbia na huku wakijikwaa, akakatiza hotuba yake, akashuka kutoka juu ya mimbari kwenda kuwapokea watoto hao wawili. Akawabeba mikononi mwake, kisha akapanda tena juu ya mimbari akasema: “Enyi watu, hakika mali zenu na watoto wenu ni fitina, Wallahi nimewaona wajukuu wangu wawili wakikimbia na kujikwaa, basi sikuweza kujizuia mpaka nimeshuka nikawabeba.”
Siku moja Mtume (s.a.w.) alikuwa anaswali, mara Hasan na Husein (a.s.) wakaingia ndani na kumpanda mgongoni kwake wakati alipokuwa amesujudu, Mtume (s.a.w.) akaendelea kusujudu tu. Alichukia kuwaharakisha washuke, mpaka waliposhuka wao wenyewe. Kisha alipotoa salaam na kumaliza Swala, akaulizwa na maswahaba wake sababu zilizomfanya asujudu kwa kitambo kirefu hivyo; akawajibu: “Wajukuu wangu wawili walikuwa wamepanda juu ya mgongo wangu nami nilichukia kuwahimiza washuke kwa haraka.”
Mtume (s.a.w.) alizoea kuharakisha Swala yake pindi asikiapo mtoto analia, na husema: “Mimi huchukia kumchosha mama yake.”
Siku moja alikuwa anapita nyumbani kwa Fatima (a.s.) (binti yake), akamsikia mjukuu wake Husein (a.s.) akilia, aliingia ndani na baada ya kumkemea Fatima akasema: “Je hujui kwamba nimsikiapo Husein akilia huwa nakereka?”
Siku moja Mtume (s.a.w.) alitembelewa na Al-Akraa Ibn Habis, ambaye alimwona Mtume (s.a.w.) akiwabusu wajukuu zake, Al-Akraa akasema: “Unawabusu watoto wa binti yako? Naapa kwa Mungu nina watoto kumi, na sijawahi kumbusu hata mmoja.”
Mtume (s.a.w.) akamjibu: “Je ni kosa langu kama Mwenyezi Mungu ameing’oa rehma kutoka moyoni mwako.”

Thursday 29 October 2015

MAWAHHABI WAMDHALILISHA MTUME KUWA HAKUJIELEWA KUWA YEYE NI MTUME

MAWAHHABI WAMDHALILISHA MTUME KUWA HAKUJIELEWA KUWA YEYE NI MTUME
Waandishi wa kiwahhabi wameeleza suala la mwanzo wa wahyi kwa njia nyingi tofauti zenye kugongana. Tunakusudia kudondoa kilitokea nini kwa Mtume Muhammad (sa.w.w) baada ya kufikiwa na malaika Jibril kwa mara ya kwanza. Hapa tutajaribu kuzitaja chache tu:
a.  Khadija na Abubakr walimpeleka Muhammad (s.a.w.) kwa Waraqa bin Nawfal baada ya kuelezwa Waraqa kuwa Muhammad amepata matatizo, Waraqa akamuuliza Muhammad ana nini? Muhammad (s.a.w.) akamwambia: "Ninasikia ninaitwa nyuma yangu, ewe Muhammad, ewe Muhammad, nikisikia hivyo mimi hukimbia ovyo." Waraqa akamkataza asiwe anakimbia bali akaze roho ili ayasikie anayoambiwa..." Muhammad alishika maelekezo hayo, mara aliposikia akiitwa: Ewe Muhammad! Sema, Bismillahir Rahmanir Rahim, Alhamdulillahi rabbil a'lamina.... mpaka mwisho wa suratul Fatiha. Akaambiwa: Sema: "Laa ilaha illallahu" Muhammad (s.a.w.) baada ya hapo alikwenda kwa Waraqa bin Nawfal, akamjulisha hali hiyo. Waraqa akambashiria habari njema ya kuwa: "Hali kama hiyo alipewa pia Nabii Isa bin Maryam".
Tazama; Albidayatu Wannihaya J. 3 Uk. 9, Assiratun Nabawiyya J. 1 uk 83, Assiratul Halabiyya J. 1 uk 250, Siiratu Mughlataya uk, 15.
b.  Khadija alipompeleka Muhammad (s.a.w.) kwa Waraqa na akamweleza yaliyomtokea. Waraqa alisema: "Huyu ni Nabii wa Umma huu, mwambie atulize moyo."
Tazama: Albidayatu Wannihaya J.3 uk, 12, Siiratu Ibn Hisham J. 1 uk. 238, Assiratul Halabiyya J. 1 Uk. 239.
c.   Khadija alimwambia Muhammad (s.a.w.) atakapokufikia huyo anayekusomesha, uniambie, Mtume (s.a.w.) alipofikiwa na hali hiyo akamjulisha mkewe. Khadija akampakata katika mapaja yake, kisha akavua shungi yake, mara Mtume (s.a.w.) akaona yule aliyemjia anaondoka haraka. Mtume akamjulisha mkewe hilo, Khadija akasema, "Huyo ni Malaika, na wala siyo shetani, basi kaza roho na furahi".
Tazama: Assiratul Halabiyya J. 1 Uk. 252.
d.  Waraqa bin Nawfal alimwambia Khadija: "Muulize Muhammad (s.a.w.), nani anaemjia! Ikiwa ni Malaika Mikaeli basi amemletea amani. Na ikiwa ni Malaika Jibril basi amemletea vita na mateka. Khadija Alipomuuliza Mtume (s.a.w.) akajibu: "Ni Jibril". Khadija akapiga uso wake.
Taz: Tarikhul Yaa'quby J. 2 Uk. 23.
e.  Khadija alipewa kipande cha karatasi na mganga mmoja ili ampe Muhammad (s.a.w.) kama hali hii (iliyomfikia Muhammad) inasababishwa na ugonjwa wa kichaa, basi atapona... Khadija aliporudi kwa mumewe akamkuta anasoma Qur'an, Khadija akamchukua akaenda naye kwa yule mganga, walipofika kwa mganga, akafunua mgongo wa Mtume akaona muhuri wa Utume uko kati ya mabega mawili!!!
Tazama: Tarikhul Khamisi J. 1 Uk. 284, Assiratul Halabiyya J. 1 Uk. 243, Assiratun Nabawiyya J. 1. Uk. 83.
f.    Muhammad (s.a.w.) alipofikiwa na hali hiyo (ya kujiwa na Malaika) alikuwa akipanda katika kilele cha mlima mrefu na akitaka kujitupa chini (ili afe).
Tazama: Almuswannaf J. 5 Uk. 323.
g.  Muhammad (s.a.w.) alirudi kwa mkewe (kutoka katika pango) akiwa nafuraha kubwa akamwambia mkewe: "Nataka kukueleza habari njema, mimi nimeona katika ndoto kuwa Jibril amenijulisha kwamba ametumwa na Mola wangu aje kwangu... Khadija akamwambia: "Furahi, wallahi Mwenyeezi Mungu hatakufanyia lolote ila lililokuwa la kheri... kisha Khadija akaenda kwa mganga wa kinasara, kuuliza uwezekano wa kumuona Jibril. Mganga alishangaa sana kusikia jina la Jibril katika nchi hiyo, kisha akasema kuwa: "Huyo ni Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu..."
Taz: Albidayatu Wannihaya J. 3 Uk. 13.

Nadhani umejionea mwenyewe uzushi wa mawahhabi, masalafi na answari sunnah dhidi ya Mtume wetu. Watu waongo na wazushi kama hawa, hawawezi kuaacha waislamu wa kawaida wakiishi kwa amani mustarehe bila kuleta chokochoko.

Lakini sisi waislamu sahihi, yaani Mashia tunaamini kuwa Mtume alikuwa Mtume bado akiwa tumboni mwa mama yake. Hivyo alipozaliwa tu alijulikana kuwa ni Mtume na miujiza mingi ilifanyika katika utoto wake na ujana wake. Kabla ya kufikisha miaka 40 ambapo utume wake ulizinduliwa rasmi na kuanza kazi ya kuueneza Uislamu duniani.

Monday 19 October 2015

WAATHIRIKA WA KARBALA – AWN BIN JAAFAR IBN ABI TALIB (R.A)

WAATHIRIKA WA KARBALA – AWN BIN JAAFAR IBN ABI TALIB (R.A)
Aun ni mtoto wa Jaafar ibn Abi Talib (r.a) na Asma’a bint Amees (r.a)..
Alizaliwa ukimbizini Ethiopia (Uhabeshi) kwani baba yake yaani Jaafar alikuwa kiongozi wa wakimbizi wa kiislamu waliokimbilia Habash kutokana na dhuluma na mauaji waliokuwa akifanyiwa na makafiri wa Makkah wakati wa mwanzo wa Uislamu kutangazwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Uislamu ulipota nguvu baba wa Aun yaani Jaafar alirejea uarabuni na kwa kipindi hicho Mtume alikuwa amekwisha hamia Madinah. Miaka michache baadaye Jaafar aliongoza jeshi la waislamu katika mapambano yanayojulikana kama vita vya Mu’tah. Vita hivi vilikuwa vikali sana na waislamu wengi waliuawa ikiwa ni pamoja na kamanda wao, yaani Jaafar bin Abi Talib (r.a). Jaafar aliacha watoto wa kiume watatu yaani Awn, Muhammad na Abdullah.
Vijana hawa walifanana sana na mzee Abu Talib (r.a), hivyo Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Imam Ally waliwapenda sana. Baadaye Imam Ally aliwaozesha mabinti wake. Ummu kulthumu aliolewa na Aun na Zainabu aliolewa na Muhammad. Hapa utagundua kuwa wale wanaosema kuwa Imam Ally waliwaozesha mabinti wake kwa Umar bin Khatab ni uongo na propaganda kwa minajiri ya kuwapotosha watu.
Awn aliendelea kuwa Mtiifu kwa Imam Ally kama imam wake wa kwanza, kisha akawa mtiifu kwa Imam Hassan kama imam wake wa pili na hatimaye akawa mtiifu kwa imam Hussein kama imam wake wa tatu. Awn alichinjwa pamoja na Mashia na Ahlulbayt wengine katika eneo la Karbala, Iraq, akipigana vita upande wa Mashia, yaani katika jeshi dogo la imam Hussein (a.s). Innalillahi wainna ilayhi rajiuun.
Source: Ashura Encyclopedia

By Jawad Muhaddithy 

Monday 12 October 2015

QURANI MUUJIZA WA MILELE QUR ANI WA MTUME (S.A.W)

QURANI MUUJIZA WA MILELE QUR ANI WA MTUME (S.A.W) 
Qur'ani ni muujiza wa Mtume (s.a.w) ulio hai na wa milele, kwani Qur'ani ndio kitabu pekee kutoka mbinguni ambacho utashi wa Mwenyezi Mungu ulitaka kibakie ni chenye kuhifadhiwa kutokana na mabadiliko, nyongeza, pia upungufu na kugeuzwa- pamoja na kukithiri kwa watu wenye nia na malengo ya kukibadilisha na wafanyao mipango ya kukizua na kukigeuza- ili kitabu hiki kiwe cha milele na katiba ya milele ya maisha hadi siku ya kiama, maadamu kuna mwanadamu anaye ishi juu ya ardhi hii na hilo ni kutokana na hukumu za hali ya juu zilizomo kwenye majalada yake mawili na mafunzo ya kiwango cha juu ambayo kuyatekeleza kwake yana mhakikishia mwanadamu saada na kumpatia maendeleo, kupea na kufikia kwenye daraja za juu mwanadamu huyo.
Hakika Qur'ani pamoja na kuwa ni kitabu cha kielimu, utamaduni hukumu, haki, maadili, adabu, siasa na uchumi, ni muujiza wa mbinguni na wa milele wenye athari kubwa ya kiroho na kimaaanawia ya hali ya juu, hakika kitabu hiki kiliwashinda wanafasaha wakubwa wa kiarabu waliokuwa na nyaraka au waandishi wa nyaraka saba zilizo kuwa zimetundikwa na kuwekwa kwenye kaaba tukufu, na hawakuweza kuleta mfano wa sura moja tu ya Qur'ani, bali kutokana na kushikwa na aibu walikuwa wakizitoa nyaraka walizo tundika juu ya kaaba kati ya zile nyaraka zao, na walifanya hivyo kutokana na kushindwa kwao na kudhalilika kwao, pia kutokana na aibu iliyo washika mbele ya Qur'ani ambayo ni muujiza katika fasaha na balagha yake na katika mfumo wake na utaratibu wake, na lau kama wangeliweza kuleta sura moja tu mfano wa Qur'ani kusinge kuwa na haja ya kutumia mapigano dhidi ya Uislamu na vile vita vibaya na vyenye kuangamiza ambavyo viliishia kuleta maafa kwao na waheshimiwa wao na watu wao na kuvunja utukufu na heshima zao na hadhi zao, pia utawala wao, na kuwavisha vazi la njaa, khofu, udhalili na taabu.
Hii ndio Qur'ani ambayo ni muujiza, na hiki ndio kitabu cha mbinguni cha milele, kitabu ambacho ndani yake kuna mambo yamfikishayo mwanadamu kwenye saada na maisha ya neema na raha, kitabu ambacho hueneza kheri na baraka kwa watu wote, na hutawanya amani na salama katika ardhi hii na katika nchii zote, kumepokelewa riwaya mbali mbali kuhusiana na ubora wa kujifunza kitabu hiki na kukisoma pia kukihifadhi na kutekeleza maamrisho yake, na kufanya matendo kwa mujibu wa maamrisho ya kitabu hicho na zingine nyingi ambazo zinazo muhimiza mwanadamu kukitilia umuhimu.