Saturday, 31 August 2013

UPOTOFU WA MAWAHHABI



Mawahhabi wanadai kuwa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab alikuwa akihubiri mawazo yake kwa ajili ya kujipatia utukufu katika imani yake katika upweke wa Allah swt na kuwakomboa Waislamu wasitumbukie katika Shirk.  Wao wanadai kuwa Waislamu wamekuwa wakitenda dhambi ya Shirk kwa karne sita mfululizo na hivyo yeye alikuja kuirejesha upya dini ya Uislamu. Yeye anazitoa Ayah za Qur’an Tukufu nambari 5 ya Surah al-Ahqaf, Ayah 106 surah  Yunus, Ayah 14 sura al-Ra’d ili kwamba Waislamu wote wakubaliane na mawazo yake. Hata hivyo, zipo Ayah nyingi kama hizo, na Maulamaa wanasema kuwa hizo Ayah zimekuwa zikiwazungumzia makafiri waliokuwa wakiabudu miungu na masanamu au waliokuwa washirikina.

Kwa mujibu wa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab, Mwislamu anakuwa Mushrik pale anapoomba kwa Mtume Muhammad s.a.w.w, au kwa Mtume a.s. mwingine, au walii au mcha Mungu karibu na kaburi au mbali kutoka hapo, yaani, iwapo anapomwomba msaada wa kutokana na shida aliyonayo, au anapoomba kutetewa mbele ya Allah swt kwa kutaja jina  lake au anapotaka kuzuru kaburi lake.  Allah swt anatuambia  kuhusu makafiri wanaoabudu miungu na masanamu katika Ayah ya tatu ya surah al-Zumar, lakini Mawahhabi wanaonyesha Ayah hii kama ndio waraka wa kuhalalisha utumiaji wao wa neno la Mushrik kwa ajili ya Waislamu waombao kwa kuwaweka Mitume a.s. au Mawalii kama ndio watu walio baina yao na Allah swt.  Wao wanasema kuwa hata Mushrik waliokuwa wakiabudu miungu pia walikuwa wakijua kuwa vyote vilikuwa vimeumbwa na Allah swt. Wao wanasema kuwa Allah swt amebainisha:  Na kama ukiwauliza, Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi na akalitiisha jua na mwezi?” Bila shaka watasema, Allah (Surah Ankabut, ayah ya 61 na Sura Zukhruf, Aya ya 87). Wao wanadai kuwa hao Mushrik walikuwa hivyo makafiri Mushrik si kwa sababu walikuwa wakiamini hivyo bali wao walizungumza kama ilivyosemwa katika Ayah ya 3 ya Surah az-Zumar: Wale wanaofanya wengine kuwa marafiki badala ya Allah, wanasema, “Wao wanatusaidia kutufikisha karibu (ya Allah swt) kwa kututetea mbele Allah” Wao wanadai kuwa Waislamu wanaoomba katika makaburi ya Mitume, ma-Awliya’ kwa utetezi na misaada basi wanakuwa Mushrik kwa kusema hivyo.

Ni jambo la kipumbavu kabisa kwa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab kuwasema Waislamu wanakuwa makafiri na Mushrik kwa Ayah hiyo. Kwa sababu, makafiri wanawaambudu masanamu ili kwamba ni masanamu hayo tu ndiyo yatakayowasaidia kuwatetea wao; wao wanamwacha Allah swt  na badala yake wanakuwa na imani moja tu ya kuwaomba miungu na masanamu hayo kuwa watetezi wao.  Lakini ni uhakika uliyo bayana kuwa Waislamu kamwe hawawabudu Mitume a.s. au Ma-Awliya’ lakini wanayo imani kuwa kila kitu kinatoka kwa Allah swt. Sisi tunapenda kuwa hao ma-Awliya’ wawe ni Wasila wetu.  Makafiri wanaamini kuwa miungu na masanamu yao inawaombea chochote kile wakitakacho na kumfanya Allah swt kuwatimizia chochote kile wakitakacho.

 Wakati ambapo, Waislamu wanaomba msaada  wa Awliya’ ambao wanawajua kuwa hao ndio watumwa wapenzi  wa Allah swt, kwa sababu Allah swt ameahidi katika Qur’an tukufu kuwa Yeye atawaruhusu waja wake wapenzi kuwatetea na atakubali utetezi wao na Sala na kwa sababu Waislamu wanaamini ubashiri mzuri katika Qur’an. Kamwe huwezi kulinganisha baina ya kafiri anayeabudu miungu na masanamu na Waislamu wakiomba msaada wa Awliya’.  Waislamu na Makafiri wote ni binadamu  kwa  miili, na wanafanana kwa kuonekana, lakini Waislamu ni marafiki wa Allah swt na watakuwa Peponi milele wakati ambapo Makafiri ni maadui wakubwa wa Allah swt  na watakuwa Motoni milele.  Kujionesha kwao hakumaanishi kuwa watabakia vivyo hivyo daima.  Wale wanaowaabudu masanamu na miungu ambao ndio maadui wakubwa wa Allah swt, yatawafikisha hadi kuingia Jahannam. Lakini wale wanaowafanya marafiki wa Allah swt kuwa marafiki wao, basi Allah swt atawabariki na kuwarehemu.  Ipo Hadith isemayo: Rehema za Allah swt zinateremka pale waja wake wapenzi wanapotajwa, nayo pia inatuonyesha kuwa Allah swt ataonyesha rehema zake na misamaha yake pale Mitume a.s. na Awliya’  wanapoombwa.

Waislamu wote kwa pamoja wanatambua waziwazi kuwa Mitume a.s. na Awliya'  si watu wa kuabudiwa na wala si washiriki wa Allah swt.  Waislamu wanatambua vile vile kuwa wapo waja wa Allah swt ambao hawastahili kuombwa na papo hapo wapo waja wengineo ambao maombi yao hukubaliwa Kwake.  Katika surah Maidah, Ayah ya 35 tunaambiwa: “Tafuteni Wasila wa kunifikia Mimi” Allah swt anamaanisha kuwa Yeye atakubalia ibada za waja wake halisi na kuwapatia kile wakiombacho. Tunapata Hadith sharif iliyonakiliwa na al-Bukhari, Muslim na katika Kunuz ad-daqaiq, isemayo: “Kwa hakika, wapo wacha Mungu halisi wa Allah swt ambapo Yeye anawaumbia kile walacho kiapo; kamwe hawasingizii.” Waislamu wanawachukulia Awliya'  kama Wasila na kutegemea maombi na msaada wao kwa sababu wao wanaamini Ayah na hadith za hapo juu.

KUHITILAFIANA KATI YA FATUMAH BINT RASULULLAH NA SAYYDINA ABUBAKAR



Muda mfupi baada ya Abubakar kujinyakulia madaraka ya kuongoza Uislamu pale Saqifat Bani Saidah, Bi Fatumah alikwenda kwa Maanswar kuwaomba watekeleze maagizo ya Mtume kwa kumpatia baia Ally ibn Abi Talib, lakini Maanswar wakamwambia tayari tumekwishampa Abubakar na kwamba kama angekwenda mapema wasingempatia baia mtu yeyote isipokuwa Ally. Kwa hili Imam Ally anasema, “hivi kweli ni busara nimuache Mjumbe wa Allah nyumbani kwake bila kumzika ili tu nitoke kuja kugombana na watu juu ya cheo changu?” Fatumah naye akasema, “alichofanya Abul-Hassan ndicho kilichompasa kukifanya, na wao wamefanya jambo ambalo Mwenyezi Mungu atawauliza na atawalipa (kwa tendo la kupora madaraka).
Tazama: tarikh Al-Khulafaa cha ibn Qutaibah J. 1 uk. 19 na Sharh Nahjul Balagha cha ibn Abil Hadid (Baiatu Abubakar).
Kwa dhuluma aliyoifanya Abubakar na wenziwe dhidi ya Ahlulbayt wa Mtume, Bi Fatumah alimchukia Abubakar kiasi kwamba alipokufa aliagiza Abubakar asihudhurie mazishi yake na wala asijue kaburi lake lilipo. Hivyo Mmewe alimzika bibi huyo usiku na mpaka leo hakuna kauli moja inayoonesha kaburi la bi Fatumah lilipo.
Tazama: sahihi Bukhar J. 3 uk 36, na Sahih Muslim J. 2 uk. 72
Hivyo utagundua kuwa bibi huyo mtukufu ambaye Mtume alimtangaza kuwa mmoja wa wanawake bora zaidi ulimwenguni akiwa kati ya wanawake bora wane tu, alihitaji mazishi yake liwe fundisho kwa waislamu ili wajiulize kuna kitu gani kilitokea baina yake na watawala wa zama hizo. Na kwa hakika tumekwisha jiuliza na kujuwa hujuma uliza fanyiwa ewe mama wa Makhalifa na maimamu watukufu.

MAANDIKO YANAYOHUSU UKHALIFA



Ukichunguza kwa makini Hadith za Mtume utakuta kuwa ukhalifa wa Imam Ally uko wazi kabisa na haupingiki.  Ebu soma hadith ya Mtume ifuatayo:
Yeyote ambaye mimi nikuwa mtawala wa mambo yake, basi huyu Ally naye ni mtawala wake.
Maneno haya aliyasema Mtume wetu baada ya kutoka katika Hijjah ya kuaga kiasi kwamba yalifanyika maandamano ya kumpa Imam Ally mkono wa kuonesha utii kwake (baia). Abubakar na Umar walikuwa miongoni mwa watu waliotoa pongezi kwa Imam Ally kwa kutangazwa kuwa kiongozi wao, wakisema, “Hongera ewe mwana wa Abu Talib, leo umekuwa mtawalia mambo kwa kila muumini wa kike na kiume”.
Tazama:
1.      Musnad Imam Ahmad ibn Hambal Juz. 4 uk. 281
2.      Sirul – Alamina cha Imam Ghazal uk 12
3.      Tarikh Ibn Asakir juzuu.2 uk. 50
4.      Ar-Riyaz Un-Nazrah cha Tabari juzuu. 2 uk. 169
5.      Kanzul Ummal juzuu.6 uk. 397
6.      Al-Bidaya wa-Nihaya cha Ibn Kathir j. 5 uk. 212
7.      Al-Hawi Lil-Fatawi cha Suyut j.1 uk. 112
Ama ile ijmai (makubaliano) inayodaiwa kuwa ilimchagua Abubakar pale Saqifah, kisha kumpa baia Msikitini haina ushahidi wa kutosha  kwani Masahaba wengi tu walipinga na baadhi yao ni: Ali, Abbas na banu Hashimu wengine, Usama bin Zaid, Zubair, Salman Farsii, Abudhar Ghiffar, Miqdad bin Aswad, Ammar bin Yasir, Hudhaifa ibn Yaman, Khuzaimah ibn Thabit, Abu Buraidah Aslam, Al-Barraa ibn Azib, Ubay ibn Kaab, Sahl ibn Hunaif, Saad ibn Ubadah, Qais ibn Saad, Abu Ayub Answar, Jabir ibn Abdillah na Khalid ibn Said.
Tazama: Tarekh Tabari, Tarith ibn Al-Athir, Tarikh Al-Khulafa, Tarikh Al-Khamis, Al-Istiiabu na kila aliyeandika kuhusu baia ya Abubakar.
Bila shaka Umar bin Khatab alishuhudia mwenyewe kuwa baia ile ilikuwa ya ghafla, Mwenyezi Mungu aliwakinga waislamu na shari yake, na akaendelea kusema, “Yeyote atakayerudia kufanya baia kama hiyo muuweni” na mahala pengine akasema, “yeyote mwenye kufanya kampeni kama hiyo asipewe baia wala Yule aliyembai”.
Tazama: sahihi Bukhar J. 4 uk. 127
Naye Saad ibn Ubadah, kiongozi wa Maanswar aliwapinga katika kampeni yao pale Saqifah kiasi kwamba alikuwa hasali pamoja na Abubakar na Umar, au nyuma yao wala hafuatani nao katika Arafah. Alibakia hivyo mpaka alipokufa huko Shamu katika ukharifa wa Umar bin Khatab.
Tazama; Tarikh Khulafah J. 1 uk. 17.
Kwa hiyo kauli ya Mashia kuhusu Ukhalifa ndio sahihi, kwani imethibiti kupatikana kwa maandiko juu ya ukhalifa wa Imam Ally kwa masunni wenyewe, na wameyafanyia taawili ili kulinda heshima ya masahaba, lakini kwa mtu muadilifu hana njia ya kukwepa, isipokuwa kukubali maandiko hayo, na hasa pindi atakapotambua utata uliomo ndani ya jambo hili.
Tazama: Saqifah wal-Khilafah cha Abdul-Fatah Abdul Maqsud na As-Saqifah cha Sheikh Muhammad Ridhaa Mudhafar. 

MAONI YA QUR’AN KUHUSU MASAHABA WA MTUME



Assalaam alaykum. Kwanza kabisa ninachukua nafasi hii kuwashukuru Masahaba wa Mtume waliokuwa wema na waliomsaidia katika ujumbe wake bila kuwa na ajenda za siri dhidi ya Uislamu. Bila shaka Qur’an imekuja na aya nyingi kuwasifu Masahaba hawa. Pamoja na kuwa na Masahaba wema, wapo vile vile Masahaba waliokuwa si wema na Qur’an imewalaumu katika aya zifuatazo:
1.      Na Mohammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwishapita kabla yake mitume wengi. Je, akifa au akiuawa ndio mtageuka kurudi nyuma (kurtadi)? Na atakayegeuka na kurudi nyuma hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Na Allah atawalipa wanaoshukuru (Qur’an 3:144).
2.      Wachache katika waja wangu ndio wenye kushukuru (Qur’an 34:13).
3.      Enyi mlioamini mna nini mnapoambiwa: Nendeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia ni chache kuliko za akhera. Kama hamuendi atakuadhibuni adhabu chungu na atawaleta watu wengine wala ninyi hamtamdhuru chochote, na Allah ni Muweza wa kila kitu (Qur’an 9:38-39).
4.      Na mkirudi nyuma, (Allah) atabadilisha (alete) watu wengine wasiokuwa ninyi kisha hawatakuwa kama ninyi (Qur’an 47:38).
5.      Je, haujafika wakati kwa wale walioamini, nyoyo zao zinyenyekee kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kwa mambo ya haki yaliyotelemka, na wala wasiwe kama wale waliopewa kitabu hapo kabla na muda wao (wa kuondokewa na Mitume) ukawa mrefu, kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu na wengi wao wakawa waasi (57:16).
6.      Na wawepo miongoni mwenu watu wanaolingania wema na kukataza maovu, na hao ndio watakaotengenekewa. Na wala msiwe kama wale waliofarikiana na kukhitilafiana baada ya kuwafikia dalili zilizo wazi, na hao ndio watakao kuwa na adhabu kubwa. Siku ambayo nyuso zitanawiri na nyuso zingine zitasawajika, wataambiwa: je mlikufuru baada ya kuamini kwenu? Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyokuwa mnakufuru. Ama wale ambao nyuso zao zitanawiri watakuwa katika rehema ya Allah. Wao humo watakaa milele (Qur’an 3: 104-106)
Ndani ya kitabu kiitwacho Ad-Durul Manthur cha Jalaludin As-Suyut imeandikwa: Pindi Masahaba walipofika Madina, wakapata maisha mazuri ambayo hawakuwa nayo kabla, wakazembea kutenda baadhi ya wajibu waliokuwa juu yao, hivyo wakakemewa kwa aya ya 5 iliyotangulia hapo juu.
Na katika riwaya nyingine itokanayo na Mtume Mohammad inasema kuwa Allah aliziona nyoyo za Muhajirina kuwa ni nzito (hata) baada ya miaka 17 ya tangu kushuka Qur’an, basi akateremsha kauli yake, “Je haujafika wakati kwa wale walioamini?
Aya hizi zinaonesha wazi kuwa kuna masahaba ambao hawakuwa wanyenyekevu mbele za Mwenyezi Mungu na Mtume wake, vinginevyo Mwenyezi Mungu asingewalaumu au kuwashauri wabadirike tabia zao.
Ama suala la Masahaba kukhitilafiana sidhani kama kuna mtu anaweza kupinga na kudai kuwa hawakukhitilafiana kwani walifikia mahala pa kupigana vita wao kwa wao. Mfano Sayyidina Uthuman aliuwawa na kundi la Masahaba. Imam Ally (a.s) akiwa na alipigana vita na kundi la Masahaba kama Aysha, Zuberi na Twalha. Vile vile alipigana vita na Muawiyyah bin Abusufian ambaye naye alikuwa sahaba wa Mtume.
Haiwezekani kwa makundi haya yenye kupigana kwamba yatakuwa yote katika haki. Hivyo kuna ulazima wa kutafuta haki iko wapi kabla ya kuliunga mkono kundi lolote miongoni mwa haya.
Kumbuka Mtume anasema pale watapokhitilafiana watu, tafadhali shikamaneni na Imam Ally kwani haki iko pamoja naye daima. Kwa mantiki hii kundi linalomfanya Imam Ally kuwa kiongozi wao wa kwanza baada ya Mtume kufariki tu huenda litakuwa katika njia sahihi zaidi. Kwani muda mfupi baada ya Mtume kufa ndio vurugu zilipoanza. Utakumbuka Sayyidna Umar alipotangaza kuwa Mtume hajafa hadi wakafiri waishe na kwamba atakayesema kuwa Mtume kafa atamkata kichwa. Hii sio imani ya kiislamu na khitilafu zilianzia hapa.

Friday, 23 August 2013

MASAHABA KATIKA JESHI LA USAMAH



Mtume Mohammad (S.A.W.W) aliandaa jeshi ili kulikabiri jeshi la Rumi siku mbili kabla ya kifo chake na akampa uamiri Usamah bin Zaidi ibn Harith, aliyekuwa na umri wa miaka 18. Katika jeshi hilo Mtume aliwaamrisha wakuu wa Muhajirina na Answar kama vile Abubakar bin Quhafah, Umar, Abu-Ubaidah kujiunga na jeshi hilo. Miongoni mwao wapo waliopinga uamiri wa Usamah na wakasema, itakuwaje tuongozwe na kijana ambaye bado hajakomaa?
Hivyo Mtume alitoka akiwa mgonjwa na amefungwa kitambaa kichwani akiyumba kati ya watu wawili akapanda juu ya mimbari na kusema, “Enyi watu ni maneno gani yanayonifikia kutoka kwa baadhi yenu kuhusu uamiri wa Usamah, basi ikiwa mtakebehi kwa kumpa kwangu uamirijeshi Usamah, kwa hakika mlikwisha kebehi kumpa kwangu uamiri baba yake kabla ya mwanawe. Basi namuapa Mwenyezi Mungu kwa hakika Zaid alistahili kuwa amiri na mwanaye pia anastahili kuwa amiri baada yake.
Tazama:
1.     Taqabat cha ibn Saad Juz. 2 uk. 190
2.     Tarikh Ibn al-Athir juz. 2 uk. 317
3.     Tarikh At-Tabari Juz. 3 uk. 226
4.     As-Siratul Halabiyyah ju. 3 uk. 207
Kisha Mtume akawa anawahimiza wafanye haraka kwenda kuungana na jeshi la Usamah ili kuindinda nchi. Lakini mpaka Mtume anafariki Masahaba wengi wakiwemo Abubakar na Umar walikuwa hawajajiunga na jeshi la Usamah, vinginevyo wasingekuwapo Madinah wakati Mtume alipofariki.
Ukweli wa tukio hili ni kuwa kwa mara nyingine tena Baadhi ya Masahaba walipinga amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Rejea Qur’an 33:36 na 59:7 upate maelekezo ya Mwenyezi Mungu juu ya kumtii Mtume wake.
Ikiwa tutataka kufanya mazingatio katika kisa hiki tutagundua kuwa Khalifah Umar bin Khatab ndiye chimbuko la upinzani huu kwani baaada ya kifo cha Mtume alikwenda kwa Khalifah Abubakar na akamtaka amuuzulu Usamah na kumbadilisha na kuweka amiri mwingine. Abubakar akamwambia, “mama yako amekula hasara ewe mwana wa Khatab, waniamuru nimuuzulu na hali ya kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alimtawalisha?”
Tazama:
1.     Taqabat al-Qubra cha Ibn Saad juz. 2 uk. 190
2.     Tarikh At-Tabari juz. 3 uk. 226