Wizara ya Kawi nchini Kenya imesema itaendelea kununua mafuta ghafi
kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran licha ya vikwazo vya upande mmoja vya
Marekani na Umoja wa Ulaya dhidi ya sekta ya mafuta ya Tehran.
Katibu
wa Kudumu wa wizara hiyo, Patrick Nyoike amesema kuwa serikali za
Nairobi na Tehran zilitiliana saini mkataba kuhusu biashara ya mafuta
mwezi uliopita na ameongeza kwamba Kenya itanunua tani milioni 4 za
mafuta ghafi ya Iran kila mwaka. Nyoike hata hivyo hakutoa maelezo zaidi
kuhusu mkataba huo kati ya nchi hizo mbili.
Hii ni katika hali
ambayo Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya zilianza kutekeleza vikwazo
vya mafuta dhidi ya Iran hapo jana Julai 1 kama njia ya kuishinikiza
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran isimamishe miradi yake ya kuzalisha nishati
ya nyuklia yenye malengo ya amani. Tehran imesema vikwazo hivyo
havitakuwa na athari kwa uchumi wake bali nchi za Ulaya zinazokumbwa na
mtitigo wa kiuchumi ndizo zitakazoumia kutokana na kupanda bei ya mafuta
katika soko la kimataifa.
No comments:
Post a Comment